zikiwa zimebaki siku chache tu watanzania tuingie kwnye uchaguzi mkuu wa 2015 uchaguzi ambao utamaliza mvutano wa wapiga kura kati ya wale wanaotaka mabadiliko Nje CCM na wale wanaotaka mabadiliko Ndani ya CCM, ninalazimika kumgeukia Rais wetu wa jamhuri ya muungano wa tanzania na kugundua kwamba ni Rais bomba wa karine hii, nalazimika kusema hivyo kwa vile wakati vyama vikiwa ktk shamrashamra za kampeni zenye mvutano wenye kutishia uhai wa chama tawala kung'oka madarakani, lkn yeye kama mwenyekiti wa chama hajapunguza speed yake ziara za nje, hajapunguza tabasamu lake usoni kwenye baadhi majukumu yake, tumeshuudia Rais akiwaaga Majaji, tumeshuudia akiwaaga wanajeshi na kuwapandisha vyeo, tumeshuhudia akiwachagua viongozi kadhaa kwa kipindi hiki kifupi kilichobaki,
ni ukweli usiopingika kwamba ktk Inchi nyingi za africa watawala wanakuwa wakali na wavunjaji wa sheria kwa kipindi kama hiki,
Kwa maana hiyo nalazimika kumsifu JK kwa vile ni Rais ambae ameshasoma alama za nyakati na kugundua kwamba Tanzania bila CCM inawezekana, na hataki kutumia nguvu kwavile wote wanaogombea wana uwezo wa kulisukuma gurudu la taifa hili,
hongera Rais Jk mungu akupe maisha marefu