Hospitali ya Muhimbili Mloganzila yaanzisha huduma ya plastic surgery ikiwa ni pamoja na kuongeza matiti, makalio, nk

TheCrocodile

JF-Expert Member
May 31, 2021
1,077
2,814
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tawi la Mloganzila wameanzisha huduma ya upasuaji ya kurekebisha baadhi ya sehemu mbalimbali za mwili (plastic surgery). Baadhi ya aina za upasuaji ambazo zitakua zikitokewa hospitalini hapo ni pamoja na kuongeza/kupunguza matiti, kuongeza hips, kuongeza makalio, kurekebisha sura (facelift), kutengeneza shingo, na kadhalika.

Gharama za upasuaji huo ni kati ya shilingi za Kitanzania Milioni 9 hadi Milioni 24 kutegemea na ukubwa na aina ya upasuaji. Jedwali hapa chini linaonyesha gharama hizo kwa aina mbalimbali za upasuaji huu.

Awali, wahitaji wa aina hizi za upasuaji walikua wanalazimika kwenda Uturuki, India na nchi zingine za Mashariki ya kati kwa ajili ya huduma hizi. Kutokana na ujio wa huduma hizi Mloganzila, kutakua hakuna tena haja ya kwenda Uturuki, kwani sasa huduma imesogezwa karibu.

Kwa sasa gharama hizi haziwi covered na bima ya NHIF.
Changamkieni fursa Watanzania.

IMG-20230419-WA0032(1).jpg
 
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tawi la Mloganzila wameanzisha huduma ya upasuaji ya kurekebisha baadhi ya sehemu mbalimbali za mwili (plastic surgery). Baadhi ya aina za upasuaji ambazo zitakua zikitokewa hospitalini hapo ni pamoja na kuongeza/kupunguza matiti, kuongeza hips, kuongeza makalio, kurekebisha sura (facelift), kutengeneza shingo, na kadhalika.

Gharama za upasuaji huo ni kati ya shilingi za Kitanzania Milioni 9 hadi Milioni 24 kutegemea na ukubwa na aina ya upasuaji. Jedwali hapa chini linaonyesha gharama hizo kwa aina mbalimbali za upasuaji huu.

Awali, wahitaji wa aina hizi za upasuaji walikua wanalazimika kwenda Uturuki, India na nchi zingine za Asia ya kati kwa ajili ya huduma hizi. Kutokana na ujio wa huduma hizi Mloganzila, kutakua hakuna tena haja ya kwenda Uturuki, kwani sasa huduma imesogezwa karibu.

Kwa sasa gharama hizi haziwi covered na bima ya NHIF.
Changamkieni fursa Watanzania.

View attachment 2593082
Safi sana hii imekaa vizuri kibiashara. Haya ndo maendeleo tunataka kuyaona kwenye sekta zote nchini wasiishie Mloganzila tu.
 
Back
Top Bottom