Kihistoria siku za ukoloni mkoa wa Iringa ulikuwa moja ya source ya manamba kwenye kanda zinazozalisha zao la Mkonge ambao kwa kwakati huo Tanganyika ilikuwa jabali namba one duniani kwa uzalishaji wa mkonge. Na wengine walivuka bahari hadi Unguja kulikostawishwa zao la karafuu na kuwa supplier number one duniani.
Kwa vyo vyote uzi wa koo nyingi za mwambao kuunganika na za ukanda wa nyanda za juu na sehemu nyingine nchini si za kusadikika tu, bali ni source za uhakika. Majina kama Kombo utakuta wengi tu huko Iringa nk. Hakuna sababu ya kushangaa au kupinga wakati tunajua karne iliyopita na kurudi nyuma jamii hazikuwa za kusetirika, uhamaji ilikuwa jambo la kawaida kama tufanyavyo siku hizi kwa sababu mbalimbali ikiwemo uchumi, uhasama, vita, na mengineyo.
Yusuf Makamba kuna walioniambia kuna ukoo wake huko Ludewa tarafa za Mlangali na Mawengi ambako ziko koo za akina makamba, ni warefu na weupe kadiri ya mmoja mtafiri alivyonipa data, ila si vizuri kuziweka taswiras hapa kwa vile zinagusa privacy ya watu.
Kipindi cha awamu ya kwanza, kuna baadhi ya jamii zilituhumiana kuhusu baadhi yao kuwa ni wachawi wanaowadhuru. Utawala wa Nyerere uliamua kuwanusuru watu hao kutouawa, na hivyo kuwahamishia sehemu nyingine na kuwa kijiji chao peke yao wanaotuhumiwa kwa uchawi, maana wakikaa wachawi peke yao vigumu kuchawiana. Kuna kijiji fulani moja wapo mkoani Dodoma walikohamishiwa, ila sipendi kukiandika hapa maana baadhi ya waheshimiwa serikalini wanatokana na jamii hizo nisije mwagiwa tindikali.
Tuendelee kujadili.