Kikwete huna adui ila wewe mwenyewe ndiye adui

CCM original

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
373
Reaction score
68
Nimekuwa msomaji mzuri sana wa mijadala mbalimbali hapa jamvini. Labla kutokana na sababu binafsi nilishindwa kupata maamuzi ya kuwa pamoja na kujadili hatma ya taifa letu.

Nimekuwa nikifuatili kwa makini sana juu ya maoni, ushauri, kejeli, matusi na dhihaka kwa Rais kikwete na serikali yake.

Aidha nimeshindwa kuamini kama uhuru wa maoni unaweza kutumiwa kwa "busara" ya namna hii.

Naandika leo kwa mara ya kwanza hapa JAMIIFORUMS "kumkumbusha" rais wangu kipenzi kuwa yeye ndiye adui kwa taifa hili kwa kufuga maadui.

Maadui wa taifa hili ni hawa wafuatao.

Mafisadi.
Rais wangu umewaonea haya hawa watu hawa. Unawajua kwa majina ila hekina, busara na upole wako wameutumia vibaya. Leo wamekaa pembeni wakishuhudia unavyotukanwa.

CHADEMA, hawa watu wanataka kuaminisha watanzania kuwa "wakiingia madarakani basi matatizo yote kwisha". Wanajenga chuki badala ya kukosoa na kuishauri serikali. Wanawaaminisha watanzania kuwa "wanataka kuwapeleka peponi watanzania" iwapo watawachagua kuongoza nchi. Wanataka kuwaambia watanzania miaka 52 tangu uhuru CCM hawajafanya jambo lolote. Wameamua kuingia hadi ktk uvunjifu wa amani ili kutafuta umaarufu(cheap populality).

CHADEMA wameamua kuteka na kuua ili kuitupia Lawama CCM. Ichukiwe mbele ya wapenzi wake wanaoiamini na bado wanaipenda na kuiamini. Lakini rais Kikwete amewakalia kimya "watu hawa".

Ndo maana nachelea kusema rais wangu wewe mwenyewe ndo adui. Unajiua mwenyewe kwa kuacha watu wawe na uhuru holela wa kutoa maoni yao.

Hali hii imesambaa hadi kwenye "mass media". Unakuta wanahabari nguli kabisa anakosoa badala ya kuhitimisha kwa mapendekezo ya suluhu anaishia kukosoa na kulaumu na kupiga vijembe na matusi rejareja.

Rais wangu, tazama mfano wa mwenzako Y. Museven, amewazuia "waandishi uchwara" kuandika au kuripoti kamja hana shahada ya habari. Wewe umewaacha hadi wenye astashahada wakuzomee kwenye "vigazeti".

Kiiza besige alipotaka kuwamobilize watu kama wafanyavyo CHADEMA ili kuvunja amani na kuchochea amani "akasimamishwa kuleta fujo".

Rais wangu mpendwa wewe umeamua kwa maksudi kuwa mpole na wanakuonea kwa kuwa wanajua kuwa umeamua "kuwapotezea".

Ushauri wangu kwako kuwa hujachelewa. Amua moja, kuwa makini na wanaohatarisha amani ya taifa. Ama sivyo nitaamini HUNA ADUI WEWE MWENYEWE NDO ADUI kwa kutoamua kukomesha hali hii.

Tunaogopa kung'olewa kucha na meno bila ganzi.
 
Mbunge wa Kigoma Mjini wee!.
Kuna watu ambao kuishi nao ni kama kubeba gunia la misumari.

Nina shaka mleta mada unaishi kwa shemeji yako, vinginevyo usingeandika maneno ya kula kulala namna hii.

Kweli cdm ni mwiba kwa wengi sana ndiyo maana haitoki midomoni mwenu.

Mbunge wa Mtera!
 
kama mara ya kwanza hamna noma mkuu,we kwako museven ndie unamungopa,nimekaa hapa kampala miaka4 sasa hakuna rais kilaza kama museven ,fanya utafiti kabla huja post kitu
 
kama Museven kilaza muulize kiiza besige
 
kama mara ya kwanza hamna noma mkuu,we kwako museven ndie unamungopa,nimekaa hapa kampala miaka4 sasa hakuna rais kilaza kama museven ,fanya utafiti kabla huja post kitu

Ila huyu wa magamba anatisha huwezi kumlinganisha na m7 mwenye maamuzi.Ubaya wewe m23 ze marcopolo sumu na wengineo mnafikiria kwa masaburi.Umeenda Ug kuuza mi2mba nini au we ni houseboy
 
CHADEMA wameamua kuteka na kuua ili kuitupia Lawama CCM. Ichukiwe mbele ya wapenzi wake wanaoiamini na bado wanaipenda na kuiamini. Lakini rais Kikwete amewakalia kimya "watu hawa".

Hali hii imesambaa hadi kwenye "mass media". Unakuta wanahabari nguli kabisa anakosoa badala ya kuhitimisha kwa mapendekezo ya suluhu anaishia kukosoa na kulaumu na kupiga vijembe na matusi rejareja.

Tunaogopa kung'olewa kucha na meno bila ganzi.

Kwa hiyo unamaana CCM wangemkamata LEMA kwa tuhuma za UCHOCHEZI waache kukamata wanaong'oa kucha na meno ya watu?..

Mwangosi pia kauawa na nani? Kama si maagizo ya sisiem kwa vyombo vya usalama?

Acha Uongo.. Kibanda na Ulimboka wameteswa na kuumizwa na usalama wa taifa.
 
Gaddafi alitumia nguvu kubwa ya jeshi lake lakini niambue aliishia wapi?

Muulize Mubaraka nae na ubabe wake aliishia wapi?

Msiendelee kumpotosha JK, kwani ameshapotoshwa vya kutosha!

Hakika wewe ndie umtakii mema JK na wewe ndie adui namba moja wa JK!

Wewe ni wa kuogopwa kama ukoma!
 
ukitumia CIA au FBI kujua kuwa usalama wa taifa ndio waliomteka Dr. Ulimboka? CCM kwa kutumia vyombo vyake wamemnasa mtu wenu CHADEMA anapanga kuua watanzania wanaowaomba ridhaa ya kuingia ikulu.
 
Gaddafi alitumia nguvu kubwa ya jeshi lake lakini niambue aliishia wapi?

Muulize Mubaraka nae na ubabe wake aliishia wapi?

Msiendelee kumpotosha JK, kwani ameshapotoshwa vya kutosha!

Hakika wewe ndie umtakii mema JK na wewe ndie adui namba moja wa JK!

Wewe ni wa kuogopwa kama ukoma!

Huyo kwenye red haamini anavyobebwa kwenye cage kama kinda la bata,cheza na nguvu ya umma!
 
Ni kweli mhe. rais hana adui, ila Tanzania ina maadui, tena bahati mbaya zaidi maadui wa Tanzania wamekuwa watanzania wenyewe, unapomuona mtanzania yeyote anaewashabikia CHADEMA kwa namna yeyote ile na kuichukia serikali yake, basi huyo ni adui wa nchi yake mwenyewe.

Tatizo lililopo hapa ni uzalendo, serikali ilifanya makosa sana kuondoa mafunzo ya JKT chini ya utawala wa mzee Mwinyi kwa vijana wa kitanzania, kwani hawa wote humu JF wanaoipinga serikali ndio walewale waliokosa mafunzo ya kujenga utaifa, ukakamavu, hekima na busara.

Huwezi kuichukia serikali hama chama kilichoshika dola hata kidogo, ni sawa na mtu kumchukia mzazi wako heti kisa hakujali hama ana tabia za ulevi, wananchi wanapoamua chama fulani kiunde dola, hata kama wewe ukipendi hiko chama unapaswa kuiheshimu serikali.

"CHADEMA NDIE ADUI NAMBARI MOJA WA TAIFA"
 
CHADEMA wameamua kuteka na kuua ili kuitupia Lawama CCM. Ichukiwe mbele ya wapenzi wake wanaoiamini na bado wanaipenda na kuiamini. Lakini rais Kikwete amewakalia kimya "watu hawa".

Tunaogopa kung'olewa kucha na meno bila ganzi.

Wewe Mnyakyusa?.. Wanyakyusa ndiyo target ya sisiem na mafisadi?... Ulimboka, Mwangosi, Mwakyembe na Kibanda ni Wanyakyusa wewe je?
 
Ni kweli mhe. rais hana adui, ila Tanzania ina maadui, tena bahati mbaya zaidi maadui wa Tanzania wamekuwa watanzania wenyewe, unapomuona mtanzania yeyote anaewashabikia CHADEMA kwa namna yeyote ile na kuichukia serikali yake, basi huyo ni adui wa nchi yake mwenyewe.

Tatizo lililopo hapa ni uzalendo, serikali ilifanya makosa sana kuondoa mafunzo ya JKT chini ya utawala wa mzee Mwinyi kwa vijana wa kitanzania, kwani hawa wote humu JF wanaoipinga serikali ndio walewale waliokosa mafunzo ya kujenga utaifa, ukakamavu, hekima na busara.

Huwezi kuichukia serikali hama chama kilichoshika dola hata kidogo, ni sawa na mtu kumchukia mzazi wako heti kisa hakujali hama ana tabia za ulevi, wananchi wanapoamua chama fulani kiunde dola, hata kama wewe ukipendi hiko chama unapaswa kuiheshimu serikali.

"CHADEMA NDIE ADUI NAMBARI MOJA WA TAIFA"

Mbona Mwigulu katoka JKT juzi lakini uzalendo wake ni zero!
 
Ni kweli mhe. rais hana adui, ila Tanzania ina maadui, tena bahati mbaya zaidi maadui wa Tanzania wamekuwa watanzania wenyewe, unapomuona mtanzania yeyote anaewashabikia CHADEMA kwa namna yeyote ile na kuichukia serikali yake, basi huyo ni adui wa nchi yake mwenyewe.

Tatizo lililopo hapa ni uzalendo, serikali ilifanya makosa sana kuondoa mafunzo ya JKT kwa vijana wa kitanzania, kwani hawa wote humu JF wanaoipinga serikali ndio walewale waliokosa mafunzo ya kujenga utaifa, ukakamavu, hekima na busara.

Huwezi kuichukia serikali hama chama kilichoshika dola hata kidogo, ni sawa na mtu kumchukia mzazi wako heti kisa akujali hama mlevi, wananchi wanapoamua chama fulani kiunde dola, hata kama wewe ukipendi hiko chamag. unapaswa kuiheshimu serikali.

"CHADEMA NDIE ADUI NAMBARI MOJA WA TAIFA"

Pole sana ila tambua CDM imeshika hatam ila nakusikitikia sana kwani unashindwa kuubali ukweli.LKN sitokulaumu couse ni ujinga ulio nao kichwan mwako.ADUI mkubwa wa kikwete ni CCM hususani watendaji wake walivyo majambazi na majangili ambao bdo ni viongozi wa ccm.
 
Mbona Mwigulu katoka JKT juzi lakini uzalendo wake ni zero!

wewe na mwigulu nani mzalendo? Wewe umefanya lipi la uzalendo la kujivunia na kukumbukwa? Mchango wa mwigulu uko dhahiri. Au kuwaumbua watesaji wa raia ndo kakosa uzalendo?
 
CHADEMA, hawa watu wanataka kuaminisha watanzania kuwa "wakiingia madarakani basi matatizo yote kwisha". Wanajenga chuki badala ya kukosoa na kuishauri serikali. Wanawaaminisha watanzania kuwa "wanataka kuwapeleka peponi watanzania" iwapo watawachagua kuongoza nchi. Wanataka kuwaambia watanzania miaka 52 tangu uhuru CCM hawajafanya jambo lolote. Wameamua kuingia hadi ktk uvunjifu wa amani ili kutafuta umaarufu(cheap populality).

CHADEMA wameamua kuteka na kuua ili kuitupia Lawama CCM. Ichukiwe mbele ya wapenzi wake wanaoiamini na bado wanaipenda na kuiamini. Lakini rais Kikwete amewakalia kimya "watu hawa".

Hali hii imesambaa hadi kwenye "mass media". Unakuta wanahabari nguli kabisa anakosoa badala ya kuhitimisha kwa mapendekezo ya suluhu anaishia kukosoa na kulaumu na kupiga vijembe na matusi rejareja.

Ushauri wangu kwako kuwa hujachelewa. Amua moja, kuwa makini na wanaohatarisha amani ya taifa. Ama sivyo nitaamini HUNA ADUI WEWE MWENYEWE NDO ADUI kwa kutoamua kukomesha hali hii. Tunaogopa kung'olewa kucha na meno bila ganzi.

"CHADEMA NDIE ADUI NAMBARI MOJA WA TAIFA"

Majangili, Mafisadi na wahujumu uchumi wengine ni marafiki wa Taifa?!!!!!, .... Mmmmm hhii ni Bongoland BWANA!
 
Back
Top Bottom