Mkodoleaji
JF-Expert Member
- Apr 27, 2008
- 458
- 138
hii statistic haijakaa kisomi zaidi ya udakuUtafiti wa kura za maoni uliotangazwa na REDET umeonyesha kwamba kama uchaguzi ungefanyika leo, CCM na Kikwete wangeshinda kwa zaidi ya asilimia 70.
Sources: Channel Ten, StarTV, TBC
Kweli REDET wamebobea kwa uongo, kwa akili ndogo tu hivi kweli Daily News linaongoza kwa kusomwa sana na watu,vijijini au mijini? hapa tu inadhihirisha kuwa utafiti umefanyika maofisini hasa ofisi za serikali na hii inanifanya nitilie mashaka utafiti wao kama ni wa kweli au wa kubuni na kufurahisha watu wao.Kwa vyombo vya habari na jinsi vinavyotoa elimu ya uraia, asilimia 42.7 ya wahojiwa waliridhika na utendaji wake ambapo redio ziliongoza kwa asilimia 73.7, televisheni asilimia 41.6 na magazeti asilimia 27.4 na upande wa magazeti gazeti la Daily News liliongoza kwa kusomwa sana kwa asilimia 25.6, Mwananchi asilimia 17.1 na Nipashe asilimia 12.4.
Kweli REDET wamebobea kwa uongo, kwa akili ndogo tu hivi kweli Daily News linaongoza kwa kusomwa sana na watu,vijijini au mijini? hapa tu inadhihirisha kuwa utafiti umefanyika maofisini hasa ofisi za serikali na hii inanifanya nitilie mashaka utafiti wao kama ni wa kweli au wa kubuni na kufurahisha watu wao.
Utafiti unatakiwa uendane na hali halisi iliyopo huwezi kusema utendaji wa serikali unaendelea vizuri wakati huohuo unasema 2/3 ya wabunge wao ambao ndio wanaunda serikali wameonekana hawatarudi maana yake hawafai, I believe in research but I dont trust every research.
Utafiti wa kura za maoni uliotangazwa na REDET umeonyesha kwamba kama uchaguzi ungefanyika leo, CCM na Kikwete wangeshinda kwa zaidi ya asilimia 70.
Sources: Channel Ten, StarTV, TBC
ndugu jamaa na marafiki tafiti hazipigwi na maneno. zinapigwa na tafiti . najua wengi hamkutaka kusikia majibu ya tafiti yakiwa hivyo bt too bad ndo utafiti huo.70% wengine wote watapata 30% as in CHADEMA , CUF, TLP ,UDP,DP na wengine wote..........
asilimia zaidi ya 70% ya wananchi hawaridhiswi una utendaji wa mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali ya JK
Hii ndio Tz, King makers wako kazini!!
Mkuu usiumize kichwa, hawa REDET wanaeleweka malengo yao ni nini
Sasa ebu tumbie wewe mwenzetu kwa huu utafiti uliofanywa na hao hao REDET miaka ya nyuma unauelewewaje
Hoja yangu hawa maafisa waandamizi waliteuliwa na JK au JK alikuwa ana uwezo wa kutengua uteuzi wao kama alifanya kwa liyumba.
Kwa hiyo ukitafakari na ukifaya detail anylysis kwenye research za REDET utagundua kuna ambiguity kama sio contradiction kwenye tafiti zao.
utata unakuja nakuja kama watu 70% wanampenda JK na watu zaidi ya 70% hawaridhishiwi na utendaji wa viongozi JK anaowateua .????? Tuelewe nini
Kwamba JK anapendwa sababu yuko presentable zaidi.?????
Na ingekuwa vizuri hizi tafiti zingeeleza hao waliohojiwa ni kwa nini wanampenda JK ni sababu z a sera za kiuchumi, kijamii, au sababu za kiamani na utulivu(CCM way)