Kikwete mrudishe ROM asaidie kuokoa jahazi Zanzibar

MM huyu bwana sioni kama ana charisma ya kuokoa Zanzibar, katika watu ambao mpaka leo huwa nawaona kama wasio kuwa na ushawishi wa kisiasa upande wa Zanzibar ni huyu Mapuri pamoja na Ali Ameir, Kama watu wana kumbukumbu nzuri kilichomtoa Mapuri wizara ya mambo ya ndani na ukatibu mwenezi wa CCM ni kauli ya kutetea Askari magereza waliojichukulia sheria mkononi kuwapiga waandishi wa habari na kuwajeruhi vibaya. Utetezi ule ulifanya waandishi wasusie kuandika habari zake zote.

Kwa kweli sioni kama jamaa ana charisma ya kutuliza watu, ila kitu pekee ambacho tunaweza kuwaambia wazanzibar ni kuwa Jamaa alipelekwa kuwa barozi China (sina uhakika kama hajabadilishwa), na haya ni matunda ya muungano. Mtu pekee wa kusikilizwa kama angekuwa hai ni Marhum Ahmed Hassan Diria, jamaa alikuwa mwanadiplomasia mzuri.
 
Namzungumzia Ramadhani Omar Mapuri...do u guys still remember him!?
Yule jamaa ni jeuri sana, badala ya kuokoa jahazi ataliongezea uzito maradufu na kuharakisha kuzama kwake. MM CCM inakufa hakuna wa kuiokoa. cha muhimu ni abiria waliomo kenye jahazi hili(CCM) kujitosa na kupiga mbizi wajiokoe wenyewe, vinginevyo wanazama nalo. Sink...Sink...CCM..Sink
 
Hii ni sawa na kusema Nyerere angekuwepo! lini tutasimama wenyewe wadanganyika?

Another Silly Season........................................................
 
MM huyu bwana sioni kama ana charisma ya kuokoa Zanzibar, katika watu ambao mpaka leo huwa nawaona kama wasio kuwa na ushawishi wa kisiasa upande wa Zanzibar ni huyu Mapuri pamoja na Ali Ameir, Kama watu wana kumbukumbu nzuri kilichomtoa Mapuri wizara ya mambo ya ndani na ukatibu mwenezi wa CCM ni kauli ya kutetea Askari magereza waliojichukulia sheria mkononi kuwapiga waandishi wa habari na kuwajeruhi vibaya. Utetezi ule ulifanya waandishi wasusie kuandika habari zake zote.

Kwa kweli sioni kama jamaa ana charisma ya kutuliza watu, ila kitu pekee ambacho tunaweza kuwaambia wazanzibar ni kuwa Jamaa alipelekwa kuwa barozi China (sina uhakika kama hajabadilishwa), na haya ni matunda ya muungano. Mtu pekee wa kusikilizwa kama angekuwa hai ni Marhum Ahmed Hassan Diria, jamaa alikuwa mwanadiplomasia mzuri.
Zanzibar kama inavyojiita kuwa ni nchi ni aibu kuendeshwa kwa kutegemea ufanisi wa mtu mmoja. Kumbuka viongozi wa dini ndo wenye sauti kuliko wa serikali kule Zanzibar na mapuri si kiongozi wa dini. Naamini leo hii kama asingekuwepo Seif Sharif Hamad,ungeomba arudi kuokoa jahazi kama suala ni ushawishi. Tatizo Zanzibar kama nilivyokwambia wenye ushawishi ni viongozi wa dini ambao wengi wao nikiwaangalia sisiti kuhoji uzalendo wao na kama kweli wana nia njema na Zanzibar. Lakini pia elimu yao inanipa mashaka,maana mtu hupata elimu imsaidie kutatua matatizo na sio kuyaongeza.
 
Hatuwezi kuwaacha wazanzibar waende zao bure,kamwe haliwezekani hili
kama kuna mambo ya kutisha na ya hatari kutokea hapa Jamhuri ya muungano
wa Tanzania ,TANGANYIKA NA ZANZIBAR(UNGUJA NA PEMBA) basi ni hili la kuwaacha
wazanzibar waende zao.
Sintakubali hata kwa neno moja kukubali kutengana na zanzibar.Ni dhambi kubwa sana.tunaongea kwa
kwa maneno rahisi sana lakini hatujui implications zake,hatujui effects zake,hatujui nini kitatokea baada ya
mfarakano huu.Hakuna anayejua nini kitatokea,

Wa-Tanzania tuungane kwa nguvu zote kuhakikisha MUUNGANO unadumu milele daima na kizazi chetu kinaukuta.
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Africa
Mungu Bariki Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
 
Wengine tunaofikiria mbali zaidi ya hapa tulipo tunaona hilo ni jambo jema. Ingekuwa vema kama tungeamua kutatua matatizo yaliyopo ili muungano uweze kuwa imara. Sasa Zenj hawataki na wamekuwa kero kubwa itakuwaje? Let them go....
 
Binafsi naona Muungano wa kinafiki,au ambao upande mmoja una sintofahamu nyingi hauna maana,kama zanzibar wanaamua kusepa wasepe tu! Ila kifo cha muungano kiende sambamba na kifo cha CCM
 
Hana Jipya. kumbukumbu zangu ni kwamba, Huyu ROM alishindwa kazi wakati akiwa mmoja wa vigogo wa serikali ya CCM, nafuu yake kama ilivyo kwa akina Dr. B .Buriani & co vigogo wenzake wa serikali ya CCM walikwenda kumficha China kama balozi.
 
Back
Top Bottom