Kikwete ashauri Serikali kupunguza gharama za matibabu kwa watoto wenye Usonji hasa hospitali za Serikali ambazo zinatumia kodi za wananchi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ameishauri Serikali na wamiliki wa hospitali kuangalia upya gharama za mazoezi tiba yanayotolewa kwa watoto wenye usonji ili kuwawezesha kupata huduma hiyo.

Kikwete alitoa ushauri huo Dar es Salaam juzi, alipozungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyolenga kuchagisha fedha za kuwasaidia watoto wenye ugonjwa huo unaoathiri mawasiliano na uhusiano na kusababisha changamoto kubwa katika malezi

Hafla hiyo iliandaliwa na taasisi ya Lukiza Autism Foundation.

Kikwete alisema kwa taarifa alizonazo kwa kila zoezi moja ambalo watoto hupashwa kufanyiwa, hugharimu Sh 20,000 kwa muda wa dakika 20 Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Sh 50,000 kwa dakika 45 hospitali binafsi.

Alisema ikiwa mtoto atafanyiwa mazoezi yote sita kila siku, mzazi atalazimika kulipa Sh 300,000 kwa wiki au milioni 1.2 kwa mwezi kwa gharama za Muhimbili.

“Haya mazoezi tiba ndiyo yanayowasaidia kupata nafuu, sasa gharama ni kubwa, ni matajiri pekee watakaomudu, lakini hata kwa familia tajiri labda kwa kina Mo (Mohamed Dewji).

“Tutafute namna ya kuzitazama gharama hizi. Na hili ni suala la kukaa wadau na Wizara ya Afya na hili litazamwe hata watu binafsi. Lakini kwa Muhimbili ambayo ni hospitali ya Serikali, lazima tulitazame hili kwa sababu na kodi zetu zinakwenda kule,” alisema Kikwete.

Pia alishauri wadau mbalimbali kusaidia upatikanaji wa basi maalumu la kuwapeleka shule watoto wenye usonji ili kuwaepusha wazazi wao na adha ya usafiri wanayokumbana nayo kwa kukataliwa kupanda kwenye usafiri wa umma unaobeba waru wengi kutokana na watoto hao kufanya vurugu pale wanapoingia.

Alisisitiza kufanyiwa kazi ushauri uliotolewa na mmoja wa walimu wanaowahudumia watoto wenye usonji wa Shule ya Msimbazi Mseto, aliyeshauri kuanzishwa kwa shule ya bweni ili kutoa nafasi kwa wazazi wao kuweza kufanya kazi za maendeleo kwani kwa sasa wanapowapeleka watoto wao shule hulazimika kusalia shuleni kuwangoja hadi masomo yamalizike.

Alisema pamoja na maboresho makubwa yaliyofanyika katika sekta ya afya nchini kwa sasa ikilinganishwa na huko nyuma, ikiwamo kuongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba, lakini safari bado ni ndefu, hivyo juhudi zaidi zinahitajika.
 
Hizo garama sina uhakika km zipo sahihi
 
Back
Top Bottom