DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, leo amemnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Welezo, Zanzibar, Bi. Asma Mwinyi, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Hawaii, Jimbo la Welezo, Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Dkt. Kikwete, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kuwa chama bora ambacho hutekeleza ilani yake kwa vitendo. Amefafanua mafanikio mbalimbali yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kuwa ni ushahidi wa utekelezaji mzuri wa sera za chama hicho.
Aidha, amewataka wananchi waliohudhuria kampeni hiyo kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba mwaka huu kwenda kupiga kura na kuwachagua viongozi wa CCM.
Kwa upande wake, mgombea ubunge Bi. Asma Mwinyi amesema atahakikisha anashirikiana na wananchi katika masuala mbalimbali ya kijamii, kama alivyokuwa akifanya awali. Ameahidi kuendeleza miradi aliyokuwa akiisimamia, pamoja na kugharamia huduma za mazishi katika Jimbo hilo.