Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 23,877
- 31,632
Rais mstaafu wa awamu ya nne ndugu Jakaya Kikwete ndiye rais bora zaidi kwa hapa nchini kuliko marais wote waliopita na huyu aliyejipa urais kinguvu
Kipindi cha Kikwete maisha yalikuwa poa sana na wengi walitoboa kipindi chake.
Japo ufisadi ulikuwa mkubwa, watumishi hewa lakini pesa mtaani ilikuwepo na amani pia ilikuwepo.
Kikwete ndiye rais aliyezingatia zaidi haki za kibinadamu na demokrasia .
Kwa asilimia kubwa kama mtu alishindwa kutoboa kipindi kile cha kikwete itamchukua muda mrefu sana kutoboa .
Ila sasa mgema akisifiwa tembo hutilia maji.
Mzee amekuja kujiharibia dakika za jioniiiiii kabisa.
Siku hizi wakitajwa watu wasiopendwa na wanapewa kashfa za kila namna ni yeye , laiti kama angejikalia zake kimya na kutojihusisha na samia angejijengea heshima zaidi na angekuwa ni rais anayekumbukwa zaidi kuliko marais wote waliopita.
Nakumbuka kipindi cha Magufuli , kuna watu walikuwa wanatamani hata Kikwete arudi tena madarakani au kama inawezekana aende hata chama pinzani aje kumchallenge magufuli kwenye uchaguzi unaofuata wa nafasi ya urais.
Hii yote ilikuwa inaonesha ni namna gani alivyokuwa anapendwa.
Kwa sasa wengi hatumpendi maana ina sadikika yeye ndio yupo nyuma anaratibu kwa haya yote yanayoendelea nchini .
Nchi mpaka sasa haijapata utulivu tangu mwaka huu uanze mpaka unaelekea ukingoni na kuanzia mwezi wa 8 mpaka sasa matukio mengi ya kuogofya yanazidi kupamba moto.
Tulimpenda ila ameshindwa kulinda heshima yake.