Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,713
Katika mwendelezo wa ziara ya Jakaya Kikwete nchini Kenya, leo Rais Jakaya Kikwete ametembelea City Hall Nairobi na kukutana na gavana wa Nairobi, Evans Kidero. Rais Kikwete amesema anaamini ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Kenya utaimarika zaidi kama matokeo ya ziara yake.
Pia Rais Kikwete ameahidi kuendelea kuzuru nchini Kenya hata baada ya kustaafu kwake, Rais Kikwete alifanyiwa sherehe ya kukabidhiwa funguo za kuingilia mji wa Nairobi kama ishara ya upendo. Katika hatua nyingine barabara ya milimani(Milimani road) imebadilishwa jina na sasa itaitwa Jakaya Kikwete Road.
Baada ya hapo, Rais Kikwete alitembelea kiwanda cha magari nchini Kenya, General Motors(GM). Kiwanda hicho kimelalamikia Tanzania kuiwekea vikwazo kwa madai kuwa ni kiwanda cha uunganishaji na sio kutengeneza magari hivyo kutopata nafuu iliyopo kwenye ushirikiano wa Afrika Mashariki. Rais Kikwete akijibu hilo amesema ameona na atarudi kuwaambia watanzania ili kuona jinsi gani watasonga nalo mbele.
Last edited by a moderator: