Kikwete: Mtaumbuka baada ya 2015

Kikwete: Mtaumbuka baada ya 2015

Kama JK ndy rais bora katika historia ya TZ mpaka sasa, basi hii nchi haijawahi kupata rais.

Katika historia ya kusafiri nje ya nchi na kuweka ahadi nyingi zisizotekeleka pamoja na kuteua mawaziri wa ajabu sana kuongoza wizara ya elimu na hasa kwa awamu hii.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Ndo maana hamuelewi kila siku;
Sijui hata kama unachangia hata shilingi kwenye
kodi; nyie ndo wakwepaji kodi na majungu kibao;

Napenda Tanzania napenda CCM.


Kwa hiyo mishahara inatoka kwenye hela ya sembe na tembo sio.
No wonder mnawaabudu sana mafisadi na kushabikia safari za jk kutembeza bakuli dunia nzima.
 
JK amejitahidi sana kujenga miundombinu japo hela zenyewe za madeni na sijui atakuja kulipa nani.
barabara ya kutoka singida hadi arusha ni moja ya sehemu zilikuwa zinaniudhi sana!!
HONGERA JK JAPO CCM mwisho wao ni 2015

Baadhi yetu tulikuwa tunasafiri kutoka Bukoba kwenda Arusha na Moshi kwa kupita Dar es salaam. Ilikuwa safari ndefu sana lakini angalau ilikuwa ni ya uhakika, haraka na salama kuliko ya kukatiza Singida na Babati.Baadae nakumbuka safari za kutoka Bukoba kuja DSM kwa kupitia Mutukula-Masaka-Kampala-Jinja-Busia-Eldoreti-Nairobi-Namanga-Arusha-Moshi-Chalinze.Nayo ilikuwa ndefu lakini ya uhakika zaidi. Hayo yote imekuwa ni historia sasa.
 
Tunasubiri meli ya ziwa nyasa, TAnganyika na reli ya umeme kutoka dar hadi kigoma. maji kutoka ziwa victoria hadi tabora usijidai umesahau mkuu wa nchi

Yapo Shinyanga yanaelekea Nzega, Nzega ni wilaya ya mkoa gani?
 
ukishikiwa kiboko na Obama na huku unakandarasi na wachina wenye mabillioni, na pia unakabiliwa na threat ya kenya na uganda na rwanda na huko kusini kuna msumbiji naye anafanya mambo yake bila kelele, utaacha kutembea au kukimbilia hayo maendeleo bila kupenda?
 
Mkuu kama watanzania tungekuwa ni watu wenye kufatilia mambo tungejua ni kwanini angalau barabara zinajengwa? Hivi nchi masikini kama Tanzania inaweza kuiacha reli ife halafu ielekeze nguvu zake kwenye kujenga barabara kweli! Hakuna nchi yenye viongozi sahihi inaweza kununua huu ujinga ni Tanzania tu hili linaweza kutokea!
Hebu tujiulize kwanini barabara lakini siyo reli? Mwakyembe amepiga tambo weeee lakini mkulu hakuna hata siku moja ameonyesha kumuunga mkono! Kuna agenda gani kwanini reli haitakiwi kufufuka? Ni kweli barabara ni rahisi kusafirishia makontena toka dar mpka mwanza,kigari, burundi, kongo nk? Ni kweli tunahitaji barabara kwa ajili ya kuwafikia wakulima kwa urahisi lakini je tunaweza kujenga uchumi mkubwa kwa kusafirisha mizigo kwa barabara kweli?
Magufuli amekuwa akilialia kuhusu magari makubwa kuharibu barabara lakini hata siku moja hadhubutu kusema hilo mbele ya raisi ni kwanini? Anaogopa nini? Kuna masilahi gani kwenye barabara? Barabara zenyewe za mkopo na zimeishi sana ni miaka 2-3 baada ya hapo ni vumbi kama kawaida!
Kwa nini tusiwe na reli imara kwanza ambayo itahakikisha mizigo yote mizito haitatumia barabara na hivyo barabara zitakazojengwa zitadumu kuliko hivi sasa tunajenga barabara za mkopo halafu ndani ya miaka 2 zimechoka na mkopo bado haujalipwa! Nani atakuja kulipa haya madeni ambayo hata investiment zake hazitakuwepo wakati wa kudaiwa?

Kwa maoni yangu raisi anafanya tu ilimradi yeye anatimiza ahadi zake bila kujali hasara na mzigo atakaotuwachia! Kama anataka akumbukwe kweli basi ajenge kwanza reli ili barabara zitakazo jengwa zidumu na mikopo ile ijekulipika bila maswali maana investiment zake zitakuwa bado zinaonekana na kila mtu!

vyakula bei juu kwasbabu mkulima anapata hasara kusafirisha mazao kwa magari.
Wamiliki wa magari ya mizigo tunawajua na anayewalinda anajulikana na uchumi unaanza kuyumba kuanzia kwenye usafirishaji hadi kwenye hii mikopo tunayokopa.
kikwete ametuingiza mjini.
 
Tunasubiri miaka 2 Kigoma iwe kama Dubai

mungu ashushe rehema zake juu ya mkoa wetu huo. maji,umeme,miundombinu, mbona majangaaaaaaaaaa, airport majangaaaaaaaaaaaa,soko mazao ya wakulima majangaaaaaaaaaaa labda bukoba akiwaletea meli may be nasisi tutafaidika.meli zipo njiani wana wa bukoba
 
Yapo Shinyanga yanaelekea Nzega, Nzega ni wilaya ya mkoa gani?

hayo maji yenyewe apo shinyanga changa la macho tu,yamepita tu kwenye pipes kuelekea kahama-buzwagi kwa wakubwa. nuksi tupu,shinyanga wanalia hawana maji hata kidogo
 
"Wapo wanaodai" "PESA NDIO KILA KI2"SI KWELI!,"PESA SIO KILA KI2".Sababu "Pesa yaweza kununua KITANDA lakini sio"USINGIZ",
Pesa yaweza kununua SAA lakini sio"WAKAT",Pesa yaweza knunua "CHEO"lakin sio"HESHIMA"
Pesa yaweza kununua"DAWA"lakin sio"AFYA"
Pesa yaweza kununua"DAMU" lakin sio"UHAI"
Pesa yaweza kununua"ANASA" lakin sio "UPENDO"...Hivyo mtegemee Mungu ndo kila kitu.
 
Kwa ufupi ametoa ujumbe kuwa ndani ya ccm hauna anayefaa kuiongoza nchi.
 
wa kwanza kukumbuka ni dr slaa na freeman mbowe. hawa watu kila kukicha wanamtukana lakini kimoyomoyo wanampongeza. nakumbuka siku ile wakati JK alipofanya ziara yake jimboni kwa mbowe aliposhindwa kuzuia hisia zake na kutamka maneno yafuatayo: mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Jk kajenga marabara nzuri jimboni kwangu kuliko marais waliomtangulia. mwisho wa kunukuu

buku 7 izo. hata wewe utakuwa fisadi.vipi kuhusu mikoa mingine kama vile kigoma?????? izo pumba unaongea
 
Deni aliloacha mkapa lilikuwa trillion 6...kilaza kikwete kaongeza deni mpaka sasa trillion 25...then anajigamba eti kaleta maendeleo...pesa za mikopo zinatumika kwenye campaign za ccm, plus uchakachuaji then anadanganya wananchi kwa hizo barabara zinazojengwa kwa kiwango duni cha chini kabisa sijapata ona popote pale duniani.kweli kikwete ni janga kubwa la taifa. Mpaka amalize muhula wake deni litakuwa trillion 30 na hazitajulikana ziliko...kikwete ni mtu mbaya sanaaa hafai hata kidogo.
 
Huwezi kujisifu kabla kusifiwa, Nani ataenda kukata kipande cha barabara aweke kwenye sufuria apike ale na watoto? ajira zipo wapi? maji safi yapo wapi? mbona bei za chakula zimepanda mara dufu Tz? watu wanakufa kiholela kwa huduma mbovu kukosa matibabu hospitalini? Rushwa, mishahara mibovu., wananchi wanajituma jasho lao ndilo unapata kuweka vitega uchumi nje ya nchi ukimaliza muda wa urais uzidi kustarehe na famili yako? umeme upo wapi nk.

Nani mwenye akili zake timamu aumbuke kwa kuondoka Kikwete madarakani 2015? New broom always sweeps clean, tunataka mabadiliko hali ni mbaya sana sana.,
 
Nampenda sana raisi wangu JK kwani wakati mwingine huwa anasemaga kaukweli.Yeye anajua kabisa alitudanganya wadanganyika tukampa kura.Sasa anajua fika kuwa hataweza kutimiza alotudanganya na hitimisho la uwongo wake ni 2015 ambapo ndo wadanganyika watakapoumbuka!Simpo sana hiyo.
 
Deni aliloacha mkapa lilikuwa trillion 6...kilaza kikwete kaongeza deni mpaka sasa trillion 25...then anajigamba eti kaleta maendeleo...pesa za mikopo zinatumika kwenye campaign za ccm, plus uchakachuaji then anadanganya wananchi kwa hizo barabara zinazojengwa kwa kiwango duni cha chini kabisa sijapata ona popote pale duniani.kweli kikwete ni janga kubwa la taifa. Mpaka amalize muhula wake deni litakuwa trillion 30 na hazitajulikana ziliko...kikwete ni mtu mbaya sanaaa hafai hata kidogo.

Kukopeshwa maana yake wanaimani na unakopesheka,ni Nchi ngapi hawakubaliwi,Daraja la Maragalasi limejengwa kwa mkopo wa miaka 40 bila riba na Wachina,tuogope kukopa kwasababu ya deni la Taifa kuongezeka??USA wanamadeni makubwa sana CHINA na yanaongezeka na hawaogopi kukopa,acha matusi tunawajua kwakawaida hamna adabu,mfano mmoja,Urefu wa barabara uliojengwa na JK kwa miaka 8 sasa,haujafikiwa na maraisi wote walio mtangulia hata ukizichanganya urefu wa barabara za JK ni refu zaidi.Akili mali!!!
 
Back
Top Bottom