Kikwete: Tatizo la maji Dar kubaki historia

Kikwete: Tatizo la maji Dar kubaki historia

Nimefungua post haraka haraka ili nione hiyo mipango ya kumaliza tatizo la maji Dar kumbe ni usanii wa mkulu wakati akitafuta tiketi ya kuongezewa muda wa ulaji.

Nimechoka kabisa.

Tiba

Mimi nimekuja mbio nikifikri jamaa katoa ahadi mpya maana hachelewi, juzi kaahidi elimu bure mwaka 2016 kama vile anayekuja ni R1 kiasi kwamba atakuwa akimwamrisha kijana wake!! Huyu kwa kikwetu huwa tunawasema "Bukulu w'isindi kugaya ndete" Yaani boga kubwa lakini linakosa mbegu. Hii ni nahau iliyowahusu watu ambao vichwa vyao havina akili!!
 
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amesema tatizo la maji mkoani Dar es Salaam litabaki kuwa historia kuanzia mwaka mmoja ujao, kwani mikakati kabambe imewekwa kwa ajili ya kuongeza vyanzo vya maji.

Vile vile, ameahidi kuzipandisha hadhi zahanati zote za jijini Dar es Salaam kuwa vituo vya afya na hospitali ya Amana kuwa ya rufaa.

Alitoa ahadi hizo jijini Dar es Salaam jana wakati wa mikutano yake ya kampeni katika maeneo ya Kiwalani, Kitunda na Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.

Alisema chanzo cha maji hivi sasa Ruvu Juu kinatoa lita 60,000 kwa siku na Ruvu chini lita 90,000 kiasi ambacho hakitoshelezi mahitaji ya maji jijini Dar es Salaam.

Kikwete alisema mahitaji ya maji ni lita 360,000 kwa siku hali iliyosababishwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu kulinganisha na miaka ya nyuma.

Alisema kwa msaada wa watu wa Marekani, Serikali inaendelea kupanua Ruvu Chini ili iweze kuzalisha kiasi kikubwa cha maji.

Alisema wakati Serikali ikiendelea na mkakati wake wa kupanua vyanzo vya maji, chanzo kingine cha maji kimegundulika Kimbiji kutokana na utafiti uliofanywa na wataalamu wa Norway.

“Watu wa Norway waliniambia Kimbiji imejaa maji mimi nikawauliza hayo si mafuta jamani wakaniambia hapana ni maji, na wakanionyesha mchoro kweli ni mengi kama nusu ya yaliyoko Ziwa Victoria,” alisema.

Alisema katika uzalishaji huo yatapatikana maji lita 260,000 kwa siku ambazo zikiunganishwa na zile zinazopatikana katika vyanzo vingine yatakuwa yanatosheleza mahitaji ya Dar es Salaam.

Aidha, alisema awali wataalam wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) na Dawasco, walimweleza kuwa mpango huo unaweza kukamilika ndani ya miaka mitatu.

“Waliponiambia kuwa mradi huo utakamilika ndani ya miaka mitatu, nikasema hapana lazima tuangalie namna ya kuukamilisha mapema, nikasema visima apewe mkandarasi mwingine, ujenzi wa matenki mkandarasi mwingine na usambazaji wa mabomba makubwa ya kuleta maji Dar es Salaam, apewe mkandarasi mwingine na nina uhakika tutakamilisha mapema,” alisema Kikwete.

Alisema mtandao wa zamani wa mabomba ambao umechakaa unaondolewa na kuwekwa mpya kazi hiyo inafanywa kwa msaada wa Serikali ya Watu wa China.

Kuhusu barabara, alisema Serikali itaendelea kuongeza fedha katika mfuko wa barabara ili nyingi zijengwe kwa kiwango cha lami.

Alisema katika kuondoa msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, Serikali itazijenga barabara za pembezoni kwa kiwango cha lami ili watu wote wasilazimike kwenda mjini kwa kutumia barabara moja.

“Tunataka mtu akitoka Morogoro anakuja huku asilazimike kwenda hadi Buguruni, akifika Kimara kule anakunja kulia anakuja huku kwa kutumia barabara nyingine, na yule aliyeko Tegeta akitaka kwenda Morogoro asilazimike kwenda hadi Ubungo apitie kule kule,” alisema Kikwete.

Kuhusu barabara ya Mombasa Kivule, alisema kinachosubiriwa ni watu waliojenga kando kando ya barabara hiyo walipwe fidia na kisha ijengwe kwani fedha za ujenzi zipo.

Aidha, alisema serikali itaendelea kuiongezea uwezo Vyama vya Kuweka na Kukopa (Saccos) ili viweze kukopa zaidi kwenye taasisi za fedha na kukopesha wanachama wake wafanye biashara na kuondokana na umaskini.

Rais Kikwete aliitumia mikutano hiyo kujibu kauli zilizotolewa na wanasiasa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, dhidi yake.

Kikwete alisema kuwa mashambulizi ya Chadema dhidi yake ni dalili za hofu ya kushindwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.

Chanzo: NIPASHE

Tupime, tujadili kuna muelekeo wa hayo yaliyoahidiwa?
Hata umeme imebaki hadithi ya bibi
 
Alisema chanzo cha maji hivi sasa Ruvu Juu kinatoa
lita 60,000 kwa siku na Ruvu chini lita 90,000 kiasi ambacho hakitoshelezi mahitaji ya maji jijini Dar es Salaam.

Kikwete alisema mahitaji ya maji ni lita 360,000 kwa siku hali iliyosababishwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu kulinganisha na miaka ya nyuma.

Alisema katika uzalishaji huo yatapatikana maji lita 260,000 kwa siku ambazo zikiunganishwa na zile zinazopatikana katika vyanzo vingine yatakuwa yanatosheleza mahitaji ya Dar es Salaam.

Khaa!!! Mahitaji ya jiji ni lita 360,000/= Kwa jicho la kisayansi (lisilo na chembe ya kisiasa) haya maji hayatoshi hata kusafishia meno. Kwani ni sawa na ndoo 18,000. Kwa idadi ya wakazi wa Dar ambao ni takriba 4,000,000 kila mmoja atapata mililita 90 ambayo hata kikombe cha chai hakijai. Hapo bado hajaoga, hajafua na wala viwanda vya bia havijachota!! Rais wetu kadanganywa na wataalam wake!:angry:
 
dhaifu squared

Anapoondoka madarakani tatizo la.maji ni mara elfu moja kuliko alipoingia madarakani. Halafu bila chembe cha aibu anatangaza elimu ya bure kwa.serikali itakayokuja wakati yeye akiwa msoga akichunga mbuzi. Sijui hao washauru wake ni akina nani. Shame on them.
 
Yatakua makosa ya mwandishi labda....
Sahihi ni mita za ujazo na sio lita!

Khaa!!! Mahitaji ya jiji ni lita 360,000/= Kwa jicho la kisayansi (lisilo na chembe ya kisiasa) haya maji hayatoshi hata kusafishia meno. Kwani ni sawa na ndoo 18,000. Kwa idadi ya wakazi wa Dar ambao ni takriba 4,000,000 kila mmoja atapata mililita 90 ambayo hata kikombe cha chai hakijai. Hapo bado hajaoga, hajafua na wala viwanda vya bia havijachota!! Rais wetu kadanganywa na wataalam wake!:angry:
 
Yatakua makosa ya mwandishi labda....
Sahihi ni mita za ujazo na sio lita!

Sure! Kwa mita za ujazo 360,000 ni sawa na lita 360,000,000 gawanya kwa wakazi m.4 wa Dar kila mkazi roughly atapata lita 90 (ndoo nne na nusu za lita 20) something realistic.

Hata hivyo, hoja ya msingi ni tungependa kujua tatizo la maji Dar/Ubungo linaletwa na John Mnyika au na nani kama hawa Ritz, ifweero, MwanaDiwani, Simiyu Yetu, mjepo, et. al. wanavyoshadadia kila uchwao?
 
  • Thanks
Reactions: RR

Jamani tatizo la maji haliko Ubungo tu. Ni almost Dar es Salaam nzima haina maji. Maeneo ya city centre bila aibu DAWASCO wanadai hakuna maji kwa kuwa mabomba ya alminium yameziba. Lakini wao ndio wauzaji wakubwa wa maji kwenye maboza. Hakuna maji Dar.
 
Back
Top Bottom