Kikwete: Ni bora Slaa awe Rais kuliko Tundu Lissu kuwa mbunge

Binafsi nimewahi pambana na Lissu ningali kiongozi wa idara fulani serikalini enzi za Ben.

Niseme tu Lissu ni wa tofauti sana linapokuja suala la kupigania anachokiamini.

Wangekua ni watu wengine angeunga juhudi tangu enzi za Ben kwa offer alizokua akipelekewa akazikataa.
 
Lissu ni tofauti na wapinzani wengine akiwemo Dr Slaa. Hajawahi kuwa mwana-CCM na sidhani kama atahamia huko. Dr Slaa alikuwa CCM kabla ya kuhamia upinzani na kurudi tena CCM.

JK na wana-CCM wengine walijua wazi kuwa Lissu ni mpinzani wa kweli. Historia yake dhidi ya serikali hasa miaka ya 90 iko wazi, sema wengi wanamjua Lissu alipojiunga na siasa.

Ni rahisi "kuwanunua" wanasiasa wa upinzani lakini siyo Lissu. You will be fighting a losing battle. Hanunuliki kwa bei yoyote ile. Mbaya zaidi the guy knows his stuff na hapindishi.

Haya na mengine ni baadhi tuu ya mambo yaliyomfanya JK aseme vile. Kwa kifupi, kama upinzani ungekuwa na Lissu 15 hivi bungeni CCM ingekuwa katika hali mbaya sana.

Nadhani hata kwa sasa CCM would be happy Lissu agombee urais ambao kwa hali ya kisiasa nchini hatashinda kuliko kugombea ubunge ambao angeshinda na kuwachefua tena bungeni.
 
Kwa mazingira yaliyopo sasa upinzani kushinda urais ni sawa na ngamia kupenya katika tundu la sindano.

CCM siyo wajinga hivyo. Wanajua nini kitatokea kama Lissu atakuwa rais. Hata kama atapata kura nyingi, CCM watakuwa radhi kushinda hata kwa "goli la mkono".

Bahati mbaya hatuna independent VAR to reviews NEC decisions, so it will be up to the wananchi, who I don't think they empowered to demand signicant change of the current system.

Don't just sit there hoping that "A Man of the People" will come and save you. That is idealistic. Unless we change our mentality first, CCM is here to rule us as much as they want.

Samahani this is something you didn't want to read, but I am saying the state of things as they actually exist at the moment.
 
Well just sit there and wait for God to come and save you then. Haya mambo ya kumtegemea Mungu ashuke kuleta mageuzi ndo yatakuponza. Unaimba wimbo uleule anayeimba aliye madarakani.
 
Sawa Mkuu all the best, but it's crystal clear that kwa mazingira ya sasa ni vigumu sana kwa upinzani kushinda uchaguzi.

Huwezi kulinganisha siasa za Malawi na Tanzania. Ni tume ipi ya uchaguzi au mahakama iliyo na udhubutu wa kubatilisha matokeo ya urais wa CCM kwa mfano?
 
Kwanza sifa namba 1 ya kiongozi bora ni kusimamia unachokiamini ili usiwayumbishe unaowaongoza. Pili je misimamo yake imemsaidia? Jibu kwa maoni yangu ni ndiyo, imemsaidia yeye plus wengi aliowahi kuwatetea kupitia taaluma yake, pamoja na kwamba imemtia kwenye misuko suko mingi sana kwenye maisha yake. Sisi binadamu tuko tofauti sana, kuna baadhi yetu hatutaki kabisa purukushani, alimradi tuu mkono unaenda kinywani, hata kama jirani yako anateketea kwa maovu anayofanyiwa wewe ukiona. Kuna wengine, kamwe roho yake haiwezi kutulia mpaka aone hali imetendeka kwa jirani au hata mtu asiyemhusu.
 
Agreed. Kenya waliamua b'se they wanted a change. Changes come with risks. You have to take risk kama unataka mabadiliko ya kweli. Kenya went through a tough time, but in the end walipata walichokitaka. Sasa sie Watanzania tunataka change bila ku-take risks.



Mungu atawapatia hiyo fursa only if they work off their arses. Wakikaa kimya tuu huku wakimwomba Mungu awaletee mabadiliko, that will never happen. Hukunaga ushindi wa mezani.

The biggest problem Tanzanians do not want to make positive changes in their lives is fear. Fear of the unknown, fear of persecution, fear of alienation and so on. Ndo maana wanamtegemea Mungu. Tena yaliyomtokea Lissu na wengine yameongeza woga kwa wengi.

Halafu kuna kundi la watu ambao wako so comfortable na maisha yao. They don't want to take the risk even if change could be positive. Pia nilishawahi kuandika hapa kuwa sie wabongo tumekuwa programmed. Nyerere alifanya mengi mzuri lakini pia alitufanya tuwategemee sana wanasiasa. Tumewafanya wanasiasa wajione kama miungu vile.

Halafu tuna watu walioelimishwa au kulazimishwa kuamini kuwa their negative belief systems are correct and do not need to be changed. These people are known as delusional or brainwashed. They don't entertain a second opinion.

Then, we have people with ego who believe that they are beyond the need for any change whatsoever.

It's sad that kila baada ya miaka mitano tuna-recyle hoja za upinzani kushinda but nothing happens b'se wapiga kura wenyewe hawajabadilika. They still have the same mentality and level of thinking. But they are expected to bring political change. How?

Mfano, tafuta threads za nyuma kama ile ya mwaka 2010/11 aliyoanzisha Masanilo inayosema: Mapinduzi yaja Tanzania. Wengi walisema kuwa upinzani ungeshinda. They didn't. Thread iliendelea mpaka 2015 still wakasema upinzani watashinda. They didn't.

Leo 2020 bado wanadhani upinzani utashinda. It's like doing the same thing and expecting different results. Lissu atachangamsha uchaguzi kama alivyofanya Dr Slaa na Lowassa but mazingira ya kisiasa nchini bado ni yale yale or probably worse for the opposition to win a presidential election.
Kweli
 
I am not sure kama nimekuelewa au umejibu point yangu. Sina lolote baya dhidi ya Lissu professionally au kisiasa. I think he is a strong person given what he went through. Maana wapo waliopigwa mkwara wa maneno tuu wakahamia CCM.

My point is that pamoja na mazuri yote ya Lissu and what he brings to the table, mazingira ya kisiasa kwa sasa hayawezeshi upinzani kushinda uchaguzi wa urais. Hata kama Magufuli angehamia upinzani leo na kugombea asingeweza kumshinda yoyote atakayesimamishwa na CCM. Huu ni uhalisia ila mchungu.



Utavuka salama kwa kuchukua hatua za kujilinda mwenyewe. Tuache kumbebesha Mungu matatizo yetu.
Hakika
 
Kwa wale waliobahatika kusoma gazeti la Mwanahalisi la leo kwenye kichwa cha habari nanukuu" Askofu huyu katumwa na nani?" mwaandishi kaandika kuwa kikwete alinukuliwa kwenye mikutano yake ya kampeni huko Singida kuwa

"Ni bora Dr Slaa kuwa raisi kuliko Tundu Lissu kuwa mbunge" hii hofu ya Muungwa kwa Tundu Lissu inatokana na nini?

======

Askofu huyu katumwa na nani?

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 10 November 2010

ASKOFU wa Kanisa Katoliki anategemewa azungumze mambo ya maadili na imani. Anatarajiwa afundishe mafundisho ya kanisa, yasiyoegemea upande wowote wa kisiasa kwa kuwa yeye ana waumini wa vyama mbalimbali katika kanisa lake analoliongoza.

Katika uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani uliomalizika hivi karibuni hali imekuwa tofauti.

Uchaguzi umepita, walioshinda wanafurahia mitaani, walioanguka wanasikitika; yote hayo ni maamuzi ya wananchi na yanapaswa kuheshimiwa.

Katikati ya shangwe, wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki walitumiwa ujumbe kupitia mbunge wao, Tundu Lisu. Ujumbe huo ulitoka kwa mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya, unaomtaka mbunge huyo mteule aache kufurahia ushindi kwa nguvu, na kupeperusha bendera huku akipita na vipaza sauti.

Sababu? Eti kwa kufanya hivyo anawaumiza wale walioshindwa. Huku ni kupotosha maana ya mashindano.

Hakuna shida. Tatizo ni kwamba waliotuma ujumbe huo ni viongozi wa serikali, yaani mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya – Singida.

Mbaya zaidi aliyetumwa kuwasilisha ujumbe huo ni kiongozi wa Kanisa Katoliki mkoani humo, yaani askofu. Tunashindwa kuelewa.

Ilikuwaje mkuu wa mkoa, na mkuu wa wilaya wamtume askofu huyo kumwambia mbunge wetu maneno hayo? Hakukuwepo na watu wengine wa kutumwa katika ofisi ya viongozi hao wa serikali ila atumwe kiongozi huyo wa kiroho?

Na kwanini kiongozi huyo wa dini alijishusha sana kiasi cha kutumwa kazi kama hii isiyo na tija kwa kanisa? Na alikubali kuifanya kwa maslahi ya nani? Kwa ajili ya nini?

Askofu ananukuliwa akimwambia Lissu kwamba K"wa kuwa umepata ulichokuwa unatafuta usiwahamasishe wananchi waache kuchangishwa." Loo!

Mojawapo ya sera zilizomwongezea umaarufu Lissu katika kampeni zake ni kuzuia michango yote haramu, ukiwemo wa sekondari. Hoja ya Lissu ni kwamba mchango huo ni haramu kwa kuwa haukupitishwa kisheria na bunge.

Lisu amekuwa akihoji kuwa pesa nyingi zinazotengwa na serikali hazifiki kwa wananchi kujenga shule, hivyo anataka serikali iwajibike kujenga shule hizo kwa pesa za kodi badala ya kuwatoza wananchi michango ambayo imekuwa ikiwanufaisha wachache.

Lissu amekuwa mkali pia kwa vizuizi vinavyowekwa barabarani kukusanya ushuru wa mazao, kwani upo kinyume. Sheria ya serikali za mitaa liyofuta ushuru wa mazao ilitolewa kupitia tangazo la serikali Na 231, la tarehe 3/5/2002, wakati huo Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi akiwa waziri mwenye dhamana.

Sasa Bunge hadi sasa halijatunga sheria nyingine tofauti na hiyo, hivyo kuonekana kuwa serikali imewaibia Watanzania michango na au ushuru haramu kwa miaka minane.

Hayo ndio madai ya mbunge huyu machachari. Lakini askofu huyu ameenda kumshauri aache kuzungumzia ajenda hizi. Inakuwaje askofu anapokuwa anapenda wananchi wake kutozwa ushuru isivyo halali? Askofu anatumia gari yake inayolipiwa mafuta kwa sadaka za wakristo toka Singida mjini hadi Dungâ€unyi kwa Tundu Lissu kueleza mawazo mepesi haya.

Njia nzima Roho Mtakatifu hakumshukia askofu huyo amshauri tofauti? Wananchi wa Singida wamekuwa wakisikitishwa na baadhi ya dhuluma zinazoonekana kufanywa na viongozi hao waliomtuma.

Wananchi wamedhulumiwa mashamba katika mradi wa umeme unaotarajiwa kuanza, wananchi wameendelea kunungâ€unikia kuuzwa kwa majengo ya Chama cha Ushirika mkoani (SIRECU), wananchi wameendelea kushuhudia mikataba tata ya kifisadi katika jengo la utamaduni lililopo mjini Singida.

Wananchi wamekuwa wakitozwa ushuru usio halali mjini Singida, hutozwa fedha kwa ajili ya usafi wakati mji wa Singida ni mchafu. Hayo yote yanahitaji mtetezi.

Askofu anapoamua kumwonya mtetezi wa haki ili kutumikia mafisadi hawa, analenga nini? Anafaidika vipi na uongozi unaolalamikiwa na wananchi? Yeye kama askofu aliumia vipi na kwa nini aliumia na ushindi wa Lissu, hadi aone walioshindwa wanahuzunika?

Je, anakubalina na rushwa iliyotumika kuwanunulia wananchi vitenge, kanga, magodoro fulana na kofia alizokuwa anatoa yule aliyeshindwa? Anamhurumia aliyeshindwa kwa kuwa alitoa fedha nyingi kupita kiasi kuhonga wananchi? Anatufundisha nini sisi waumini wake kwa siku zijazo?

Je, kuwahurumia watoa rushwa walioshindwa huku akiwawaonya walioshinda kihalali waache kushangilia ushindi wao ni msimamo wa kanisa au wake binafsi?

Maaskofu wangapi walifanya kitu kama hicho kwenye majimbo yao? Askofu huyu atatumiwa na mkuu wa mkoa kwa mambo mangapi? Na atatumiwa vile kwa muda gani? Na alipotumwa hakugundua kuwa mkuu wa mkoa anao watu wengi wa kutuma kwa mambo mepesi kama hayo ili amshauri vinginevyo kuliko kujitolea kwenda?

Ziara yake kwenda kuonana na Lissu ililipiwa kiasi gani toka kwa mkuu wa mkoa? Kwa nini hakupewa gari na ofisi ya mkuu wa mkoa akaamua kutumia gari yake inayolipiwa na waamini wa kanisa hilo? Ni kitendo cha aibu, ambacho kama bado kipo kwenye akili za waumini, basi ni cha kuvumilia.

Lakini mkuu wa mkoa wa Singida na askofu huyu wamedhalilisha kanisa kwa kutumia gari ya askofu kufanyia siasa ambazo hazina lengo la kumkomboa maskini wa Kitanzania.

Si vema askofu kuwabeba viongozi wa aina hii, ni aibu katika jamii. Tunamwomba Mungu awajalie busara wasirudie mchezo mchafu kama huu. Na kwa aibu hii ingefaa askofu na mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya waombe radhi wakristo kwa Singida kwa kutumia gari la wakristo kwa shughuli zenye manufaa ya kifisadi, yasiyo na tija hata kidogo kwa maendeleo ya Kanisa.

Hofu ya viongozi wa serikali kwa ushindi wa Lissu imekuwa kubwa tangu wakati wa kampeni, ndio maana akiwa Singida, Jakaya Kikwete alinukuliwa akisema; "Heri Dk. Slaa awe rais, kuliko Tundu Lissu kuwa mbunge."

Pamoja na hayo yote tunawaomba viongozi wa serikali na viongozi wa dini msipingane na sauti za wananchi. Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu.

Chanzo: Mwanahalisi
Lissu alipokuwa Nje ya Nchi kimatibabu nchi ilikuwa imezubaa sana ilibaki kidogo nchi iwe Zezeta.. Ila tangu Lissu arudi taifa limechangamka. Mambo yanapaswa kuwa namna hii ni haramu akili ndogo kuitawala akili kubwa.
 
Back
Top Bottom