Apologise lady
JF-Expert Member
- Sep 16, 2013
- 5,980
- 3,115
Kiongozi asiyekuwa na maamuzi yake binafsi, kila jambo anataka hadi ashauriwe hafai kuwa kiongozi wa nchi.
Nashukuru mno kwa maelezo ya kina kuhusu msimamo wako.Kuhusu madhehebu mengine nao wafanye MOU na serikali inawezekana na hata Waislamu walishahimizwa kufanya hivyo. Lakini kumbuka kuwa kuna majengo ya serikali yaliyokabidhiwa kwa taasisi za kiislamu ili kuanzisha chuo kikuuu kwa ajili ya kuhudumia wananchi wote. Sijui ni kwa kiwango gani wananchi wasiowaislamu wanapata fursa ya kusoma kwenye chuo hicho cha waislamu au ni kwa kiwango gani wananchi wasiowaislamu wanapta ajira katika chuo hicho. Pamoja na mapungufu ambayo yanaweza kuwepo ya ugumu kwa wasiowaislamu kupata nafasi katika taasisis hiyo ya serikali waliyppewa waislamu, bado tatizo kiimani na haliwezi kufanana na tabia ya JK na Pinda kulazimisha wananchi wote wawe waislamu kupitia sheria ya mahakama ya kadhi. Hili la kusema limeona MOU kama tatizo, kimsingi sioni tatizo kubwa kama ambavyo sioni tatizo kubwa kwa chuo kukuu cha waislamu. Limependekeza MOU ifutwe kama ndiyo tatizo kwa sababu kuna hoja ambazo hazina mashika zinazofananisha MOU na mahakama ya kadhi.
Kwanza MOU siyo sheria, pili huduma za jamii kama hospitali zinazotolewa na makanisa au hata taasisi za kiislamu, hutolewa kwa wananchi wote bila kujali dini zao. Ni tofauti na mahakama ya kadhi ambayo inashughulika na mambo ya ibada ambayo asiyemuislamu hafaidiki wala kuhusika nayo. Shida ni kuwa sheria yoyote ya mahakama ya kadhi inaifanya serikali kufanya kazi ya kutangaza uislamu kwa vile mambo ya mahakama ya kadhi msingi wake ni kurani na mafunsisho ya mtume na ni ibada, ndiyo maana "kafiri" haruhusiwi kuyasimamia. Ingawa MOU na mahakama ya kadhi ni vitu viwili tofauti naona kwamba ni vema ifutwe kwa ajili ya kulinda umoja na amani ya nchi. Nadhani kwamba madai, kutumiwa kwa mahakama kadhi na watawala kwa masilahi yao binafsi ya kisiasa lakini kwa hasara ya kuvuruga nchi yetu yatakoma kabisa.
Kuhusu MOU kuendekeza serikali kutotimiza wajibu wake ndiyo kitu nilichosema. Bora tutafute miti shamba kwa kukosa huduma bora za hospital za serikali kuliko kuwa na MOU inayotumiwa kama chambo cha madai ya mahakama ya kadhi. Ninafahamu kuwa huduma katika hospitali za serikali zinaweza kuwa mbaya ulinganisha na za taasisi za dini. Lakini bora serikali ikose wadau wa taasisi za kidini katika kutoa huduma za hospitali kuliko JK na Pinda kupalilia udini utakaoleta machafuko nchini.
Mkuu taasisi zingine haziwezi kuomba MOU kwasababu hazina social service institutions. Hili la pili, Kilindi ikiwa ni mfano, huu ni udhaifu mkubwa sana. Na kama MoU iliridhia secondment ya wafanyakazi kwa malipo ya serikali hili ni bomu linalosubiri kulipuka.STABILAIZA naona ni respond kwa jambo moja tu na mengine tuwaachie wadau wengine.Hili la MOU kati ya serikali na kanisa.
Kwa mtizamo wa haraka ni kuwa kwani taasisi nyingine nazo zisiombe MOU na serikali ili zitoe huduma,hii inaweza kuwa na mashiko kama mtu hatangalia historia.
La pili kuwa hii MOU inatumika vibaya na serikali inaitumia kukwepa wajibu wake na nitakupa mfano.
Wilaya mpya ya Kilindi ilipoanzishwa palikuwa na kituo cha Afya lakini badala ya serikali kuwekeza katika kukipandisha hadhi au kujenga hospitali yake imeachia KKKT kujenga hospitali ya wilaya.Hospitali hizi zinaendeshwa kwa kutumia wafanyakazi amabo wamekuwa seconded na serikali lakini faida inakwenda kanisani,hili ni hatari na nashukuru umeliona.
Mkuu, kumbe una akili unajua kuwasilisha mada kwa usahihi, ungeandika hivi ningekupa LIKE tangu mwanzo. Jizoeze kuandika hoja namna hiyo, ukizunguka mbuyu hatuna muda wa kufuatilia akili yako ilikuwa inawaza nini hasa. kama unasink au unathink. Vizuri sana sasa.Hivi Nikuulize swali, wewe ni great thinker au great sinker? Haya ngoja nikutafunie. Kwa ufupi ni kwamna JK na Pinda wanapalilia udini kwa maslahi yao binafisi na kuficha udhaifu wao kwenye kichaka cha udini lakini kwa hasara ya kuvuruga umoja na amani ya nchi yetu. Wanaitengeneza nchi yetu ifanane na Afrika ya kati ambayo imevurugika kwa sababu ya watawala kutumia udini kama karata ya kisiasa na kuficha udhaifu wao kwenye kichaka cha udini. Mwisho nikasema wananchi tuendelee kuungana na kuwa thabiti kukataa vurugu hizi zinazopaliliwa na kuchochewa na watawala kwa maslahi binafsi ya kusaka urais na kuficha udhaifu wao kwenye kichaka cha udini. Umeelewa sasa?
Mkuu wameshakuwa sugu kwa maombi, hawasikii wala hawashituki.wanahitaji maombi yetu ili wafanye maamuzi sahihi
Kwa hiyo jibu ni nchi igawanywe waislamu nchi yao na wakristo nchi yso au sivyo?Kusema kuwa Kama taasisi nyingine zinataka kuingia Mou na Serikali ziingie Ni sawasawa na mtu anayeweza kusema kuwa kama wakiristo nao wanataka Mashauri ya kanisani yawe Rasmi nao Waombe tu serikali ipeleke Muswada bungeni kama ilivyotaka kufanya kwa mahakama ya kadhi.
Kimsingi Mou ya Kanisa na Serikali ni partnership ya Serikali kulisaidia Kanisa Kibiashara. Kwanza kwa nini hiyo Mou inaipa Taasisi Moja advantage ya Kibiashara kuliko nyingine zenye kutoa huduma sawa?
Na kwa nini miaka yote hii Serikali haitumii mabilioni inayolipa Kanisa kujenga Mahospitali yake yenyewe ya rufaa?
Hii ndiyo inaitwa Mfumo Kristo, The Christian Hegemony, ambapo Wakiristo wanasikilizwa, wanapewa Ruzuku kijanja kwa kisingizio cha huduma za kijamii Halafu Waislamu Mfumo wao wa maisha hauheshimiwi, wanapuuzwa katika nchi yao wenyewe. Kiufupi hii hali haijakaa sawa hata kidogo.
Nami nasema ikibidi walaaniwe, maana sauti za watu wakiwemo maaskofu ni sauti ya Muumba.Tuwaule kipi bora kura au amani? Nyerere aliliona hili lakini wao kwa uchu wa madaraka wakaahidi na kutumbukiza kwenye ilani ya CCM eti tutawaletea Mahakama ya Kadhi na ndiyo inayotutesa sasa. Walaaniwe wanaoleta chokochoko za kidini
Hana huruma huyu, urais umempofusha. Hawa ni wa kulazimishwa wawajibike kwa wananchi.Pinda pinda pinda tuhurumieeeeeeeee
Ujiulize pia kwa nini Pesa za EPA, Richmond, Escrow, n.k. hazikutumika kujenga mahospitali. Serikali ya CCM haina huruma kwa wananchi wake, ndiyo maana madhehebu ya dini yameziba ombwe la serikali kushindwa kutoa huduma za hospita. Lakini kikubwa ni kwamba kama tatizo ni MOU ni bora ifutwe kuliko kuislimisha nchi yote kwa lazima kupitia sheria ya mahakama ya kadhi.Kusema kuwa Kama taasisi nyingine zinataka kuingia Mou na Serikali ziingie Ni sawasawa na mtu anayeweza kusema kuwa kama wakiristo nao wanataka Mashauri ya kanisani yawe Rasmi nao Waombe tu serikali ipeleke Muswada bungeni kama ilivyotaka kufanya kwa mahakama ya kadhi.
Kimsingi Mou ya Kanisa na Serikali ni partnership ya Serikali kulisaidia Kanisa Kibiashara. Kwanza kwa nini hiyo Mou inaipa Taasisi Moja advantage ya Kibiashara kuliko nyingine zenye kutoa huduma sawa?
Na kwa nini miaka yote hii Serikali haitumii mabilioni inayolipa Kanisa kujenga Mahospitali yake yenyewe ya rufaa?
Hii ndiyo inaitwa Mfumo Kristo, The Christian Hegemony, ambapo Wakiristo wanasikilizwa, wanapewa Ruzuku kijanja kwa kisingizio cha huduma za kijamii Halafu Waislamu Mfumo wao wa maisha hauheshimiwi, wanapuuzwa katika nchi yao wenyewe. Kiufupi hii hali haijakaa sawa hata kidogo.
Mkuu ni ibada na kwamba siyo tu wanataka iwe kwenye katiba lakini JK na Pinda walikuja na version ya kuitungia sheria bungeni. Iwe kuwekwa kwenye katiba au kutungiwa sheria, mahakama ya kadhi inafanya mambo ya ibada ya kiislamu, na ni kuislimisha nchi kwa lazima wakati si kazi ya serikali kueneza dini na pia katiba inatoa uhuru wa kuabudu bila kulazimishwa kushiriki ibada usiyotaka.dah kwamba mahakama ya kadhi ni ibada! sasa inakuwaje suala la ibada liwekwe kwenye katiba ya nchi? siku nyingne mtadai na kwenda makka iwekwe kwenye katiba!