Kikwete na OPEN HEART SURGERY MUHIMBILI!!

Kwa hilinitampa Shikamoo!
by the way JK alidhaminiwa na marehemu babu yangu kuwa mbunge!

Mbongo utamjua wakati wa mavuno, lazima undugu utafutwe. Lakini wakati wa maandalizi ya kilimo anajiweka mbali- hana uhakika kama mvua itanyesha-hawezi kujiassociate.
 
Mbongo utamjua wakati wa mavuno, lazima undugu utafutwe. Lakini wakati wa maandalizi ta kilimo anajuweka mbali- hana uhakika kama mvua itanyesha-hawezi kujiassociate.
Kipindi kile nilikuwa naclarify reality kwa kile kilichosemwa.

Na sasa na-appreciate kilichotendeka!huu sio ubongo ni uzungu!

Napenda kuwa honest!!
 
Jackbauer ulitaka iwe mara ya ngapi ndipo uridhike? Kila siku huwa unaanza kutembea na mguu wa upande gani? Kila siku huwa unamara ya kwanza. Acha Tz ipige mbio ktk maendeleo.
 
Hongera sana mwenyekiti wangu, nakuamini kuliko chochote, kasoro Mungu tu. Wewe ni zaidi ya yeyote na kila ulichokipanga na kukianzisha kitadumu milele, watakuja wengi na kejeli za kila namna, lakini mwisho watashindwa tu. Niliwahi kusoma mahala zamani sana kuwa KATIKA VITA MUNGU HUWA UPANDE WA HAKI. Na atasimama kwa kila jambo lako la heri.
 
Unahitaji special diploma?
1. Upasuaji wa moyo, huo unaoitwa open heart surgery ni kati ya operesheni rahisi sana ambazo any surgeon can perform after a few months orientation in an appropriate centre. Zinahusu kuziba vitundu kwenye moyo (closure of septal defects) kwa nyuzi moja au mbili, kuweka valve bandia kwenye valve iliyochoka (valve replacement), kuzibua mishipa ya moyo iliyoziba (coronary arteries endoarectomy or by pass grafting) au kutumbukiza pacemaker bandia kwenye sinus node iliyochoka.

2. Kikwazo ni kuwa ili surgeon aweze kufanya hizo procedures, moyo na mapafu yanatakiwa kuwa yamesimamishwa kipindi chote ambacho surgeon anacheza na huo moyo wako. Hivyo huwa kuna mashine ya moyo na mapafu (heart lung machine) ambayo huwa connected na mfumo huo kabla ya kazi kuanza. Gharama ya mashine hii ni zaidi ya bei ya kununua ndege za aina ya airbuses mbili. Utalamu wa kuendesha mashine hizi anaethetists wetu wanao, huhitaji tu orientation of a few months in an appropriate centre.

3. Hiyo gharama ya equivalent to two air buses kwa kila mashine ndipo utashi au jukumu la siasa linapokuja. Awamu ya nne imewezesha upatikanaji wa mashine moja ya aina hiyo Muhimbilì na nyingine moja Bugando. Hivyo hospitali hizi zilishaanza hizo operesheni.

4. Tatizo sasa ni kupata hivyo vifaa tiba vingine (consumables) kama hizo artifcial valves, artificial pacemakers, stents na kadhalika ambavyo navyo bei yake si mchezo, ni zaidi ya bei ya madawati 100 kwa kila mgonjwa. Hili sasa ni jukumu la awamu ya tano ambayo muda mwafaķa wanaweza kulala nalo mbele. Tatizo ni uchumi wetu ndiyo maana awamu ya tano imeeanza kulala nalo mbele suala la kodi ili mambo haya mazuri yawezekane. Mkono mtupu haulambwi, acha kulalama tu hapa kama ma.......! Kila mmoja afanye kazi badala ya kucheza pool, hii ndicho kitawezesha mambo kama haya. Tuige kwa wenzetu wa China, wao kazi ni usiku na mchana.
 
Back
Top Bottom