Nimekuwa msomaji mzuri sana wa mijadala mbalimbali hapa jamvini. Labla kutokana na sababu binafsi nilishindwa kupata maamuzi ya kuwa pamoja na kujadili hatma ya taifa letu.
Nimekuwa nikifuatili kwa makini sana juu ya maoni, ushauri, kejeli, matusi na dhihaka kwa Rais kikwete na serikali yake.
Aidha nimeshindwa kuamini kama uhuru wa maoni unaweza kutumiwa kwa "busara" ya namna hii.
Naandika leo kwa mara ya kwanza hapa JAMIIFORUMS "kumkumbusha" rais wangu kipenzi kuwa yeye ndiye adui kwa taifa hili kwa kufuga maadui.
Maadui wa taifa hili ni hawa wafuatao.
Mafisadi.
Rais wangu umewaonea haya hawa watu hawa. Unawajua kwa majina ila hekina, busara na upole wako wameutumia vibaya. Leo wamekaa pembeni wakishuhudia unavyotukanwa.
CHADEMA, hawa watu wanataka kuaminisha watanzania kuwa "wakiingia madarakani basi matatizo yote kwisha". Wanajenga chuki badala ya kukosoa na kuishauri serikali. Wanawaaminisha watanzania kuwa "wanataka kuwapeleka peponi watanzania" iwapo watawachagua kuongoza nchi. Wanataka kuwaambia watanzania miaka 52 tangu uhuru CCM hawajafanya jambo lolote. Wameamua kuingia hadi ktk uvunjifu wa amani ili kutafuta umaarufu(cheap populality).
CHADEMA wameamua kuteka na kuua ili kuitupia Lawama CCM. Ichukiwe mbele ya wapenzi wake wanaoiamini na bado wanaipenda na kuiamini. Lakini rais Kikwete amewakalia kimya "watu hawa".
Ndo maana nachelea kusema rais wangu wewe mwenyewe ndo adui. Unajiua mwenyewe kwa kuacha watu wawe na uhuru holela wa kutoa maoni yao.
Hali hii imesambaa hadi kwenye "mass media". Unakuta wanahabari nguli kabisa anakosoa badala ya kuhitimisha kwa mapendekezo ya suluhu anaishia kukosoa na kulaumu na kupiga vijembe na matusi rejareja.
Rais wangu, tazama mfano wa mwenzako Y. Museven, amewazuia "waandishi uchwara" kuandika au kuripoti kamja hana shahada ya habari. Wewe umewaacha hadi wenye astashahada wakuzomee kwenye "vigazeti".
Kiiza besige alipotaka kuwamobilize watu kama wafanyavyo CHADEMA ili kuvunja amani na kuchochea amani "akasimamishwa kuleta fujo".
Rais wangu mpendwa wewe umeamua kwa maksudi kuwa mpole na wanakuonea kwa kuwa wanajua kuwa umeamua "kuwapotezea".
Ushauri wangu kwako kuwa hujachelewa. Amua moja, kuwa makini na wanaohatarisha amani ya taifa. Ama sivyo nitaamini HUNA ADUI WEWE MWENYEWE NDO ADUI kwa kutoamua kukomesha hali hii.
Tunaogopa kung'olewa kucha na meno bila ganzi.