Tume ya Katiba
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,896
- 1,862
Hivi huu muungano ni kwa faida ya nani?
Mwenye heri
Hivi huu muungano ni kwa faida ya nani?
Mwenye heri
Ukipukutika huu na utakatifu ndio kimbembe, si ndio maana yake?
China si yupo Marmo?
Jambo la msingi ni kutatua kasoro zilizopo
ndani ya muungano,ili kuliweka katika msingi
bora wa sheria na uhalali wake.
Kero hizi zilikuwepo tangu uanzishwaji wake na
watu wengi wa zanzibar wamechukua kama ajenda
ya kuthubutu kuuvunja muungano.Nawahakikishia m
wazanzibari wote pamoja na UAMSHO kuwa MUUNGANO
Utadumu milele na wao wataondoka zao waende wanakotaka
kwenye kuishi,kama hawaamini basi wasubiri tume ya katiba imalize kazi yake.
PERIOD.
Namzungumzia Ramadhani Omar Mapuri...do u guys still remember him!?
Hivi huu muungano ni kwa faida ya nani?
Namzungumzia Ramadhani Omar Mapuri...do u guys still remember him!?
Bila shaka namkumbuka ROM. Mara ya mwisho kabla hajaondoka nchini alikuwa ni waziri wa mambo ya ndani na kama sijakosea alikuwa pia ni katibu mwenezi wa CCM yaani NAPE wa wakati huo. Alikorofishana na waandishi baada ya kushabikia kipigo cha waandishi wa habari waliopigwa na askari magereza. Baada ya maneno yake ya kashfa kwa waandishi alitakiwa aombe radhi lakini aligoma. Matokeo yake vyombo vyote vya habari viliamua kumsusia habari zake zote na huo ukawa mwishi wa ukatibu mwenezi wa CCM ana hatimaye uwaziri.
naunga mkono hojaHatuwezi kuwaacha wazanzibar waende zao bure,kamwe haliwezekani hili
kama kuna mambo ya kutisha na ya hatari kutokea hapa Jamhuri ya muungano
wa Tanzania ,TANGANYIKA NA ZANZIBAR(UNGUJA NA PEMBA) basi ni hili la kuwaacha
wazanzibar waende zao.
Sintakubali hata kwa neno moja kukubali kutengana na zanzibar.Ni dhambi kubwa sana.tunaongea kwa
kwa maneno rahisi sana lakini hatujui implications zake,hatujui effects zake,hatujui nini kitatokea baada ya
mfarakano huu.Hakuna anayejua nini kitatokea,
Wa-Tanzania tuungane kwa nguvu zote kuhakikisha MUUNGANO unadumu milele daima na kizazi chetu kinaukuta.
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Africa
Mungu Bariki Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Wewe Mzee una siasa kali za kihafidhina siku zote japo huwa unajipambana unapenda mageuzi lakini sio kweli.naunga mkono hoja
P
Zanzibar ndani ya muungano wetu huu adhimu ni the minority, kwenye muungano yote the minority ndio huwa wanasumbua kama ilivyo kwenye ndoa za mitala, mke mdogo ndio mwanzo WA chokochoko. Hivyo being a very sensitive to handle, isipokuwa mhafidhina mke mdogo atakupeleka puta!.Wewe Mzee una siasa kali za kihafidhina siku zote japo huwa unajipambana unapenda mageuzi lakini sio kweli.
Paskali bwana. Watu watafoka hii analysis yako kama vichaaZanzibar ndani ya muungano wetu huu adhimu ni the minority, kwenye muungano yote the minority ndio huwa wanasumbua kama ilivyo kwenye ndoa za mitala, mke mdogo ndio mwanzo WA chokochoko. Hivyo being a very sensitive to handle, isipokuwa mhafidhina mke mdogo atakupeleka puta!.
Tulipoungana , tulikubaliana tunaunda nchi moja ya JMT, na Zanzibar kuwa na mamlaka yake ya ndani kwa mambo ambayo siyo ya muungano. Zanzibar ilikuwa inachangia gharama za uendeshaji wa muungano, wimbo wa taifa na bendera moja.
Mara ghafla akagoma, mara naomba wimbo, bendera, katiba, sasa anajiita nchi. Kwa vile mtu kapenda kwa dhati, kila atakacho bi mdogo atapewa, na hata afanye vitimbi vipi, talaka hapewi!.
P
MhhhOmari Ramadhani Mapuri ni miongoni mwa wahafidhina huko Zenji ambao walijengwa na Komandoo. Mwingine ni yule aliyekuwa Naibu Waziri Kiongozi wa awamu iliyopita Bw. Shamuhuna. Hakika hawa wamepitwa na wakati na siasa za Zanzibar. Hawa walikuwa miongoni mwa watu wsioamini na wasiotaka mtu toka kisiwa cha Pembe aitawale Zanzibar; sasa imekuwa na siasa za uhasama Zanzibar zimepungua kwa kiasi kikubwa wakipewa hatamu hawa waungwana tutarudi tulikokuwa ambapo watu walikuwa hawashirikiani hata misibani.