Kikwete baba tunakukumbuka na tunazidi kukukumbuka

Kikwete baba tunakukumbuka na tunazidi kukukumbuka

Uliweza kuwavumilia hata uliokuwa ukitofautiana nao kimtazamo bila kuwasimanga na kuwanyanyasa. Penye utata ulikaa na waponzani mkashauriana hadi kufikia muafaka, hukutawala miiili ya watu, uliongoza mioyo ya watu, ulisubir kabla ya kutoa matamko, uliwatia watanzania moyo penye ugumu, ulikubali kukosolewa na kufanya mabadiliko pale penye mapungufu. Ulijenga miundo mbinu nchi nzima, Barbara, vyanzo vya umeme vya uhakika. Kiufupi Umeweka misingi ya Tanzania endelevu , ktk demokrasia na miundombinu. Mungu atakulipa.
 
Jakaya alikuwa na akili nyingi sana za kisiasa akawahadaa wapuuzi waliodhani ni dhaifu kisiasa.
Mbinu ya kumshinda adui yako ni kujifanya dhaifu ili avimbe kichwa kama vile chui akinyatia kitoweo
Alimtumia Sitta kumsambaratisha Lowasa 2007
Alimtumia Lowassa 2010 kumsambaratisha Sitta 2010 kwny uspika.
Akawatumia Chadema kusambaza Sumu za wizi wa Lowassa kwa wananchi 2007-2015.
Kawatumia Maadui zake kutimiza malengo ya kisiasa kuliko marafiki zake
The art of war.
-when you are strong make your enemy think you are weak.
-when you are weak,make your e nemy think that you are strong
 
Tusiwe vigeugeu kiasi hiki huu ni unafiki na uzandiki wa kiasi chake
Bob ni tunda la JK , mapungufu yao yanafanana kwa ujumla wake
JK alikuwa mwanasiasa kuliko mtendaji, bob ni mtendaji hana siasa
JK alisikiliza sana watu, bob hasilizi yeyote
Wote hawa wawili walishindwa kubalance siasa na utendaji
Mkuu vipi kuhusu maisha ya mtanzania kwa sasa je utalinganisha maisha yalivyokuwa kipindi cha JK na sasa? miezi tisa tu hii majanga je huko tunapoelekea?? nadhani hali iliyopo kwa sasa wewe haikugusi kabisa mkuu hakuna unafuu sana sana wananchi tunakufa njaa tu.
 
Jk tutakukumbuka kwa safari zako za ulaya zisizoisha na uhuru wa kula bata kwa watumishi wa umma ila huyu magu anazunguka hapahapa tz tu huku akizidi kuwasomesha namba wananchi wote kwa ujumla
 
Mkuu vipi kuhusu maisha ya mtanzania kwa sasa je utalinganisha maisha yalivyokuwa kipindi cha JK na sasa? miezi tisa tu hii majanga je huko tunapoelekea?? nadhani hali iliyopo kwa sasa wewe haikugusi kabisa mkuu hakuna unafuu sana sana wananchi tunakufa njaa tu.
Hali ni mbaya sana na hii ni matokeo ya hicho nilichoandika
 
Ivi wana ccm wanashabikia uongozi uliopo kunanini nyuma ya pazia kuna ka neema wanapata zaidi au maana hali ilivyo ngumu bado mtu anashabkia hali ngumu. Na hali iko wazi mwelekeo hauonekani kabsaa. Sasa mashabiki wa ccm ni akili yakuchambua mambo hamna au kuna mgao mnaupata

Kila kitu ni sawa kila kitu mzee akiongea hakikoselewi au kwasababu jamaa kajivika u mungu hamuwez mkosoa.
 
Hivi mnafikiri magufuli ndo kaanza kazi?,bado sana hizo ni mvua za rasharasha tu,kasema sasa ameamua kuongeza dozi ya kutumbua,ha ha,yaani tutalimia meno safari hii
 
The art of war.
-when you are strong make your enemy think you are weak.
-when you are weak,make your e nemy think that you are strong
Nimekupata vyema sana Mkuu!
Kwny Kinyang'anyiro cha Uspika wa Bunge la Katiba Chadema wakaingizwa tena Mkenge kwa kumkampenia Sitta wakidhani atakuwa against Jakaya badala ya Chenge waliodhani ndo Pro Jakaya. Mara zote maadui wa Jk walishindwa kuitambua Karata ya ushindi ya Jk kabla ya pambano
 
NAMMISI SANA JK kwa kweeli...we acha tuu...
Mke/mume ukiwa nae huoni faida, ila akiondoka ndio unajua faida yake.....sasa tunalia..
Ulikuwa huna hiyana na mtu....
Sasa tunadai tunanyoosha watu tunaoumia ni sisi wa chini mwisho wa siku.
Sukari mwisho wa siku sisi wa chini wenye kipato duni ndio tunabakia kununua kwa bei ile ya juu
Pesa haionekani, bajeti sisizowezekana zinalazimishwa zote kwa mkupuo wkt fungu hakuna. Mwisho wa siku tunaokosa hela na chakula ni sisi wa chini.. Tutakukumbuka baba JK.
 
Watanzania tulio wengi hatuna ujasiri wa kuwakoromea watawala wetu.

Hivi unadhani Watanzania wanaweza wakafanya uasi wa kupinga watawala waliopo madarakani?

Mi bado sijauona huo ujasiri aisee.


Sababu hatukuzoea hali ya vita, na hasa ukizingatia vizazi hivi vya sasa mfano vijana wa sasa hawakupitia hali ya vita, babu zetu ndio walipitia hali ya vita, hii ndio maana tunakuwa wagumu kupinga. Ukiona tuu kifaru kinakuja unaweza ukazimia kabla hakijafika. Bado sana watanzania..Amani yetu imetufanya tuwe wapole
 
Jpm ndio mzuri zaidi ya jpm heshima inaonekana mtaani napenda sana watumishi wa serikali wanavyolia njaa, natamani jpm akaze zaidi


Huyo mtumishi wa Serikali akilia njaa usifikiri itaishilia kwake tuu, hata wewe itakukuta....Wa juu akikosa wa chini nawe ndio unakosa zaidi sababu hawezi gawa au mpa mtu wakati yeye hajapata.....
Sasa hivi hata Waosha magari, wapiga mizinga hawapati kitu. Ila kipindi cha JK akija mtu akikulilia naomba sh. 500 unatoa unampa sasa hakuna. Wasiokuwa na mishahara na biashara zisizoeleweka sasa wataula wa chuyua...vibaka wataongezeka zaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom