Kikwete ateua Mwandishi Mpya wa Hotuba: Msafiri Wilbert Marwa

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
5300192.jpg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Agosti 17, 2011, amemteua Bwana Msafiri Wilbert Marwa kuwa Mwandishi wa Hotuba Msaidizi wa Rais. Uteuzi huo unaanza mara moja.

Kabla ya uteuzi wake, Bw. Marwa alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mwandamizi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Bw. Marwa (39) alijiunga na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Januari 1999 na tokea Agosti 2004 alifanya kazi katika Ubalozi wa Tanzania mjini Addis Ababa, Ethiopia kabla ya kurejea nyumbani mwaka jana.

Bw. Marwa ana Shahada ya Kwanza ya Biashara (Bachelor of Commerce) kutoka Chuo Kikuu cha Mysore, India na Diploma ya Juu kutoka Kituo cha Centre for Foreign Relations cha Dar es Salaam.
Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu,
DAR ES SALAAM.
17 Agosti, 2011
 
mwandishi wa hotuba asiye na sifa za uandishi ndio maana tunasikia Raisi na hotuba zenye vituko. Ninapita tuuu
 
Kuwa muandishi lazima usomee uandishi?

Mwandishi mteule ana sifa yoyote ya uandishi? Kuna andiko lake hata moja linaloweza kuwekwa hapa?

Angalau hata January tumemsoma tangu Young African.com, na pamoja na kigugumizi chake pamoja na matatizo yote ya Kikwete nobody can tell me that January is on the South end of a policy wonk. Sasa kama January pamoja na pedigree and all that hakuweza kutoa a memorable speech itakayo wa inspire Watanzania for generations, kwa nini tutegemee kipya kutoka huyu Msafiri Marwa ?

Halafu hivi Foreign ndo kuna monopoly ya vipanga Tanzania?
 
Mwandishi mteule ana sifa yoyote ya uandishi? Kuna andiko lake hata moja linaloweza kuwekwa hapa?

Angalau hata January tumemsoma tangu Young African.com, na pamoja na kigugumizi chake pamoja na matatizo yote ya Kikwete nobody can tell me that January is on the South end of a policy wonk. Sasa kama January pamoja na pedigree and all that hakuweza kutoa a memorable speech itakayo wa inspire Watanzania for generations, kwa nini tutegemee kipya kutoka huyu Msafiri Marwa ?

Halafu hivi Foreign ndo kuna monopoly ya vipanga Tanzania?

Mkuu inategemea unataka uandishi wa namna gani kama ushahidi. Ila kama foreign service officer ni lazima ilitakiwa aandika reports mbali mbali na pia kama afisa ubalozi tena Addis Ababa it is quit possible kasaidia kuandika hotuba ya raisi one way or another. Cha muhimu ni hicho kuulizia ila siyo kumdiscredit moja kwa moja.
 
Sikuwahi kufikiria kuna mtu seriously kaajiriwa kuandika

hizo hotuba za kikwete...

Well what if kungekuwa hakuna kabisa mtu wa kuandika?

Awe anaandaa mwenyewe........
Sipati picha.....
 
Sikuwahi kufikiria kuna mtu seriously kaajiriwa kuandika

hizo hotuba za kikwete...

Well what if kungekuwa hakuna kabisa mtu wa kuandika?

Awe anaandaa mwenyewe........
Sipati picha.....

Kazi ya kumuandikia raisi tabu tupu maana inategemea unamuandikia raisi gani. Kuna mtu unamuandikia speech akiongea anaongea mambo tofauti kabisa na ulicho kiandika. Au unamuandikia mwishoni anapiga editing mpaka ulicho andika wewe kina potea kabisa.
 
Kuwa muandishi lazima usomee uandishi?

Unajua mwandishi sio amabye anadata za hotuba, bali hutumia data ambazo zinahitajika kutoka kwenye sehemu husika ili kuziweka pamoja na kuandika hotuba. Sasa kama kweli kazi ni uandishi tulitegemea kuona mwandishi mwenye uwezo, elimu, na uzoefu wa uandishi na lugha husika. Sasa sijui huyu wetu kazi yake haswa ni nini?

Inawezekana tunatumia vigezo vya juu sana kuliko vinavyotakiwa ikulu. labda Critics wangejibu kazi hasa ya mwandishi wa hotuba ya raisi wa Tanzania ni ipi ili tujue. Inawezekana ni kanyaga twende ilmradi raisi kaongea.

wenzetu huwa wanakuwa na timu ya waandishi wa ikulu, ambao wanataalamu nzuri za lugha na uandishi. Kwani kuwa na points ukishindwa kuzipangilia unaweza kuaharibu unayotaka kusema. Taaluma na uzoefu ni muhimu sana. Na je huyu mwandishi ni wa lugha gani kwani najua tunatumia lugha mbili. Nimesikiliza hotuba nyingi za Mkuu wa kaya za Kiswahili na kiingireza huwa najiuliza ni nani anayeziandika, kwani ziko kama mwandishi alikurupushwa, hazina hamasa wala mtitiririko wa kiandishi na kuweza kuuza mada husika.

Shamba la bibi kula kwa zamu.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Sikuwahi kuhisi wala kupata clue kwamba MArwa was good in writing.............

congrats pal and waiting to hear from you very soon

By the way, yule Kairuki vipi?
 
hongera sana kwani kwa jinsi ninavyomfahamu kijana huyu si uandishi tu bali ata biashara na uchumi anaufahamu sana kila la heri ila usigeuke ukawa kama salva
 
Nitasema kitu kimoja: huwezi kumuandikia mtu hotuba ambaye haamini katika kile ulichoandika. Vinginevyo ataonekana kama TV au radio tu! Na siri haiko katika kuandika hotuba tu bali pia katika kutoa (delivery) Kikwete ni miongoni mwa Marais ambao wanatoa hotuba vibaya sana kiasi kwamba huwa naamini ni mateso na ukiukwaji wa haki za wasikiilizaji. Lakini hili tatizo la kudeliver haliko kwa Kikwete tu nimeona pia kati ya watendaji mbalimbali; inatisha.

Lakini kwa vile watu walimchagua yeye na chama chake well, they have to learn to live with it.
 
Hivi mwaandishi wa habari wa preside ana kazi gani? Maana naona hotuba zake anapotembelea taasisi mbalimbalii zinaandikwa na wenyeji wake (mara nyingi hata editing huwa hafanyi). Utasikia rais kasema hivi, kaahidi kile, etc. kumbe ni mawazo ya watu baki. Hata mimi (si mwandishi wa habari na wala sijui policies zao) nilishawahi kushiriki kumuandikia hotuba fulani na akaireproduce kama illivyo hadharani.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Naomba mnijulishe hili tafadhali kwa anayejua J.K Nyerere alikuwa anaandikiwa na nani
 
majibu yenu yako hapa:

waliomba thread ifutwe au ihamishwe kwani bosi wa Foreign kila akiingia anakuta watu wanamkamulia tuu kijana wake


https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/120080-ministry-of-farce-affairs-aka-foreign-afairs.html




sijui kwa nini unawachukia foreign na wala sijui jamaa walikuboa nini lakini naona ukingangania jambo lako mpaka kieleweke

let it go. Mbopo mwenyewe keshaamua kuachia ngazi lakini naona unaye tuu \

walau wao wanajitahidi kwa nini huwabebei bango ikuliu kama unavyofanya na hawa foreign?

eti ministry of farce affairs
 
Mnafikiri kazi ya Muandishi wa hotuba wa Rais ni kukaa na kungoja kuandika hotuba tu? Hebu ongeeni mambo ya maana saa zingine.

Mshenga kisha leta habari humu, nyinyi ama ipokeeni au msiipokee. Mtaanza majungu, fitina, ujinga. Hivi siasa zenu ni za kuongelea watu? Huo unaitwa umbea na si siasa.

Ndio maana sera za simenti mfuko shs 500 hatujaona zikitekelezeka majimboni kwenu mpaka leo.

Great minds talks about ideas, nyinyi kwa kuongelea watu hampo hata kwenye average minds. Mpo kwenye kundi la mwisho la "poor minds". Tena hizo akili zenu ni masikini kweli kweli.
 
Back
Top Bottom