Kikwete azidiwa jukwaani, akimbizwa mapumziko

pole sana mkuu jk ila asisahau afya yake ni muhimu kuliko kazi, na fikiri anahitaji uangalizi wa madaktari zaidi vinginevyo mzee ataliacha jukwaa huku akiwa bado analipenda. bado tunazihitaji busara na hikma zako kipindi kijacho cha uongozi. mungu akuponye linalokusumbua.
 
pole sana muheshimiwa kwa yaliyokusibu..ila mbona waenda sana mwanza wkt huku mbeya twataka kukuona pia..uje ututembelee..kulikoni huko mwanza..kuna siri gani mzee..tuna mashaka sana raia wako..mbona mbeya huji?????
halafu bado tunakuhitaji..punguza misele..wewe una makamu wa rais,kuna waziri mkuu,mawaziri kibao kuliko mabaraza yaliyowahi kuwepo nchini..sasa kwanin huwatumi hao..kila mara wataka kupanda mandege tu...ukifululiza kuzurula yatakukuta kama hayo..baki dar fanyakazi...nchi isije ikakushinda
 
Maneno yako hapa chini mkuu ni mazito sana. Kwa mtu mwelewa hahitaji kujiridhisha juu ya ukweli wake. Reading between the lines naona wewe uko karibu sana sana na info za huyu prezo wetu. Mhh inatisha though.
Ni kweli muungwana ni mgonjwa anasumbuliwa na ninadhani ni tatizo la NERVE katika sehemu za medula oblangata kwa lugha ya kitaalam, na kwa taarifa nilizonazo baada ya kuanguka pale jangwani wakati anamalizia kampeni zake za Urais 2005 alipata kutibiwa na Daktari mmoja huko ufaransa na alishauri afanyiwe upasuaji lakini muungwana hakukubaliana na hilo. Baadae akapata Daktari mmarekani nadhani wa Boston ambaye anamtibu mara zote kwa kumpatia dawa, na huyu Daktari kamshauri aachane na kazi za siasa baada ya 2010 kwani ndizo zinampatia stress na tatizo alilonalo halihitaji stress, lakini madaraka matamu hataki kufuata masharti ya Dr.

Huyu Dr wa marekani ndo yule alimleta akampeleka mbuga za wanyama na baadae alitoa misaada pale MOI. Tatizo hili la kupoteza fahamu na ku collapse limekuwa likimtokea mara kwa mara hata akiwa IKULU tu, nakumbuka ile ziara ya mkoani Mbeya aliopopolewa mawe alipata kuanguka pia katika moja ya shughuli zake za ndani ikulu ndogo ya huko.

Mimi nawashauri wasaidizi wa Rais wawaambie watanzania ukweli, waache kutupamba kwa maneno kuwa anafanya kazi nyingi ndo maana ananguka, wawaeleze watanzania tatizo la msingi la afya ya Rais wao. Hizi safari za Marekani kila kukicha ni danganya toto, kinachompeleka huko ni matibabu tu.
 
kwa hiyo inawezekana hizi trip za mara kwa mara za Marekani ni doctor's appointments? maana sidhani kuna raisi aliyekuwa akienda huko maranyingi kama Kikwete
 
Does he excercise, what does his diet consist of, when was his last vacation?

A healthy body and mind are essential for such a stressfull and punishing schedule.
 
mhhh labda lile jini lake la kike liliotajwa na sheik yahya ndo lilikuwa
linataka kutoka baada ya maombi.....................
tutaona mengi mwaka huu.........
 
Hili tatizo la ugonjwa Mwanakijiji aliwahi kulidokeza hapa ama kwenye Cheche (sikumbuki vyema). Lakini hakutoa details kama alizotoa Ndanda To Lomwe kwenye post yake.

Tatizo la sisi waswahili tunachanganya mambo mengi kwa wakati mmoja. Ugonjwa unaweza kuwa unatibika kwa tiba za kisasa (hospitalini), lakini bado tutaenda kwa waganga wa kienyeji kuagua na kuangalia nani mbaya wako anaekuroga. Waganga wa kienyeji kwa kawaida huwa hawakosi maelezo, ambayo in most cases ni uongo tu. Na hasa ukizingatia kwamba JK ni Rais kwa hiyo mganga anaemtibu lazima atakuwa anaona ujiko sana kumtibu Rais wa nchi.

Bwana Philemon Mikael kwenye post yake anasema msafara wa Rais ulionekana Dar mishale ya saa 3 usiku ukitokea Bagamoyo, may be alipotua airport alienda kwa mganga wake ili kuona kama kuna rafu amechezewa huko Mwanza.

Kwa mwendo huu tunaweza kumpoteza hivi hivi kwa sababu za kijinga ama kuamini matunguli ambayo hayatamponya ama kumpa nafuu.
 
Kikwete hatogombea mwakani; tulilidokeza hili a while ago. Tunamuombea afikie uamuzi huu mapema zaidi ili apate muda wa kushughulikia afya yake.
 
Does he excercise, what does his diet consist of, when was his last vacation?

A healthy body and mind are essential for such a stressfull and punishing schedule.

Alpha,

Is that even a question? just by looking, do you think that's a work out body? and he has all the time in the world, they should have a gym, Ikulu, and a personal trainer (am ready to volunteer for their own good)......I suggest!
 
Are you guys for Real?

WOW!.........JUST WOW!

MUNGU IBARIKI TANZANIA!
 
Na bado......mwaka huu tutaona wapi zaid Bagamoyo or in the midst of the presence of Almight God. Watu wa Mungu jamani wakazane kuomba. 2010 is just around the corner. If it happened at Kirumba, it can happen all over the country.

GOD BLESS TANZANIA!
 
For this case, majengo ya Ikulu yote inabidi iwekewe mikono na kutakaswa na kupakwa mafuta na kuzungukwa mara saba, kuitishwa moto na kukemewa kwa Jina la Yesu. It's scary to think that whoever step their foot over there, needs serious prayers under the name of Jesus. GOD BLESS TANZANIA
 
Jamani watanzania hili liwe funzo kwetu, Jangwani raisi wetu alianguka akiutubia watanzania, na sasa ameanguka tena akiutubia waanglikana, vyote ni udhaifu/uchovu wa mwili. Sasa tuseme NO, kila mgombea urahisi apimwe afya yake kwanza na majibu yawekwe adharani kwa watanzania wajue wanamchagua mtu wa namna gani. Kwani ata hali ya afya ufanya mawazo ya mtawala yawe na mwelekeo bora au dhaifu.
pole rais wangu JK
 
kwa nini kila siku yeye na si wengine?,mara ya kwanza ilikuwa Viwanja vya jangwani wakasema alikuwa kwenye mfungo wa Ramadhani na swaumu ilisababisha ,tukio lingine ni hili akiwa ameshiba mapishi yaliyothibitishwa na kwa uangalifu mkubwa hata wa Doctor ..!!
 
Utampima wapi na kuhakikisha vipi objectivity?
 
Alpha,

Is that even a question? just by looking, do you think that's a work out body? and he has all the time in the world, they should have a gym, Ikulu, and a personal trainer (am ready to volunteer for their own good)......I suggest!

Mimi pia ni mtaalamu wa mazoezi najitolea pia ku mtrain Mh! Rais kwenye aerobic for free kabisa every day 1 hr. Ikulu ni pm tuanze kazi.
 
kwa nini kila siku yeye na si wengine?,mara ya kwanza ilikuwa Viwanja vya jangwani wakasema alikuwa kwenye mfungo wa Ramadhani na swaumu ilisababisha ,tukio lingine ni hili akiwa ameshiba mapishi yaliyothibitishwa na kwa uangalifu mkubwa hata wa Doctor ..!!
 
Jamani watanzania hili liwe funzo kwetu, Jangwani raisi wetu alianguka akiutubia watanzania, na sasa ameanguka tena akiutubia waanglikana, vyote ni udhaifu/uchovu wa mwili. Sasa tuseme NO, kila mgombea urahisi apimwe afya yake kwanza na majibu yawekwe adharani kwa watanzania wajue wanamchagua mtu wa namna gani. Kwani ata hali ya afya ufanya mawazo ya mtawala yawe na mwelekeo bora au dhaifu.
pole rais wangu JK

huu mkutano haukuwa wa "Waanglikana", ulikuwa wa AICT ambalo ni kanisa linaloitwa African Inland Church of Tanganyika (....nzania).

maninkus
 
Rais Jakaya Kikwete leo amepatwa tena maswaibu yaliyomkuta Mwanza wakati wa kampeni 2005 akiwania kura za Watanzania huko Mwanza, safari hii siyo kwa kukabwa na Msukuma, bali afya kutetereka.

Afya ya Rais Kikwete ilitetereka akiwa jukwaani akihutubia waumini wa Kanisa la AICT na wananchi katika Kiwanja cha Kirumba ambapo iijisikia vibaya na kubebwa na watu wa usalama kutoka jukwani hadi chumba cha watu maarufu katika uwanja huo kwa mapumziko.

Rais Kikwete baada ya kuwa huko kwa mapumziko mafupi alirejea na kuendelea na hotuba yake.

Inawezeana ni uchovu wa safari kama alivyosema na safari hii amesema hatarudia 'mchezo' wa kuunganisha safari ili apate muda wa kupumzika.

Pole Rais Kikwete

Pole sana Mpendwa Rais wetu. Mwenyezi Mungu akulinde, akupe afya na mema mengi, uweze kuiongoza Nchi yetu Tanzania hadi mwaka 2015. Amen.
 
Back
Top Bottom