Kikwete kwenda Tehrani?

Centrifuge ya Wairan iko operational my arse!! Wana-bluff tu hao hawana lolote. Hii si mara ya kwanza wala mwisho kutoa madai kama hayo na mikwara yao hewa. They are just full of hot air just like the North Koreans. The only difference is that their citizens are not starving in droves.
 
Centrifuge ya Wairan iko operational my arse!! Wana-bluff tu hao hawana lolote. Hii si mara ya kwanza wala mwisho kutoa madai kama hayo na mikwara yao hewa. They are just full of hot air just like the North Koreans. The only difference is that their citizens are not starving in droves.

Ina maana hadi wajaribu kifaa cha nyuklia kama North Korea ndipo tuwachukulie serious?
 
hivi kuna mtu anaweza kuzuia hisia za mtu ati kwa vile ameona neno fulani? Wengine wanapata hisia kwa kuona "hisia" tu kwani hilo nalo lina connotations fulani fulani. Huwezi kuzuia ndege kuruka juu ya kichwa chako, hata hivyo unaweza kuzua wasijenge kiota!

Kweli kabisa! Unaweza ukazuia wasijenge kiota and in this case kiota cha watakachojibanzia wadini ndio tunataka kuzuia...
 
Kutoka Gazeti La Majira la Leo 8/11/2007
Mjumbe wa Ahmedinejad akutana na JK

Habari Zinazoshabihiana
• Shein akutana na Balozi mpya wa Korea Kusini 08.02.2007 [Soma]
• Migiro akutana na Ki-moon 17.01.2007 [Soma]
• Amina Chifupa 'awapa' ushindi wanawake Moro 31.08.2007 [Soma]

*Aahidi kufikiria kukopesha wakulima matrekta
*Akubaliana na Rais kuanzisha kituo cha mikopo

Na Mwandishi Maalumu, Dodoma

MJUMBE wa Rais wa Irani, Bw. Mohammed Ahmedinejad, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Bw. Manouchehr Mottak, ameahidi kufikiria maombi ya Tanzania kuhusu kuanzisha kituo cha kukopesha wakulima wa Tanzania matrekta.

Bw. Mottak alisema hayo jana mjini hapa, alipozungumza na Rais Jakaya Kikwete ambaye alipendekeza Serikali hiyo kuanzisha kituo hicho ili wakulima wa Tanzania wapate zana hizo kwa gharama nafuu na kuboresha kilimo chao.

Rais Kikwete alisema iwapo Irani itakubali kushirikiana na Tanzania katika kuanzisha kituo hicho, wakulima watakopa matrekta hayo kwa gharama nafuu na kufanya kilimo chao kuwa cha kisasa na kuongeza pato lao na tija kwa Taifa.

"Kwa pamoja tunaweza kuanzisha kituo hiki ambacho kitawawezesha wakulima wetu kukopa matrekta kwa gharama nafuu na hivyo kukifanyia mageuzi kilimo chetu na kuwa cha kisasa. Lakini pia wakulima wetu watanufaika, na Taifa pia litanufaika...sisi tuko tayari kutoa ushirikiano wa karibu kama Serikali," alisema Rais.

Kuhusu uhusiano wa kidiplomasia, Bw. Mottak alisema Irani inaandaa utaratibu wa kuanzisha uhusiano wa urafiki kati yake na Afrika kama ilivyo kwa China na Afrika, ambapo maofisa wa pande hizo mbili watakutana na kufuatiwa na vikao vya mawaziri wa mambo ya nje na hatimaye mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi za Afrika na Irani.

Aidha, Rais Kikwete alimweleza Waziri huyo jinsi Tanzania inavyounga mkono wazo la Palestina kuwa Taifa huru na kwamba Tanzania inaendelea na mchakato wa upatikanaji wa amani ya kudumu katika Mashariki ya Kati.

Tarishi hauwawi.
 
Ina maana hadi wajaribu kifaa cha nyuklia kama North Korea ndipo tuwachukulie serious?

Sijali ni wakifikia wapi ndiyo tuwachukulie serious. Kwanza kuna ubaya na wao wakiwa na hizo silaha? Mbona Marekani na washirika wake including Israel wanazo? Usiniambie na wewe umenunua hii hoja ya Wamarekani kuwa baadhi ya nchi hazistahili na hazipaswi kuwa na nguvu na nyuklia (iwe kwa matumizi yoyote yale). Wamarekani wana unafiki mkubwa na wanakatabia ya kujiona wao kama ndio wateule pekee na wanastahili kuwa na vitu fulani fulani na wengine hawastahili. Nani wao aliwapa hizo haki pekee za kumiliki nyuklia?
 
nipo nashangaa tu kama Rais Kikwete ana mpango wa kwenda Tehrani hivi karibuni au hadi mwakani?

Nadhani wana JF wanashangaa kuona muungwana amekaa kipindi kirefu Ikulu akiangalia Njiwa, inabidi tumtafutie safari atumie pesa zetu walipa kodi kwenda kuomba misaada ...nafikiri IRAN itakuwa destination nzuri...
 
...mnaosema iran wanaweza kutusaidia teknoloji ya nuclear naona mna ndoto za mchana na hamko serious au hamjui kinachoendelea,ila ningependa sana Iran naye awe nalo hilo bomb maana ndio linakupatia heshima kutoka kwa wakubwa na hawawezi kukufanyia walichomfanyia Saddam...si unaona Korea everyday anasema leta chakula wanaleta,leta mafuta wanaleta,futa madeni wanafuta...damn nuclear bomb limemfanya Musharraf anakunywa coffe na tende meza moja na Bush.
 
very good point



Nafikiri Libya, Venezuela na Urusi ni mifano mizuri zaidi kuliko Irani. Na kwa upande wa Afrika tunaweza kujifunza zaidi kutoka Angola kuliko Irani. So sioni kama hiyo ni sababu kubwa zaidi.

Kwanza kwa nchi kama ya Urusi ni muhimu kuisingle out, baada ya kuwa imehadhirika sana kwa kuvunjika iliyokuwa Soviet Union, urusi kwa sasa imekita mkakati wake katika mafuta kama Silaha kuu ya Kurudi kwenye usuper power, ndio maana hata nchi za ulaya zenye kutegemea mafuta ya Urusi zinalalamika sana kutokana na ubabe wa urusi kufanya wanachotaka na mafuta yao hata kama ina "jeopardise" chumi za nchi nyingine. mfano mzuri juzi hapa warusi walifunga bomba la mafuta yanayoenda Georgia kutokana na kutokuelewana kwa mambo kadhaa. kwa hili Urusi siyo credible na kutokana na umasikini wetu hatuwezi kuleta impact yoyote katika biashara husika.
Kwa upande wa Libya, Libya hatuwezi kumuexploit kisawasawa kwa sababu sasa hivi anaenjoy diplomatic security ya hali ya juu, unlike to Iran ambayo iko under constant threats ya wakubwa, irani inahitaji diplomatic allies. kwa hiyo sisi tunaweza kuitumia opportunity hiyo kama tulivyoitumia opportunity ya china enzi hizo ilipokuwa inatengwa na wakubwa.
kwa hiyo ukiondoa hizo nchi mbili, zinabaki venezuela na iran, kati ya hizo tuchague ipi kudeal nayo zaidi?. hapa mimi ninaona ni Iran kwa sababu kwanza irani ina mafuta mengi zaidi kulikoa venezuela. na vile vile irani ipo karibu na Tanzania kuliko Venezuela gharama ya usafirishaji wa mafuta na bidhaa nyingine za kibiashara ni rahisi kwenda iran kuliko venezuela.
Kwa upande wa Angola japo mafuta yao ni kidogo kuliko Irani lakini tayari tuna contact nao mara kwa mara kupitia jumuia za kikanda katika Afrika. na pia Angola zaidi ya mafuta hawana technologia ya Nyuklia ya umeme ambayo tunaweza kujifunza kutoka kwao.na pia angola ni Nchi japo ina uchumi mkubwa kuliko sisi lakini bado ni nchi Masikini.

hii nayo ni point nzuri lakini haioneshi kwanini Irani, kwani Israeli wako mbali katika nguvu za Nyuklia na kama umeme wa Nyuklia nadhani tunaweza kujifunza zaidi kutoka Afrika ya Kusini (kuliko kufungua magroceries) kuliko Irani. Inawezekana utayari wao wa kushare teknolojia hiyo hauna conditions nyingi, au una conditions chache lakini ngumu. Sidhani watafanya hivyo kwa sababu sisi ni binamu zao.

Israeli wako mbali lakini kumbuka Uhusiano wetu na Israeli toka enzi Za mwalimu haukuwa mzuri,halafu Wairani wanatuhitaji zaidi kuliko Waisraeli ni rahisi kufanya mazungumzo na Irani kuliko israeli kwa sasa.Well la Afrika ya kusini linajadilika lakini kumbuka Raisi wa Irani Mahmoud Ahmednejad alishatoa ofa ya Wazi kabisa ,kwamba jamani eeh anayetaka hii kitu sisi tuko tayari kushirikiana naye kufanikisha hii kitu, mimi mpaka sasa sijaona Raisi yoyote duniani aliyetoa generous offer kama hii, Thabo Mbeki naye kimya tu isipokuwa raisi wa Irani


Sidhani kama hili ni kweli, vinginevyo wangekuwa wa Kwanza kupiga vita dhulma kule Darfur, Ethiopia, n.k Wao wanapinga dhulma ambazo zina maslahi kwao. Na kama kweli wao wanapinga dhulma wasingetoa vitisho vya kutaka Israeli "ifutwe kwenye ramani za dunia". Wakati wao wanapinga ubeberu wa Marekani, wao wenyewe wanaanzisha ubeberu wao dhidi ya Israeli!

Walipinga dhulma lebanon, waisrael walipowatwanga wananchi wa lebanon Mwezi mzima ,walipinga dhulma Iraq pindi Majeshi ya Uvamizi wa marekani yalipokuwa yanawaua wananchi wa Iraq ambao hawakufanya kosa lolote, kama tutakubaliana kwamba kupinga dhulma kwa mtu yeyote ni kwa faida yako pia, basi bila shaka Wairani wananufaika na principle hii,na isitoshe kila jambo lina staili yake ya kulitafutia ufumbuzi, siyo lazima jinsi ya kutafutia ufumbuzi suala la israel iwe sawa na lile la darfur

Kuhusu kauli ya "kuifuta Israeli katika ramani" serikali ya Irani imeshaitolea tamko kauli hii. Irani imesema inapinga System haipingi nchi as nchi, inapinga System ya ukandamizaji, uonevu, kutokuthamini Maisha ya binadamu wenzao, na unevu uliokithiri wa Wapalestina. kwa hiyo Tamko hilo la raisi Ahmednejad inamaanisha kufuta uonevu wa Israel katika ramani ya dunia.

Hili ni wazo zuri sana! Ila la ustaarabu sidhani kama tunaweza kujifunza ustaarabu wao wa kileo...
Ustaarabu wao wa kileo kuna mambo mengi sana ya kujifunza.
mfano iran ina ethnic group za minority ambao wameweza kuwaintegtate katika jumuia yao pasi na kutishia distinction yao.
na sisi pia Tanzania tunao ethnic group zinazohitaji care ya pekee kutoka serikalini mathalani Wahadzabe,

Pili Iran ina Wayahudi ambao ni minority pia lakini inaheshimu uhuru wao wa kuabudu vizuri kabisa.kwa mfano "antisemitism" katika Irani ni ndogo kuliko hata ya Ulaya.

Wairani leo hii Wameadvance katika medani ya Ulinzi kwa kuwathamini na kuwatumia Wataalamu wao vizuri. mfano sasa hivi irani ina lazer guided mesile iliyotengenezwa ndani na Wataalam wake yenyewe.

Wairani wana uzalendo wa hali ya juu na nchi yao na hawaombiombi misaada na wala hawazifanyii masihara rasilimali zao

Now.. you are getting where I was heading.. Hivi mtu hawezi kushangaa isipokuwa hadi ajustisfy kwanini anashangaa!? Nani alisema kushangaa ni himaya ya watu wachache? Kama wengi hawajafuatilia habari za Kimataifa jana Irani imesema centrifuge yake iko operational. Wakati huo huo US na washirika wanasema hawataiacha Irani iwe na silaha (siyo nguvu) za nyuklia. Na sisi tunaamua kujibanza na Wairani huku tunabembeleza kwa Wamarekani? What is goin on, je tunacheza bahati nasibu ya siasa za Kimataifa?

Well mimi naona kama Wamarekani wana beef na Wairani, tena beef yenyewe ni dhahiri inalenga katika dhulma, nadhani ni busara sisi kuside na upande wa Haki. Tumeshajifunza toka Vietnam na Iraq, marekani siyo mmiliki wa hii dunia na anaweza kuwa defeated na Anawahitaji walimwengu pia. sisi siasa yetu ya kutochaguliwa Marafiki ni siasa nzuri sana na nisiasa yenye misingi ya utu na heshima, nadhani tusikubali kuuza turufu yetu katika meza ya wanadamu kwa sababu ya misaada michache.
 
Hii dunia ina wenyewe,tukubali tusikubali.Ukiingia kwenye anga zao wanakubana mbavu taratibu kama Anaconda mpaka pumzi inakuishia. Iran is heading the same way pamoja na mafuta yote aliyonayo.Libya walijitutumua lakini wakasalim Amri,Mugabe kajitutumua lakini yuko taabani,North Korea hivyo hivyo sasa hivi anasambaratisha mitambo yake,Cuba taabani,Kuwa rais lazima uwe na busara kwa manufaa ya ustawi wa watu wako.Angalia Kuwait,Qatar na Saudi Arabia ambao wote wanamafuta lakini ziko mbali sana.Hizo pesa anazozitumia Irani kuendeleza hivyo vinu vya Nyuklia zitapotea bure,wenzie wanaandaa bomu maalum la kusambaratisha vinu vyake.
Mie yangu macho na masikio.
 
Jamani Mbona Mmenifutia Jina Langu La Kad'sadvocate ??

Mimi Ni Kada Jamani, Mbona Kila Siku Mnataka Nibadirishe Majina Tu ?? Mara Mnaniban, Mnanifutia Jina, Then Whats Next ?
 
Masikini Kada, una tatizo gani kwani, angalia labda unapotumia majina mengine hayatumiki vibaya halafu watu wanadhani ni mtu mwingine mleta matatizo. Pole sana.
 
bobu, sikia !

hakuna lolote, majina ni hayo tu mawili kadampinzani na kadasadvocate, sasa inakuwaje yasitumike wakati nishayatumia yote na nikaweka wazi kwamba ni mimi ?
 
Jamani Mbona Mmenifutia Jina Langu La Kad'sadvocate ??

Mimi Ni Kada Jamani, Mbona Kila Siku Mnataka Nibadirishe Majina Tu ?? Mara Mnaniban, Mnanifutia Jina, Then Whats Next ?

Ohoo Mkuu, kumbe ni wewe bwana, aisee mimi ninapinga kwa nguvu zote kumbadirishia mkuu kada jina lake, Jamani hata Mwendawazimu hupewa jina vipi Mumbadirishie kada jina lake?

Admin chonde chonde tafadhali, si vyema hata kidogo kuingilia uhuru wa Mtu kuteua jina lake ambalo halivunji kanuni za JF.

Mkuu kada ni mtu ambaye ametoa mchango mkubwa wa mawazo, hebu tuthamini muda ambao antumia kujumuika na Watanzania Wenzake kujadili mustakbali wa Taifa letu.

na mkuu kada inaonekana ni mtu mwenye nia safi, ndo maana pamoja na maumivu tele, lakini hachoki kujikongoja ili aufikishe ujumbe wa mtima wake kwa Watanzania.

Jamani Admin. Mtu hanyimwi Neno hunyimwa Tonge, vipi hali hii itokee kwa Mkuu Kada?.

Admin with due to all respect Mr sir, i hope you'll do some thing about this. -Gamba la nyoka
 
Ohoo Mkuu, kumbe ni wewe bwana, aisee mimi ninapinga kwa nguvu zote kumbadirishia mkuu kada jina lake, Jamani hata Mwendawazimu hupewa jina vipi Mumbadirishie kada jina lake?

Admin chonde chonde tafadhali, si vyema hata kidogo kuingilia uhuru wa Mtu kuteua jina lake ambalo halivunji kanuni za JF.

Mkuu kada ni mtu ambaye ametoa mchango mkubwa wa mawazo, hebu tuthamini muda ambao antumia kujumuika na Watanzania Wenzake kujadili mustakbali wa Taifa letu.

na mkuu kada inaonekana ni mtu mwenye nia safi, ndo maana pamoja na maumivu tele, lakini hachoki kujikongoja ili aufikishe ujumbe wa mtima wake kwa Watanzania.

Jamani Admin. Mtu hanyimwi Neno hunyimwa Tonge, vipi hali hii itokee kwa Mkuu Kada?.

Admin with due to all respect Mr sir, i hope you'll do some thing about this. -Gamba la nyoka

ndio mimi babu, naomba dua zako zitimie !

jamani admn. plz plz plz plz naombeni hayo majina yangu mawili, tafadhalini ! sijipi thanks, wala sijisifii kutumia hayo majina na ndio maana nikaweka wazi kwamba ndio mimi ! na majina hayo hayajakiuka misingi sheria ya JF !

asanteni !
 
kada una uhakika hauna undugu na Brazameni? nadhani watakufungulia tu.. vinginevyo inawezekana ni "kompyuta yako" ina matatizo..
 
Back
Top Bottom