Wakazi wa asili kabisa wa Bagamoyo ni kina nani?. Wengi wa hao waliopo ni masalia ya watumwa wenye afya duni walio chukukuliwa bara na kutelekezwa hapo sokoni Bwagamoyo hivyo kuloweya hapo.
Kama jamaa wamethibitisha Kikwete ni jina la Iringa, then wako right kabisa.
Kitu ambacho tusikifanye ni kuzishauri jamii zetu zirejee kwenye asili zao. Wangoni warudi kwao Zulu land baada ya kuletwa nchini na Zongendamba. Wayao nao warudi kwao utawala wa Mwanamutapa. Waarabu wa Unguja na Pemba warudi kwao Oman baada ya kuletwa na Sultan Sayed Said.
Wachaga Wamasai na Wameru warudi kwao Kenya. Wahaya na Waangaza warudi kwao Baganda Kingdom. Kigoma warudi kwao Zaire. Wamakonde warudi kwao Msumbiji, Wanyasa warudi kwao Malawi, Makabila ya Mara warudi kwao Kenya.
Kwa kifupi wenyeji wa asili wa Tanganyika ni bantustans wa Tanganyika, Wasukuma na vizalia vyake, Wagogo, Wahehe, Waluguru na vizalia vyao. Makabila ya Singida na Arusha kama Warangi, Wasandawe, Wabarbaig, Wahadzabe etc, hapa sio kwao, hawa si wabantu ni semi nilotic ambao hutanga na nyika kutafuta survivor hivyo kujijuta Tanganyika.
Maadam tulipopata uhuru wetu ile Desemba 1961, Katiba iliwatambua wale wote walio kuwepo kwenye ardhi ya Tanganyika kuanzia ile saa 6 usiku wa uhuru ni Watanzania halali.