Kikwete kwenda Tehrani?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
nipo nashangaa tu kama Rais Kikwete ana mpango wa kwenda Tehrani hivi karibuni au hadi mwakani?
 
Tanzania yetu inaongozwa na kulindwa na katiba yenye siasa za kutofungamana na upande wowote... macho, masikio na subira tunazo!

SteveD.
 
ninachotaka kuchokonoa ni suala la Irani na Tanzania.. Mwanzoni tulipokuwa na Urais wa Baraza la Usalama nilidhani ilikuwa ni mkakati tu wa Jamhuri ya Iran kupata kura in case wakubwa wataamua kuingilia kati.... Kuna mada nilianzisha miezi kadhaa iliyopita inayoitwa "The Iranian Connection".. Rais anaweza kwenda kokote kule, kinachonishtua ni jinsi gani kati ya marafiki zote wa mataifa ya Kiislamu duniani tunavutwa sana na wa Irani, kwanini isiwe Libya, Jordani, Morocco au Saudi Arabia au UAE?
 
Naona hii thread imeshaanza kunukia udini....mie simo

FNN, wrong.. hili halina Udini naangalia hasa kutokana na mwelekeo wa siasa za dunia sasa hivi. Hayo ya Udini wanayo wengine kwa sababu nina uhakika uhusiano wetu na Irani hautokani na msingi wa Udini kwa sababu tayari tuna nchi nyingi rafiki za Kiislamu na sikuulizia hilo... Wenye udini ni rahisi kuuona udini..
 
ninachotaka kuchokonoa ni suala la Irani na Tanzania.. Mwanzoni tulipokuwa na Urais wa Baraza la Usalama nilidhani ilikuwa ni mkakati tu wa Jamhuri ya Iran kupata kura in case wakubwa wataamua kuingilia kati.... Kuna mada nilianzisha miezi kadhaa iliyopita inayoitwa "The Iranian Connection".. Rais anaweza kwenda kokote kule, kinachonishtua ni jinsi gani kati ya marafiki zote wa mataifa ya Kiislamu duniani tunavutwa sana na wa Irani, kwanini isiwe Libya, Jordani, Morocco au Saudi Arabia au UAE?

Nani kasema kuwa uhusiano wetu na Libya, Jordani na hizo nchi zingine una mashaka?
Tuhabarishe juu ya hayo matatizo IF ANY!!!!!!!!!
 
hivi mtu unafikiri mara ngapi mpaka kuanzisha thread kama hii ambayo unajua itaamsha hisia tafauti baina ya watu? tena kwa kuandika kwamba unashangaa.fikiri kabla kuanzisha mathread yako yanayofitinisha, mjomba.
 
FNN, wrong.. hili halina Udini naangalia hasa kutokana na mwelekeo wa siasa za dunia sasa hivi. Hayo ya Udini wanayo wengine kwa sababu nina uhakika uhusiano wetu na Irani hautokani na msingi wa Udini kwa sababu tayari tuna nchi nyingi rafiki za Kiislamu na sikuulizia hilo... Wenye udini ni rahisi kuuona udini..

Haya bwana...lakini usishtuke kuona thread imekula detour kali sana na kuelekea kwenye udini na siyo kule unakotaka ielekee wewe kama unavyosema. Sometimes it is not what you say but how you say what you want to say or saying....if you get my drift
 
Ni matumaini yangu kwamba safari hii ya Muungwana itakuwa na mafanikio. Iran si tu kwamba ni Taifa ambalo sisi watanzania tunaweza kujifunza mambo mengi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kujitegemea kwa rasilimali tulizokuwa nazo lakini ni Taifa lenye kutetea Usawa na heshima kwa watu wote(mfano mzuri ni ishu ya wapalestina).

Irani ni Taifa lenye kuzalisha mafuta kwa wingi na kutokana na kuendelea kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia ni matumaini yangu kwamba raisi kikwete ataweza kufanya mazungumzo yatakayoinufaisha tanzania katika suala zima la mafuta.

na kwa hivi sasa irani inafanya maendeleo makubwa katika Sayansi kwa kutumia wataalam wake yenyewe na pia katika utafiti wa nishati Ya Kinyuklia kwa matumizi ya Amani inapiga hatua . na ukizingatia Raisi wa Iran Mahmoud Ahmednejad aliahidi alipokuwa anahutubia Umoja wa Mataifa kwamba Irani ipo tayari kusaidia nchi nyingine katika Tecnolojia hii ya umeme wa nishati ya Nyuklia ni matumaini yangu kwamba Raisi Kikwete ataitumia Fursa hii kuchangamkia Ofa hii. hasa ukizingatia matatizo ya umeme tuliyokuwa nayo, basi tunaiihitaji sana hii technolojia,

Pia Wairani wapo katika kundi la Kupinga ubeberu na Dhulma inayofanywa na baadhi ya mataifa yaliyoendelea. ni matumaini yangu kwamba Raisi Kikwete ataitumia Fursa hii kudumisha na kusisitiza msimamo wa Tanzania juu ya Haki Kwa Watu wote Pasi na kujali Mataifa yao.

Pia ningefurahi kama mheshimiwa Raisi Kikwete atazungumzia uwezekano wa kuwepo kwa scholarship kwa Wanafunzi wa kitanzania nchini irani. au uwezekano wa kuwepo exchange students kati ya hizi nchi mbili. tuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwao na wao pia kutoka kwetu kwani ni miongoni mwa jamii zenye ustaarabu wa zamani sana kabla hata ya Ulaya hii iliyo Maarufu.
 
na kwanini tuna uhusiano na marekani ambae hakuna asiejua kwamba ni taifa terrorist duniani, kwanini tusiwe na uhusiano na mataifa mengine ya kikristo kama ya ulaya mashariki.basi tu una lako kama wenzangu walivyokwisha sema hapa.
 
hivi mtu unafikiri mara ngapi mpaka kuanzisha thread kama hii ambayo unajua itaamsha hisia tafauti baina ya watu? tena kwa kuandika kwamba unashangaa.fikiri kabla kuanzisha mathread yako yanayofitinisha, mjomba.

Neno "nashangaa" mara nyingi lina connotations mbaya...na ktk ishu zinazohusu Iran kama Mwanakijiji alivyoandika linaweza kabisa likaleta mlipuko wa hisia kali na watu kuishia kutukanana...
 
FNN na Under age hebu acheni majibishao yasiyo kuwa na maana. kama hamna ishu za kujadili Hebu tulieni kwanza watu tukate ishu!
 
nadhani kafungwa macho na siasa , imekuwa siasa mbele ,hisia baadae.pia bado anatawaliwa kifikira na super power nations kama usa na uingereza. hivyo adui wa marekani ndio aonekane adui ulimwengu mzima. tunaishi kwenye dunia ya reality, usifate mshengesha wa marekani kasema, fuata reality na reality tayari gamba la nyoka kaitoa .tutasoma mengi tukifungamana na iran kuliko tukifungamana na marekani ambae milele anataka autawale ulimwengu.kama hujui huo umaskini wetu wa bongo basi mmarekani anachangia, lakini kwakuwa upo huko wanakugaia dola 4 tena ndio wao hawana kosa.
 
Ni matumaini yangu kwamba safari hii ya Muungwana itakuwa na mafanikio. Iran si tu kwamba ni Taifa ambalo sisi watanzania tunaweza kujifunza mambo mengi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kujitegemea kwa rasilimali tulizokuwa nazo lakini ni Taifa lenye kutetea Usawa na heshima kwa watu wote(mfano mzuri ni ishu ya wapalestina).

very good point

Irani ni Taifa lenye kuzalisha mafuta kwa wingi na kutokana na kuendelea kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia ni matumaini yangu kwamba raisi kikwete ataweza kufanya mazungumzo yatakayoinufaisha tanzania katika suala zima la mafuta.

Nafikiri Libya, Venezuela na Urusi ni mifano mizuri zaidi kuliko Irani. Na kwa upande wa Afrika tunaweza kujifunza zaidi kutoka Angola kuliko Irani. So sioni kama hiyo ni sababu kubwa zaidi.

na kwa hivi sasa irani inafanya maendeleo makubwa katika Sayansi kwa kutumia wataalam wake yenyewe na pia katika utafiti wa nishati Ya Kinyuklia kwa matumizi ya Amani inapiga hatua . na ukizingatia Raisi wa Iran Mahmoud Ahmednejad aliahidi alipokuwa anahutubia Umoja wa Mataifa kwamba Irani ipo tayari kusaidia nchi nyingine katika Tecnolojia hii ya umeme wa nishati ya Nyuklia ni matumaini yangu kwamba Raisi Kikwete ataitumia Fursa hii kuchangamkia Ofa hii. hasa ukizingatia matatizo ya umeme tuliyokuwa nayo, basi tunaiihitaji sana hii technolojia,

hii nayo ni point nzuri lakini haioneshi kwanini Irani, kwani Israeli wako mbali katika nguvu za Nyuklia na kama umeme wa Nyuklia nadhani tunaweza kujifunza zaidi kutoka Afrika ya Kusini (kuliko kufungua magroceries) kuliko Irani. Inawezekana utayari wao wa kushare teknolojia hiyo hauna conditions nyingi, au una conditions chache lakini ngumu. Sidhani watafanya hivyo kwa sababu sisi ni binamu zao.

Pia Wairani wapo katika kundi la Kupinga ubeberu na Dhulma inayofanywa na baadhi ya mataifa yaliyoendelea. ni matumaini yangu kwamba Raisi Kikwete ataitumia Fursa hii kudumisha na kusisitiza msimamo wa Tanzania juu ya Haki Kwa Watu wote Pasi na kujali Mataifa yao.

Sidhani kama hili ni kweli, vinginevyo wangekuwa wa Kwanza kupiga vita dhulma kule Darfur, Ethiopia, n.k Wao wanapinga dhulma ambazo zina maslahi kwao. Na kama kweli wao wanapinga dhulma wasingetoa vitisho vya kutaka Israeli "ifutwe kwenye ramani za dunia". Wakati wao wanapinga ubeberu wa Marekani, wao wenyewe wanaanzisha ubeberu wao dhidi ya Israeli!

Pia ningefurahi kama mheshimiwa Raisi Kikwete atazungumzia uwezekano wa kuwepo kwa scholarship kwa Wanafunzi wa kitanzania nchini irani. au uwezekano wa kuwepo exchange students kati ya hizi nchi mbili. tuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwao na wao pia kutoka kwetu kwani ni miongoni mwa jamii zenye ustaarabu wa zamani sana kabla hata ya Ulaya hii iliyo Maarufu.

Hili ni wazo zuri sana! Ila la ustaarabu sidhani kama tunaweza kujifunza ustaarabu wao wa kileo...

Now.. you are getting where I was heading.. Hivi mtu hawezi kushangaa isipokuwa hadi ajustisfy kwanini anashangaa!? Nani alisema kushangaa ni himaya ya watu wachache? Kama wengi hawajafuatilia habari za Kimataifa jana Irani imesema centrifuge yake iko operational. Wakati huo huo US na washirika wanasema hawataiacha Irani iwe na silaha (siyo nguvu) za nyuklia. Na sisi tunaamua kujibanza na Wairani huku tunabembeleza kwa Wamarekani? What is goin on, je tunacheza bahati nasibu ya siasa za Kimataifa?
 
Neno "nashangaa" mara nyingi lina connotations mbaya...na ktk ishu zinazohusu Iran kama Mwanakijiji alivyoandika linaweza kabisa likaleta mlipuko wa hisia kali na watu kuishia kutukanana...

hivi kuna mtu anaweza kuzuia hisia za mtu ati kwa vile ameona neno fulani? Wengine wanapata hisia kwa kuona "hisia" tu kwani hilo nalo lina connotations fulani fulani. Huwezi kuzuia ndege kuruka juu ya kichwa chako, hata hivyo unaweza kuzua wasijenge kiota!
 
nadhani kafungwa macho na siasa , imekuwa siasa mbele ,hisia baadae.pia bado anatawaliwa kifikira na super power nations kama usa na uingereza. hivyo adui wa marekani ndio aonekane adui ulimwengu mzima. tunaishi kwenye dunia ya reality, usifate mshengesha wa marekani kasema, fuata reality na reality tayari gamba la nyoka kaitoa .tutasoma mengi tukifungamana na iran kuliko tukifungamana na marekani ambae milele anataka autawale ulimwengu.kama hujui huo umaskini wetu wa bongo basi mmarekani anachangia, lakini kwakuwa upo huko wanakugaia dola 4 tena ndio wao hawana kosa.

badala ya kuangalia hoja, unaanza mashambulizi ya mtu!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom