Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,710
- 40,777
nipo nashangaa tu kama Rais Kikwete ana mpango wa kwenda Tehrani hivi karibuni au hadi mwakani?
nipo nashangaa tu kama Rais Kikwete ana mpango wa kwenda Tehrani hivi karibuni au hadi mwakani?
Naona hii thread imeshaanza kunukia udini....mie simo
ninachotaka kuchokonoa ni suala la Irani na Tanzania.. Mwanzoni tulipokuwa na Urais wa Baraza la Usalama nilidhani ilikuwa ni mkakati tu wa Jamhuri ya Iran kupata kura in case wakubwa wataamua kuingilia kati.... Kuna mada nilianzisha miezi kadhaa iliyopita inayoitwa "The Iranian Connection".. Rais anaweza kwenda kokote kule, kinachonishtua ni jinsi gani kati ya marafiki zote wa mataifa ya Kiislamu duniani tunavutwa sana na wa Irani, kwanini isiwe Libya, Jordani, Morocco au Saudi Arabia au UAE?
FNN, wrong.. hili halina Udini naangalia hasa kutokana na mwelekeo wa siasa za dunia sasa hivi. Hayo ya Udini wanayo wengine kwa sababu nina uhakika uhusiano wetu na Irani hautokani na msingi wa Udini kwa sababu tayari tuna nchi nyingi rafiki za Kiislamu na sikuulizia hilo... Wenye udini ni rahisi kuuona udini..
Kwa nini unashangaa...mbona Vatizan kaenda?
hivi mtu unafikiri mara ngapi mpaka kuanzisha thread kama hii ambayo unajua itaamsha hisia tafauti baina ya watu? tena kwa kuandika kwamba unashangaa.fikiri kabla kuanzisha mathread yako yanayofitinisha, mjomba.
sorry boss, basi endelea, kidogo hisia zangu ziliamka.ila kwa sasa ziko under control.endeleaFNN na Under age hebu acheni majibishao yasiyo kuwa na maana. kama hamna ishu za kujadili Hebu tulieni kwanza watu tukate ishu!
Ni matumaini yangu kwamba safari hii ya Muungwana itakuwa na mafanikio. Iran si tu kwamba ni Taifa ambalo sisi watanzania tunaweza kujifunza mambo mengi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kujitegemea kwa rasilimali tulizokuwa nazo lakini ni Taifa lenye kutetea Usawa na heshima kwa watu wote(mfano mzuri ni ishu ya wapalestina).
Irani ni Taifa lenye kuzalisha mafuta kwa wingi na kutokana na kuendelea kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia ni matumaini yangu kwamba raisi kikwete ataweza kufanya mazungumzo yatakayoinufaisha tanzania katika suala zima la mafuta.
na kwa hivi sasa irani inafanya maendeleo makubwa katika Sayansi kwa kutumia wataalam wake yenyewe na pia katika utafiti wa nishati Ya Kinyuklia kwa matumizi ya Amani inapiga hatua . na ukizingatia Raisi wa Iran Mahmoud Ahmednejad aliahidi alipokuwa anahutubia Umoja wa Mataifa kwamba Irani ipo tayari kusaidia nchi nyingine katika Tecnolojia hii ya umeme wa nishati ya Nyuklia ni matumaini yangu kwamba Raisi Kikwete ataitumia Fursa hii kuchangamkia Ofa hii. hasa ukizingatia matatizo ya umeme tuliyokuwa nayo, basi tunaiihitaji sana hii technolojia,
Pia Wairani wapo katika kundi la Kupinga ubeberu na Dhulma inayofanywa na baadhi ya mataifa yaliyoendelea. ni matumaini yangu kwamba Raisi Kikwete ataitumia Fursa hii kudumisha na kusisitiza msimamo wa Tanzania juu ya Haki Kwa Watu wote Pasi na kujali Mataifa yao.
Pia ningefurahi kama mheshimiwa Raisi Kikwete atazungumzia uwezekano wa kuwepo kwa scholarship kwa Wanafunzi wa kitanzania nchini irani. au uwezekano wa kuwepo exchange students kati ya hizi nchi mbili. tuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwao na wao pia kutoka kwetu kwani ni miongoni mwa jamii zenye ustaarabu wa zamani sana kabla hata ya Ulaya hii iliyo Maarufu.
Neno "nashangaa" mara nyingi lina connotations mbaya...na ktk ishu zinazohusu Iran kama Mwanakijiji alivyoandika linaweza kabisa likaleta mlipuko wa hisia kali na watu kuishia kutukanana...
nadhani kafungwa macho na siasa , imekuwa siasa mbele ,hisia baadae.pia bado anatawaliwa kifikira na super power nations kama usa na uingereza. hivyo adui wa marekani ndio aonekane adui ulimwengu mzima. tunaishi kwenye dunia ya reality, usifate mshengesha wa marekani kasema, fuata reality na reality tayari gamba la nyoka kaitoa .tutasoma mengi tukifungamana na iran kuliko tukifungamana na marekani ambae milele anataka autawale ulimwengu.kama hujui huo umaskini wetu wa bongo basi mmarekani anachangia, lakini kwakuwa upo huko wanakugaia dola 4 tena ndio wao hawana kosa.