Stabilaiza
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 1,843
- 1,143
Baba wa taifa Mwalimu JK Nyerere alituanchia nchi yenye amani na umoja isiyokuwa na mgawanyiko ya kibaguzi kama vile wa kidini na kikabila. Umoja huu na amani umeitofautisha nchi yetu na nchi nyingine kama vile Kenya, Rwanda na Somalia. Katika kuchukua uongozi wa nchi, JK na Pinda waliapa kulinda katiba ya nchi yetu ambayo inaikataza serikali kutangaza dini.
Lakini sasa JK na Pinda kwa makusudi wameamua kuivuruga nchi yetu kwa kuleta mgawanyiko wa kidini. Wanalazimisha kutunga sheria ya mahakama ya kadhi huku wakijua kuwa mahakama ya kadhi haijishughulishi na masuala ya kijamii bali ni ibada kwa sababu kadiri ya mafundisho na maelekezo yanayotolewa na mashehe, masuala ya kadhi yanaongozwa na kurani na mafundisho ya mtume.
Ndiyo maana wanaoitwa "makafri hawatakiwi kunusa pua kuamua mambo hayo ya ibada ya kiislamu" Wadau mbalimbali wamewakaza JK na Pinda kuacha kueneza dini ya kiislamu kwa sababu serikali haina dini bali watu ndiyo wenye dini. Wanananchi wamekataa nchi yetu kusilimishwa kwa lazima kupitia mahakama ya kadhi.
Masuala yote ya ibada na imani yanashughulikiwa na wenye dini husika siyo serikali. Kazi ya serikali inaishia pale inapotoa uhuru wa kuabudu bila kuwa na upendeleo kwa dini yoyote.
Kama kisingizio ni MOU kati ya serikali na taasisi za kidini zinazotoa huduma za matibabu ikiwemo hospitali ambazo zinahudumia wananchi wote, tena wa dini zote hata wapagani, ni bora serikali ifute kabisa MOU hiyo ili kuinusuru nchi yetu.
Ni bora wananchi tugeukie matibabu ya asili, kama serikali inashindwa kutoa huduma nzuri ya hospitali kuliko kuitumbukiza nchi hii kwenye machafuko ya kidini.
Hivi JK na Pinda watapata faida gani ikiwa wanatengeneza na kutuachia nchi kama Afrika ya kati ilivyo? Wananchi tuendelee kuungana na kuwa thabiti kukataa vurugu hizi zinazopaliliwa na kuchochewa na watawala kwa maslahi binafsi ya kusaka urais na kuficha udhaifu wao kwenye kichaka cha udini.