Kikwete: Mtaumbuka baada ya 2015

Kikwete: Mtaumbuka baada ya 2015

Rais , Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amesema wale wote wanaombeza kuhusu utendaji kazi wake wataona aibu atakapomaliza muhula wake 2015.

Rais ameyasema hayo wakati akizindua mradi wa kusambaza umeme katika mikoa ya Mwanza na Geita unaofadhiliwa na mfuko wa Changamoto wa Milenia(MCC).

Rais amesema Serikali yake itavunja recodi ya kusambaza umeme katika vijiji vingi nchini.

Jk amesema Tanzania inaongoza kwa mtandao wa barabara ambao ni bora afrika mashariki huku akiwahakikishia wakazi wa Kagera kuwa meli mbili alizowaahidi wakati wa kampeni ziko njiani zinakuja.

Rais alikuwa akishangiliwa na wananchi wakati wote wa hotuba yake.

Alisema Tanzania ni nchi kubwa kuliko nchi nyinine za Afrika Mashariki ,lakini ina mtandao mkubwa wa barabara kuliko nchi kama Kenya , lakini akawalaumu watu wanaoisifia nchi hiyo jirani na kubeza mafanikio ya serikali yake.

Aidha, Rais Kikwete amewashangaa baadhi ya viongozi wa CCM pamoja na wananchama kushindwa kuzungumzia mafanikio yaliyofikiwa na serikali ya CCM na badala yake wamekuwa hodari wa kujadili wanapobezwa na wapinzani"

Source: Mwananchi
Huo ukubwa wa eneo letu ndio unaofanya ionekane tunamtandao mkubwa wa barabara, ukifanya proper scalling tunatoka hata nje ya normal distribution curve.
 
  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu - Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
  56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha

Jamaa amejitahidi sana! mnyonge mnyongeni haki yake mpeni jamani, sasa tusijadili kiushabiki sasa ndo ubaya wenu najua hapa Chadema watapinga sana na CCM watasifia ila mimi sina chama wakuu, kuweni tu na uvumilivu,
 
ndio nitaumbuka sana kama ahadi ya reli ya kati itakuwa imetekelezeka hadi iyo 2015.

Mkuu kama watanzania tungekuwa ni watu wenye kufatilia mambo tungejua ni kwanini angalau barabara zinajengwa? Hivi nchi masikini kama Tanzania inaweza kuiacha reli ife halafu ielekeze nguvu zake kwenye kujenga barabara kweli! Hakuna nchi yenye viongozi sahihi inaweza kununua huu ujinga ni Tanzania tu hili linaweza kutokea!
Hebu tujiulize kwanini barabara lakini siyo reli? Mwakyembe amepiga tambo weeee lakini mkulu hakuna hata siku moja ameonyesha kumuunga mkono! Kuna agenda gani kwanini reli haitakiwi kufufuka? Ni kweli barabara ni rahisi kusafirishia makontena toka dar mpka mwanza,kigari, burundi, kongo nk? Ni kweli tunahitaji barabara kwa ajili ya kuwafikia wakulima kwa urahisi lakini je tunaweza kujenga uchumi mkubwa kwa kusafirisha mizigo kwa barabara kweli?
Magufuli amekuwa akilialia kuhusu magari makubwa kuharibu barabara lakini hata siku moja hadhubutu kusema hilo mbele ya raisi ni kwanini? Anaogopa nini? Kuna masilahi gani kwenye barabara? Barabara zenyewe za mkopo na zimeishi sana ni miaka 2-3 baada ya hapo ni vumbi kama kawaida!
Kwa nini tusiwe na reli imara kwanza ambayo itahakikisha mizigo yote mizito haitatumia barabara na hivyo barabara zitakazojengwa zitadumu kuliko hivi sasa tunajenga barabara za mkopo halafu ndani ya miaka 2 zimechoka na mkopo bado haujalipwa! Nani atakuja kulipa haya madeni ambayo hata investiment zake hazitakuwepo wakati wa kudaiwa?

Kwa maoni yangu raisi anafanya tu ilimradi yeye anatimiza ahadi zake bila kujali hasara na mzigo atakaotuwachia! Kama anataka akumbukwe kweli basi ajenge kwanza reli ili barabara zitakazo jengwa zidumu na mikopo ile ijekulipika bila maswali maana investiment zake zitakuwa bado zinaonekana na kila mtu!
 
Kikwete amejitahidi wala sio unafiki ila ambacho mimi sikifurahii ni kutokudhiti mfumuko wa bei za vyakula maana wananchi wengi hasa wa vijijini wanaumia sana na bei za vitu kama mchele, sukari, maharage nk.

Mkapa aliweza kudhibiti mfumuko wa bei sana, ila wajipange tu vizuri.
 
Kikwete amejitahidi wala sio unafiki ila ambacho mimi sikifurahii ni kutokudhiti mfumuko wa bei za vyakula maana wananchi wengi hasa wa vijijini wanaumia sana na bei za vitu kama mchele, sukari, maharage nk.

Mkapa aliweza kudhibiti mfumuko wa bei sana, ila wajipange tu vizuri.

Ahadi ni nyingi kuliko uwezo kwani hata iweje hawezi kuzitimiza kwa muda uliobaki!
 
Chadema wanafanya siasa tu ila wanajua kuwa hakuna raisi bora katika historia ya nchi yetu ya tanzania km jk.

Kama JK ndy rais bora katika historia ya TZ mpaka sasa, basi hii nchi haijawahi kupata rais.
 
Lazima akumbukwe Jakaya ni Rais gani msikivu kama Jakaya tutampata sie Wanyonge wa Taifa hili? Watoto wa wanyonge waliopata shahada chini ya Mpendwa Jakaya ni wengi kuliko waliopata shahada kuanzia kuumbwa kwa dunia mpaka 2005 kabla hajaingia, Hata Slaa analijua hili, barabara, umeme,maji,demokrasia, uwazi yanazidi awamu zote hata kama utajumlisha. Kwa ufupi Jakaya Success > (Nyerere + Mkapa+Mwinyi) Success.

Mkuu umepitiliza nadhani hasa hapo mwisho.
Kama JK ndy rais bora katika historia ya TZ mpaka sasa, basi hii nchi haijawahi kupata rais.

Ona mwenzako mpaka kapitiliza hapo juu sasa.
 
siku CCM itaacha kuwatetea mafisadi ndio siku hiyo hata mafanikio yake yataonekana ambapo siku hiyo haitafika!
jk amefanya mengi ya maana ila yanachafuliwa na sifa mbaya ya chama chake

Hachafuliwi anajichafua kupitia his son kukwapua mali za inji hii
 
Rais Kikwete, atakumbukwa kwa kusaidi watoto wa masikini kusoma elimu ya juu, kuanzia sekondari mpaka vyuo vikuu.

Lol mkuu kuna msemo wanasemaga wahenga eti 'mtoto hajui umuhimu wa mzazi mpaka akishaaga dunia' nadhani ndicho kitachowapata watanzania wengi.
 
Aliyekwambia Rais Kikwete ni Dr. nani?

hebu waulize TCU wakwambie nani anastahili kuitwa Dr.
 
Ngoja siku tupate Dikteta mmoja,ndio tutakumbuka vizuri.
 
Back
Top Bottom