Kikwete asimulia alivyoiba wali JKT!

Kikwete asimulia alivyoiba wali JKT!

Rais Mwizi ww ubwabwa? .... Hii pekee unatosha kupima uwezo ww Rais wetu mtukufu
 
kuna mtu hapa jukwaani ambae hajawahi hata kuiba sukari jikoni?
kuna mtu hapa hajawahi kuiba mlo wa mwenzake akiwa boarding? lau hata mikate au majani chai?
Jk amekiri na watanzania tuache unafiki wa kumwandama mtu anaesema kweli.
 
Kumbe ndio maana hadi leo ni mwizi wa pesa za Epa na za walipa kodi Lol kweli amepata uzoefu JKT kutoka wali hadi pesa za walipa kodi kweli huyu amekubuhu
 
Laiti kama hotuba hii ingepita kwa wasaidizi wake kwa kuiandaa wangemzuia kutamka swala la yeye kuiba akiwa JKT. Maana maneno yatakuwa meng sana
 
NDO MAANA ALIPOINGIA MADARAKANI NA MASWAIBA WAKE edward lowasa na rostam azizi KUJITENGENEZEA KAMPUNI FEKI LA RICHMOND....
 
RAIS Jakaya Kikwete amesimulia maisha yake ya jeshini, huku akikumbuka namna alivyokamatwa na mkuu wa jiko (afande ubwabwa) akiiba wali. Rais Kikwete alitoa ushuhuda huo wakati akifunga mafunzo maalumu ya uongozi kwa wabunge na kuzindua mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria.

Hafla hiyo ilifanyika juzi katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha 832 KJ, kilichopo Ruvu, Kibaha mkoani Pwani, ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria.

Rais Kikwete aliwakumbusha vijana hao kwamba yeye ni miongoni mwa watu waliochukua mafunzo ya JKT kambini hapo akiwa katika Operesheni Tumaini mwaka 1972.

Rais Kikwete alisema katika mafunzo hayo alijengwa vizuri, ingawa hadi leo bado anakumbuka matukio mawili ya kufurahisha na kusikitisha akiwa kambini hapo.

Alisema tukio la kwanza ambalo hawezi kusahau ni pale alipokamatwa akiiba wali na tukio jingine ni kuhusu kifo cha askari mwenzao aliyefariki dunia baada ya kukanyagwa na trekta.

"Nawashukuru kwa kunialika katika shughuli hii, nimetembelea na kujionea miradi mbalimbali inayoendelea kufanywa hapa kambini.

"Wakati tukiwa kule nilikuwa naangalia kwa makini, hasa nilikuwa naangalia lile bweni letu, sisi tuliokuwa Kombania A mwaka ule, nimepakumbuka ingawa sasa pamekarabatiwa vizuri.

"Yapo matukio mawili ninayoyakumbuka siwezi kuyasahu hadi leo wakati nikiwa hapa kambini…(kicheko) jeshi si mchezo, nawaeleza haya mjue maisha ya jeshi hayana mzaha.

"Nakumbuka namna nilivyokamatwa na bwana ubwabwa nikiiba wali kule katika bwalo la chakula," alisema Rais Kikwete huku wananchi na askari wanafunzi (kuruta) waliokuwapo wakiangua kicheko.

Rais Kikwete aliendelea kusema. "Katika kombania yetu tulikuwa na mchezo siku zikipikwa nyama na wali tunaiba tunakwenda kuficha kisha baadaye tunakuja kula baada ya kazi.

"Sasa siku hiyo ilikuwa zamu yangu kuiba wali, kama kawaida nikachukua mestini zangu mbili nikachukua wali ili nikafiche, natoka tu nje, hamad! afande ubwabwa huyu hapa mlangoni (kicheko).

"Akaniambia piga magoti, huku nimeshikilia mestini zangu za wali. Akaniambia hivi! Brother maana alikuwa anapenda sana kuita brother, wewe ni form six (kidato cha sita) umekuja kuchukua mafunzo.

"Huko juu kuna makamu wa rais anaitwa Rashid Mfaume Kawawa, akisikia kwamba kuna kijana wa form six ameiba wali kambini atafurahi?

"Nikamwambia hapana, akasema kama hivyo ndivyo acha tabia hiyo, akanikanya nisiendelee na tabia ile. Nilikamatwa lakini nilifanikiwa kuondoka kwa huruma.

"Tukio la pili ninalokumbuka ilikuwa ni masuala ya kufundisha, tulikuwa tunakwenda Misugusugu kulikuwa na umwagiliaji katika skimu ya mpunga.

"Sasa tukiwa tunajiandaa zilifika habari kambini kwamba kuna askari mwenzetu amekanyagwa na trekta amefariki dunia, tukiwa bwenini nikapaza sauti ‘Stanley kuna habari gani, nasikia askari amekanyagwa na trekta'.

"Wakati napiga kelele, sikujua kumbe huyo ninayemwita ndiye aliyepatwa na janga hilo, tulienda kule barabarani kujua mazingira ya kifo yalikuwaje.

"Tulipofika pale tuliambiwa kwamba mwenzetu alikuwa amepanda trekta na alikaa kwenye madi gadi huku akila muwa, kwa bahati mbaya aliteleza akaanguka na kukanyagwa na tairi kubwa," alisema Rais Kikwete huku watu wakisikitika.

Rais Kikwete pia alitumia fursa hiyo kuwaeleza vijana hao chimbuko la kuanzishwa kwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ambapo vijana wanaomaliza kidato cha sita watajiunga na jeshi hilo kwa mujibu wa sheria kabla ya kujiunga na vyuo.

Rais Kikwete alisema JKT ilianzishwa mwaka 1963 na kwamba msingi wake mkuu ni kutoa fursa kwa vijana kujifunza na kujenga umoja wa taifa.

Akielezea historia ya jeshi hilo, Rais Kikwete alipinga madai ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakidai kuwa wananchi walisomeshwa bure chini ya utawala wa awamu ya kwanza.

"Wazo la kuanzisha JKT lilianzia TANU Youth League, 10/07/1963 wazo lilitolewa na aliyekuwa katibu wake, Joseph Nyerere wakati huo, ndiye aliyependekeza JKT ianzishwe.

"Aprili 19, 1963 Baraza la Mawaziri liliridhia uanzishwaji wake. Sheria namba 64 ya mwaka 1966 ilitungwa na hapo JKT ilianza kupokea vijana wasomi wa elimu ya juu.

"Enzi zetu mafunzo ya JKT yalikuwa miezi 5 kambini, halafu miezi 18 kazini, baadaye unarudi kumalizia mwezi mmoja.

"Ilikuwa huwezi kuanza kazi bila kupitia JKT. Katika miezi yako 18 ya kazi, hapakuwa na ruhusa ya kuchukua mshahara wote.

"Unachukua asilimia 40 ya mshahara wako, asilimia 60 inayobaki Serikali inachukua kufidia gharama zake za mafunzo ya JKT, suala la kwamba watu walisoma bure katika nchi hii mimi silioni.

"Tumedhamiria kuboresha na kuongeza uwezo wa JKT ili iweze kutimiza wajibu wake. Jeshi hili lina wajibu mkubwa katika kuwajenga vijana na suala zima la uzalishaji mali," alisema.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Kaimu Mkuu wa Kambi hiyo, Luteni Kanali Menas Mbele na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza.

Katika hatua nyingine, wabunge 25 wameshindwa kujiunga na mafunzo ya JKT yaliyofanyika katika kambi mbalimbali nchini, licha ya kujiandikisha.

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, wabunge 47 walijiandikisha, lakini wabunge walioripoti kambini ni 24 na waliohitimu mafunzo hayo ya wiki tatu ni 22 tu.

Wabunge waliohitimu mafunzo maalumu ya uongozi katika Kambi ya 832 KJ, Ruvu ni pamoja na Mbunge wa Mchinga, Said Mtanda, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.

CHANZO
:MTANZANIA

.........Laiti kama kila mtu akelezea maisha ya utoto na ujanan wengi tumefanya mengi kushinda hili... sio ishu
 
Mshua akitoka ikulu atakuwa na utitiri wa visa vya kuiba,kumbe ndo maana anawasamehe wahujumu uchumi wa EPA,yeye alisamehewa kwa uhujumu wa msosi!
 
Someones background(Characteristics) is essential for a society to decide type of leaders and leadership.
 
Yaani Amiri Jeshi Mkuu kakosa yote ya kuhadathia yahusuyo jeshi anahadithia vitu hivi?

Mengine kama anayaona muhimu sana ayaandikie kitabu auze, hapo sio pahala pake
 
Safi sana jk kwa kueleza ukweli mtu! Wote mnaye mkosoa hapa mi na waona ni wapu.mbafu na wangese tu
 
Bwana ubwabwa ndo sababu ya haya yote anayoyafanya uyu jamaa mpaka wa leo kwani nna uhakika kama angefukuzwa JKT sidhani kama tungekuwa na mwizi anayeitwa kikwete ktk nchi ii...
 
Aliana kuiba ubwabwa leo anaiba billions......kweli wizi unaanzaga taratibu
 
mwiziiiiiiiii....hakutakiwa kusimulia hilo kwa wadhifa alionao sasa
 
Big deal! Y'all need to loosen up!

Mtu katoa kistori chake cha jeshini ambacho kusema ukweli ni youthful indiscretion.

Hadhira iliyokuwepo imecheka.

Sasa hapa watu lawama tu.

Je angekiri kutumia unga au kuvuta bangi enzi za ujana wake?
 
Laiti kama hotuba hii ingepita kwa wasaidizi wake kwa kuiandaa wangemzuia kutamka swala la yeye kuiba akiwa JKT. Maana maneno yatakuwa meng sana

Wasio pitia jeshi ndo wataongeeea, lakini ni jambo la kawaida na ni moja ya mbinu za kuwa mjanja !
Kula mapema ua kumanuva na kupata msosi bila maafande kujua kunaitwa 'mashituzi' ! Na kuficha kiporo, haswa cha wali kilikuwa kikiitwa 'kijogoo'
JKT huli bila kujulikana siku hiyo ulifanya kazi wapi ! Wewe kimbia kimbiaaa, lakini break ya mwisho kwenye gudulia !
 
.........Laiti kama kila mtu akelezea maisha ya utoto na ujanan wengi tumefanya mengi kushinda hili... sio ishu

Watu wanapiga mbuzi mzima, anachinjwa kisha anafukiwa kwenye shimo ambalo juu yake unakoka moto. Nyama inaiva kama imepikwa kwa microwave !
 
Yeye ni muwazi anaeleza kile alichokifanya wakati ule jamani!!!!!hata wewe kumbuka historia yako uiweke basiQUOTE]

Wengi tuliopita majeshi tuna visa kibao tulivyofanya tukiwa majeshi.

Kuna jamaa yetu, alimlamba Kapteni wa Jeshi, mkuu wa kombania !
Habari ikavuja mpaka kwa CO ! Hapakukalika kombania A coy ! Uzuri hawakuwa na uhakika ni nani !
 
Back
Top Bottom