Kikwete na Lowassa: Kazi imeanza rasmi!

Kikwete na Lowassa: Kazi imeanza rasmi!

Nadhani huo si mkakati mahsusi kwa muda huu.naamini kwa aina ya watanzania tluionao leo msisitizo ungewekwa katika kutekeleza ilani ya ccm ya kuwaletea wananchi maendeleo(kama ilani hiyo inatekelezeka).watashangaa mpango huo utakaposhindwa na kuanza kushikana uchawi.
 
Hii si habari ya kupuuzwa. Lakini kwa kuisambaratisha Chadema nadhani wamechelewa.

Jamani wana CDM wenzangu, mimi kila nikimfikiria kamanda Zitto uzingizi hauji kabisa! Mbona kabadirika ghafla? Msaada tafadhali.
 
Hata mgonjwa wa ukimwi huwa anajipa matumaini,na anakuwa na mipango miingi ambayo haitamfikisha popote.
 
Rais hatatoka kaskazini! na Bahati mbaya El ni kama kaniki hatakati hata umwoshe vipi
Mwambieni na hata kupendekezwa katika Wagombea Urais hatakuwemo kwenye list
mbona watu mnakurupuka na vihabari bila ya kuelewa wanaopiga kura ni akina nani na ni Kamati zipi?
yeye Kambi yake ilishameguka sasa watu wanamalizia michakato kwenye Kata,
El atumie mbinu ingine kwani anaelewa yote hayo na ni maji marefu kuingiza mguu Mkutano Mkuu
 
Noti Mpya Tz na Wana JF,
Tunakushukuru kwa taarifa,
kumbe ukiunganisha Dot. com unapata majibu, Ukifuatilia kauli zao utajua mengi, Membe amelalamika ana Maadaui 11, na waandishi wa Habari 2, ameenda mbali akisema kuwa inakuwaje kila Mwezi au baada ya miezi 2 anawekewa mitego na propaganda.
My Take: Kuna mambo mengi yanaendelea nyuma ya Pazia, sisi hatujui.
Nawakilisha




Membe kaundiwa kikundi anatembea nacho bila yeye kujua kama umesikia kauli ya Mgeja kuwa Membe hamwezi EL maana EL kawekeza sana katika mbio za urais. Kikundi kilichoundwa kina wakuu wa mikoa na waziri wa mambo ya ndani wametega vijana ambao wanamfuatilia membe kila kona.
 
Hivi vyote ni viashiria tu ila mkanda mkubwa uko nyuma unakuja hata ile issue ya Membe kuanza kulalama kuhusu maadui zake Membe anao mkanda mzima na jinsi mambo yanavyopelekwa hivi sasa, mwangalie Sitta na Mwakyembe ni kama wamenyoosha mikono juu na kujisalimisha na iangalie kauli ya Mgeja mwenyekiti wa ccm Shinyanga kujusu Membe na EL...

Lowasa ni heavy weight, wewe mchukue Sitta,Mwakyembe,Anne Kilango, Nape nk waweke upande mmoja upande mwengine akikaa Lowasa uzani unaelemea kwa Lowasa.
 
Hawa washabiki wa CDM sijui wanaamini chama chao kama kimeshuka toka mbinguni vile,yaani nikitakatifu kwa asilimia zote,kumbe historia inaonyesha viongozi wao wengi ni magamba yaliyotoka CCM,huyo Slaa hakuhamia CDM hivi hivi tu ni baada ya kushindwa kura za mchujo,kama angeshinda basi mpaka leo angekuwa gamba la maana kabisa,tena alivyo na uchu wa madaraka angekuwa pacha wa mwigulu nchemba

Sahihisho:
Dr Slaa alishinda kura za maoni ndani ya CCM mwaka 1995 huko Karatu (kwa maana ya kupata kura nyingi zaidi kuliko wagombea wengine wote), ila hakupitishwa. Akahama na kumbwaga mgombea aliyepitishwa na CCM kwenye uchaguzi wa ubunge. Toka wakati huo hii ni awamu ya nne jimbo lipo CDM.
Uongozi wa CCM wana mtindo huo wa kuengua chaguo la wanachama. Yalitokea pia mfano kwa Hussein Bashe na marehemu Phares Kabuye.
 
Kwa hili la mwarabu wa Iran kuonekana kwenye siasa za kenya nikiunganisha na hizi taarifa mpya hapa kama kuna kitu kinaendelea...
 
Kuna taarifa za chini ya kapeti toka makao makuu ya nchi kuwa bwana mkubwa baada ya kukutana na EL Ughaibuni wamekubaliana kuanzisha mikakati mizito ambayo itapelekea EL aingie madarakani kama rais mwaka 2015, mtoa taarifa wangu ambae ni mmoja wa wana kamati ya mambo ya nje ambae alikuwemo ktk msafara ulioenda Ulaya anapasha kuwa kuwa kati ya mikakati iyo ni pamoja na kutumia vyombo vya habari marafiki na ambavyo tayari EL amevianzisha huku vikisimamiwa na Balile na wahariri wengine na mpango mwingi ni kufanya Lobbying kwa mataifa jirani hasa kenya, Uganda na Congo ambapo mmoja wa watekelezaji wa mpango huo bwana Rostam Aziz tayari ameripotiwa kufanya safari nchini Kenya kwa ajili ya kuwashawishi viongozi wa huko hasa wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi nchini humo. Pia kuna mpango ambao umeanzishwa kwa spidi kubwa kuhakikisha chadema wanaparanganyika kwenye uchaguzi wao wa ndani na kumeguga, mpango huo umeshaanza na unatekelezwa na baadhi ya vyombo vya habari na viongozi wa ccm na watu wengine ambao wako ndani ya cdm wegine ni wabunge.
Kanieleza mambo mengi mengine nahitaji kuyafatilia kabla sijayaleta hapa maana yanahitaji ushahidi.

My take: Chadema inabidi wawe makini sana na nyendo zao na waangaliane vizuri ili kubaini nani anawatumikia hawa mabwana ndani ya chama.

Kwani hayo uliyoyaeleza una ushahidi nayo?! Uweke hapa tuuone vinginevyo acha fix kwamba una mengi!!
 
Hii si habari ya kupuuzwa. Lakini kwa kuisambaratisha Chadema nadhani wamechelewa.
Hizi mbinu chafu ikiwa pamoja na kupanga mauaji ya baadhi ya viongozi inaweza kuitikisa CDM na si kuisambaratisha. Chama sasa hivi kiko mioyoni mwa watanzania. CDM inaweza kusambaratishwa na makosa ya viongozi wake kama ilivyo kwa CCM na si kutokana na hujuma za nje.
 
Huyo mbunge aliekwambia kina lowasa na jk walimuita kwenye mazungumzo ya ya faragha ama waliita press conference?.
Story za kutunga utazijua tu
 
Kama kuna mtu anaweza akaisaliti CDM ni Zitto.Ana mtandao wa vijana fulani kanda ya ziwa akiwemo diwani wa Igoma na kajamaa fulani hivi kanadai kalikuwa ka katibu ka Chacha Wangwe,ndio wanaoneza kashfa za Dr. pamoja na Mbowe.Kuna siku moja walinikuta hotel fulani hata hawanijui,wakaeneza propaganda zao,sasa ilipofika kipindi cha maswali na majibu, nililiwapa ukweli baadae wakajifanya kuniomba namba ya simu,hawakunipigia na hicho kiwanja hawajakanyaga tena.
 
bila watanzania kutoana NGEU tutalalama hadi jua lishuke.
 
Back
Top Bottom