Jackbauer
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,038
- 2,199
Salam sana wana Jf,mimi naingia hapa JF kwa mara ya kwanza na kwa lengo moja tu,kumueleza Kikwete na timu yake feki waache kuwafanya watanzania wajinga.nasisitiza kuwa kikwete na timu yake kwani yawezekana hajui analosema au anafanya makusudi kupotosha.ni mengi ya uongo yanasemwa ila hili linalohusu afya ni kero kwangu na watz wote kwa ujumla kuendelea kulisikia.Eti Muhimbili wanafanya Open Heart surgery hivyo sasa hatuna haja ya kwenda India etc.ukweli ni kwamba Muhimbili bado wako katika mchakato wa kufikia mafanikio yanayosemwa na kikwete.eti anasema wataalamu karibu 47 hivi wamesomeshwa na wanafanya OHS(wanafungua vifua) bila wasiwasi.hii si kweli.ni kweli kuna madaktari walipelekwa Israel na kwengineko kujifunza baadhi ya mambo yanayohusiana na Vasicular surgery(upasuaji wa mishipa ya damu).ni kweli mchakato wa kuanzisha kitengo cha magonjwa ya moyo kitakachohusisha upasuaji wa moyo,ni kweli kwamba wataalamu wetu wanafanya baadhi ya procedure ndogondogo ili kuangalia ufanisi na changamoto za kuanzisha OHS(msinikoti vibaya sina maana ya majaribio kwenye miili ya watu).tatizo langu hapa ni kwamba mwanasiasa huyu uchwara anayependa sifa na kuona watanzania wote wapo UMASAINI au kule kIROMO na wasiojua au kuweza kufuatilia mambo,anajaribu kuingilia mipaka ya profession.namuomba kikwete ajikite kwenye siasa na asiingilie weledi tena eneo hili muhimu linalohusu afya ya mtu.ombi langu kwenu wanJf :nujua kuna medical personell ambao wantumia jukwaa hili kupata habari na kuelimisha.naomba msaada wenu katika kulielezea hili swala kwa mapana.LENGO LANGU SIO SIASA HAPA ILA SIASA IMEINGILIA MIPAKA YATAKA KUCHEZEA UHAI WANGU,NDUGU ZANGU NA WATZ WENZANGU.
UPDATES
Leo hii Mheshimiwa Rais mstaafu anaingia kwenye vitabi vya kumbukumb na historia katika afya hasa hasa afya ya moyo.
Kitengo cha upasuaji wa moyo Muhimbili kinafanya operesheni ya kwanza ya kwekeza kifaa cha kupanga mrindimo yaani pacemaker kwenye moyo wa mtanzania kwa mara ya kwanza.
Sifa zimrudie JK kwa kulisimamia hili baada ya criticism kutoka kwa wadau wa afya.o
UPDATES
Leo hii Mheshimiwa Rais mstaafu anaingia kwenye vitabi vya kumbukumb na historia katika afya hasa hasa afya ya moyo.
Kitengo cha upasuaji wa moyo Muhimbili kinafanya operesheni ya kwanza ya kwekeza kifaa cha kupanga mrindimo yaani pacemaker kwenye moyo wa mtanzania kwa mara ya kwanza.
Sifa zimrudie JK kwa kulisimamia hili baada ya criticism kutoka kwa wadau wa afya.o