Kikwete: Mtaumbuka baada ya 2015

Kikwete: Mtaumbuka baada ya 2015

Sishangai kusikia ahadi zikiongezwa, 2015 si mbali. Sijui mgombea Rais ajaye kutoka CCM ataahidi nini tena. Tuliahidiwa kuishi kama peponi Maisha Bora kwa kila Mtz. 2005 sukari ilikuwa kilo shs 400 leo 2500 nyama kilo 800 leo 6000. Kweli haya ni maisha bora. 2010 tukaambiwa tutatoka Dar mpaka Tabora masaa 2 mpaka 3 kwa treni ya reli ya kati. Leo tunakaa siku 3 njiani tena kwa mbinde watu wamejazana kama magunia ya makopa. Anaendelea kuahidi meli mbili ziwa Victoria, Mheshimiwa Rais wangu. Si ulete moja tu kwanza hiyo ya pili hata ikichelewa tuonyeshe huo mfano?
Mbona nakujua wewe ni mswahili safi tu. Kwenu huwa mnasemaga; "Ada ya mja, kunena tu, muungwana kutenda." Nakuomba tu mtukufu Rais, ngonjera punguza tu baba, tenda zaidi.
CCM tutaikumbuka sana baada ya 2015, kwa;
Kuwatetea mafisadi, Kutetea Wauza sembe ng'ambo baada ya soko la hapa kujaa
Kufukua madini yetu yoote kama kwamba yalikuwa yanalipuka huko ardhini mkaogopa yataua watu wetu.
Kuwaomba Makaburu warudi kwa kasi kuja kugandamiza mazawa yasiyo na uwezo, mpaka waziri anasema uwezo wa mzawa ni kukoroga juice tena inywewe na watu wa kijijini kwani juice zilisoko super markiti ni za South tu.
CCM tutaikumbuka, kwa kuuza nyumba zote za serikali na za viongozi kama kwamba hakuna tena kiongozi ajaye. Ni Ikulu tu imebaki na hata hiyo tuna wasiwasi kuwa huenda tukaambiwa ibaki kama makumbusho ya kitaifa kumbe ishauzwa.
Kweli CCM tutaikumbuka kwa mengi waliyo fanya. Hakuna ambaye hakuyaona.
KIDUMU CHAMA! Sema; KIDUMU. Kwa heri
 
Kinachoniachaga hoi ni kwamba Rais ambaye anatakiwa kutofungamana na upande wowote katika nchi yake kwa kuwa ndiye kiongozi wa Taifa naye anatoa mipasho. Kwa mantiki hii Rais anatofauti gani na Nape au Mwigulu? Busara ni jambo muhumu sana kwa kiongozi mkuu wa nchi.
 
Ni kweli tutamkumbuka kama tulivyo mkumbuka Mkapa! maana jinsi awamu zinavyosonga ndiyo tunazidi kujuta, hivyo cha maana ni kubadilisha mfumo na kuachana na chama cha kifisadi, alafu jambo la muhimu mafanikio haya tangazwi mtu anayaona, hakuna aliye fundisha pilipili ni kali na sukari ni tamu kila mtu alijua mwenyewe kwa kuonja, hicho kiduchu lichofanya JK si fadhira ni wajibu wake na still ameperform below...tanzania kazi bado tunayo miaka 50 ya nchi yetu lakini uatadhani nchi ina miaka kumi. tuamke tuache kubweteka na kujipa sifa za kipuuuzi!
 
Kama Mwenyekiti wa Chadema Mbowe,anakiri Jk ni rais wa maendeleo Bavicha hata wakipinga kazi bure.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Miundombinu Mhe John Pombe Magufuli Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe L:eonidas Gama na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe wakikata utepe mojawapo ya magreda katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na kupewa shukurani na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaidiwa kuzindua jiwe la msingi na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai

 
1235450_601345819917115_1397038609_n.jpg

Ajivunie na mafanikio ya kijana huyu....
 
JK amejitahidi sana kujenga miundombinu japo hela zenyewe za madeni na sijui atakuja kulipa nani.
barabara ya kutoka singida hadi arusha ni moja ya sehemu zilikuwa zinaniudhi sana!!
HONGERA JK JAPO CCM mwisho wao ni 2015

Wapinzani bwana, mazuri mnayaona lakini kukubali ukweli mpaka muweke manjonjo.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaidiwa na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasini kukunjua pazia kama ishara ya kufungua rasmi wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea leo Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasini kukunjua pazia kama ishara ya kufungua rasmi wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea leo Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne.
 
Lazima akumbukwe Jakaya ni Rais gani msikivu kama Jakaya tutampata sie Wanyonge wa Taifa hili? Watoto wa wanyonge waliopata shahada chini ya Mpendwa Jakaya ni wengi kuliko waliopata shahada kuanzia kuumbwa kwa dunia mpaka 2005 kabla hajaingia, Hata Slaa analijua hili, barabara, umeme,maji,demokrasia, uwazi yanazidi awamu zote hata kama utajumlisha. Kwa ufupi Jakaya Success > (Nyerere + Mkapa+Mwinyi) Success.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasin katika hafla ya ufunguzi rasmi wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea leo Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne.

:violin:​
 
ndio nitaumbuka sana kama ahadi ya reli ya kati itakuwa imetekelezeka hadi iyo 2015.
 
nita mkumbuka kama mzee mpiga picha hovyo hata na maboga anapga picha, mzee wa kucheka cheka hata kwenye misiba ana chekacheka, rais aliye wai kusafiri kuliko hata waziri wake wa mambo ya nnje, pia ni rais anae shikilia rekodi ya kusafiri mara nyingi kuliko wote dunia,
 
wewe kweli mama toto. sidhani kama uliwahi kutongozwa na mwanaume yeyote yule kwa hizi hulka zako mitandaoni. naam machinga complex ni utekeleza wa ilani ya uchaguzi ya ccm 2010 hadi 2015. lengo ni kupanua fursa ya ajira kwa vijana na kutengeneza mazingira mazuri ya kibiashara. hilo hujui? au kwa vile ilani yenu haizungumzi hilo
Nikweli kabisa sijawahi kutongozwa kwasababu wewe unanizibia kwavile unajirahisisha sana
 
JK ni kama maji. hakwepeki. usipomsikiliza, utamwangalia na usipomwangalia, utamsoma kama ulivyosoma uzi huu na kuuchangia
Mkuu hii kalo hebu irudie tena nahisi kuna mamburula humu hawajakuelewa.
 
Rais Kikwete, atakumbukwa kwa kusaidi watoto wa masikini kusoma elimu ya juu, kuanzia sekondari mpaka vyuo vikuu.
 
Ritz hiyo barabara ya kwasadala_masama mkandarasi alishakimbia na kazi haikwisha.usanii kibao
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom