Kikwete anastahili sifa

AAH Ukiwa kwenye payroll yake huoni baya. Sasa sisi wa kambo ndio kibano. JK Afanye mambo mawili tu nitamwona wa pekee moja atengue mikataba ya umeme pili ampeleke slaa mahakamani kwa kumchafua.[/QUOTE
Today they are crawling out of the woodwork. The Kikwete acolytes.
 
Mijitu mingine ina mawazo mgando kweli, haya nieleze mifumo ya kikwete imesaidia nini katika kuzuia ubadhilifu wa mali za umma? mifumo mingi imewekwa kwa mashinikizo ya nchi wahisani baada ya kugundua pesa zao za misaada hawaoni matumizi yake kwenye maendeleo ya nchi. zamani kipindi cha nyerere mtu alikuwa akigundulika anamakosa anachukuliwa hatua kama unabisha kawaulize wakina mwinyi uone walichofanywa na mwalimu. leo unamsifia bosi wa magamba ya ruswa, ufisadi na unyonyaji unaakili kweli au unafikiri kwa kutumia ******. bila shaka ww utakuwa mke wa bosi wa magamba.
 
kweli anastahili sifa kwa hili.
ila elewa kupanda mbegu si kazi, kazi ni kupalilia na kuukinga dhidi ya wadudu waharibifu
tatizo lake riporti anazikalia tu ili upepo upite
tuone sasa kama atachagua baraza jipya,dogo na lenye kuwajibika lisilokuwa la kishkaji
 
Umpe sifa kwan wewe nan? Sifa zako zina umuhim gan? Ukimsifia ataongezeka nn? Usipomsifia atapungukiwa nn? Wanaomsifia wanatosha sifa zako peleka kwa yule mshkaj wako!

Umempa jibu linalomfaa ..
 
Ndiyo anastahili sifa maana ni mpenda sifa mno. Ndio maana kila wakati anasubiri mpaka mwisho aone upepo unakwendaje ndipo anarukia jambo ili tu yeye ndiye apate sifa. Mwisho wa siku atahakikisha wengine wote wanachafuka na kubaki yeye tu msafi. Mimi namsifia tu kwa staili yake ya uongozi inayoiangamiza CCM.

Alipoamua CAG iwe inatoa ripoti ya ukaguzi mapema zaidi na alipomteua Utoh na alipompa uwezo wakukagua wizara, idara na taasisi zote zinazopewa fedha na serikali na alipoamua ripoti ikajadiliwe bungeni alikuwa anangoja aone upepo wako unaelekea wapi au sio?

Ngojeni Utoh aanze kuingia na kukagua ofisi za vyama vya siasa vinavyopewa ruzuku na Serikali ndipo mtakapo muelewa vizuri Kikwete. Muoneni anacheka cheka tu yule ni "chaguo la Mungu".
 
Mwanzo nilikuchukulia juu juu, lkn sasa naona upuuzi wako haupaswi kupuuzwa. Msijitie ubingwa wa kumkosoa Nyerere, nakuhakikishia kuwa hata kama ni hali ngumu, basi ilitokana na hali halisi na sio uzembe. Hakukuwa na wasomi wala teknolojia tulionayo leo na exploitation ya resources zetu haikuwa ya kiasi hiki.

Huu unaoturudisha nyuma kwa sasa ni uzembe. Wasomi kibao lkn serikali legelege. Na hili la kusema enzi za Nyerere tulikuwa hatuna ruksa ya kusema nao ni upuuzi. Ulitaka useme nini?

Halafu sisi tulioko mjini story za Nyerere kuchoma Benki Kuu kwetu ni upuuzi

Huo ni ufinyu wa mawazo ulionao na waliokudanganya. Hali ngumu ya kukosa wasomi? kabla hajachukuwa nchi na mpaka miaka sita baada ya kuwa madarakani, kabla hajafanya ujinga wa kutaifisha mali za watu, Tanganyika na Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza katika Afrika kusafirisha mazao ya kilimo nje. Baada ya upuuzi wa kutaifisha tukawa ombaomba wa mwisho duniani. Au hulijuwi hilo? Funguwa akili japo kidogo ufikiri ilikuwaje hakuna wasomi tukawa wasafirishaji wa kwanza wa mazao katika Afrika? na ilikuwaje miaka sita tu baadae akaharibu kila kitu tukawa ombaomba? The man was a total failure. Usitake kusifia ujinga.
 
Baada ya Rais Kikwete kuunda upya mfumo wa ukaguzi wa mahesabu ya Serikali na baada ya kulazimisha ukaguzi huo uwe unafanywa kwa haraka zaidi, sio kama ilivyokuwa kwa uongozi wa kabla yake, na baada ya kufanya kila njia hesabu hizo ziwe zinajadiliwa kwa uwazi bungeni. Tunaona matunda yake.

Kikwete, unastahili kila sifa njema kwa kuwa mwenye kutoa na kufanya maamuzi kidemokrasia bila kuchukuwa hatua mkononi mwako (udikteta). Tunaona CAG ilivyofanya kazi, hakuna aliyetegemea kama itakuwa hivi.

Wapinzani, wameirukia hoja kama vile ni ubunifu wao, wanasahau kuwa wewe ndiye muasisi wa huu mfumo mpya na wewe ndiye uliyemteua Utoh.

Wanasahau pia kuwa wewe ndiye uliyeamuwa na kuanzisha mfumo wa hizi ripoti za mkaguzi mkuu zijadiliwe bungeni, hakuna aliyekuwa na moyo huo kabla yako. Mungu akuweke uendelee kuonesha njia.

Nakuhunga mkono mkuu, huyu jamaa anaona mbali sana we sema tu baadhi ya viongozi wenzake wanamwangusha sana; na inasikitisha zaidi pale raia wanaposema kwamba baadhi ya viongozi alikuwa anajuana nao tangu enzi za ujana wake, sasa kama ndiyo hivyo kwa ubinadamu wa kawaida mtu ungetegemea kwamba viongozi wa namna hiyo ndio wangekuwa wanafanya kazi marudufu hili waonyeshe mfano mzuri kwa wenzao, lakini wapi bwana yaani hao ndiyo wanakuwa vinara wa kufanya madudu, sasa unafikili Mh. JK anajisikiaje mwoyoni mwake kuangushwa na watu walio karibu naye - mtu mwenye roho nyepesi unaweza kuchanganyikiwa kabisa. JK ni binadamu mvumilivu sana.

Mimi jana nilimwangalia kwa makini wakati anafungua Jengo la CAG, kusema kweli sura yake ya haiba ilifutika kabisa! alionekana hana furaha hata kidogo, na hii sikawaida yake, sababu za kuonekan hana furaha ni obvious; vile vile hotuba yake iligusia sana umuhimu wa CAG na alisema wazi wazi kwamba CAG asiogope mtu yeyote hata kama ni mawaziri - akampa CAG ruksa ya kufanya kazi zake bila kuingiliwa na mtu yeyote, mtu mwenye akili unajua JK alikuwa anatuma ujumbe gani wa Watendaji wakuu. Watu tunasahau kwamba yeye ndiye aliye ipa meno CAG sasa kama ndiyo hivyo kwa nini tuwe na wasi wasi naye kuhusu ukomeshaji wa ufujaji wa fedha za UMMA na ufisadi.

Mwisho JK huyu huyu ndiye aliye wezesha Tanzania kuteuliwa na kupewa kazi ya ukaguzi wa mahesabu za UN Agancies, hili si jambo la kawaida - maana yake ni kwamba International Community inamuheshimu na kumsikiliza sana JK - lakini sisi hapa nyumbani tuna mbeza beza tu, mimi naona cha muhimu ni kumpa ushirikiano na ushauri, mimi sina tatizo naye namuona mtu ambaye yuko truely independent minded, actions speaks volume I mean angalia uteuzi wake kamati ya kukusanya maoni ya kurekebisha katiba - we unafikili angekuwa mtu legelege au mtu anaye endekeza majungu zile sura zilizo kuwa zinakusoa chama na serikali yake wazi wazi bila woga zingekuweno kwenye list, tuwe wakweli hapa - sasa huyo ndiye the real JK.

 
Kwani uliposema tumsifie ni yeye anayefanya hesabu za CAG?

Sasa tusifie nini basi? Tusifie mfumo au matokeo ya jumla ya kazi? Kweli wewe kilaza. Kwa hiyo ukiwa unasahihisha mitihani, yule aliyepiga mistari vizuuuuri ktk karatasi la majibu ndio shujaa wako hata kama baada ya hiyo mistari hakuandika jibu lolote?! Duh, kweli kikwete ana washauri

Huyo CAG aliteuliwa na Slaa? kwa hiyo msifie Slaa.
 
Mijitu mingine ina mawazo mgando kweli, haya nieleze mifumo ya kikwete imesaidia nini katika kuzuia ubadhilifu wa mali za umma? mifumo mingi imewekwa kwa mashinikizo ya nchi wahisani baada ya kugundua pesa zao za misaada hawaoni matumizi yake kwenye maendeleo ya nchi. zamani kipindi cha nyerere mtu alikuwa akigundulika anamakosa anachukuliwa hatua kama unabisha kawaulize wakina mwinyi uone walichofanywa na mwalimu. leo unamsifia bosi wa magamba ya ruswa, ufisadi na unyonyaji unaakili kweli au unafikiri kwa kutumia ******. bila shaka ww utakuwa mke wa bosi wa magamba.

Unajuwa kushinikizwa? uliza kuhusu Nyerere na Tiny Rowlands, utajuwa maana ya kushinikizwa.
 
Baada ya Rais Kikwete kuunda upya mfumo wa ukaguzi wa mahesabu ya Serikali na baada ya kulazimisha ukaguzi huo uwe unafanywa kwa haraka zaidi, sio kama ilivyokuwa kwa uongozi wa kabla yake, na baada ya kufanya kila njia hesabu hizo ziwe zinajadiliwa kwa uwazi bungeni. Tunaona matunda yake.

Kikwete, unastahili kila sifa njema kwa kuwa mwenye kutoa na kufanya maamuzi kidemokrasia bila kuchukuwa hatua mkononi mwako (udikteta). Tunaona CAG ilivyofanya kazi, hakuna aliyetegemea kama itakuwa hivi.

Wapinzani, wameirukia hoja kama vile ni ubunifu wao, wanasahau kuwa wewe ndiye muasisi wa huu mfumo mpya na wewe ndiye uliyemteua Utoh.

Wanasahau pia kuwa wewe ndiye uliyeamuwa na kuanzisha mfumo wa hizi ripoti za mkaguzi mkuu zijadiliwe bungeni, hakuna aliyekuwa na moyo huo kabla yako. Mungu akuweke uendelee kuonesha njia.

Your argument is very weak. hapana kikwete hastahili sifa kwa hilo kwakuwa ni wajibu wake kama mkuu wa nchi kufanya hivyo asipo fanya hivyo atafanya nani? pia misingi ya utawala bora na uwazi inamuelekeza kuwa hizo ripoti ziwe wazi kwakuwa ni mali ya public. pia wapinzani hawajadakia kama ulivyodai kwa kuwa wapinzani ni watu makini kama vile MAKAMANDA WA CHADEMA NA SIO HAO VILAZA WENU WAZEE WA MAGAMBA AMBAO WAMEKUTUMA UANDIKE ****
 
[h=3]Udhaifu wa Kikwete kadiri nilivyojiridhisha leo ni mwoga kwani anaiogopa sana CCM na ndio maana ameamua kutumia katiba ya CCM kuongoza nchi badala ya Katiba ya nchi. Rais anapoomba ridhaa ya kufanya mabadiliko baraza la mawaziri kutoka chama kimoja cha siasa maana yake anaiongoza nchi kwa katiba ya chama hicho badala ya kufuata katiba ya nchi inavyotoa mwongozo katika kuongoza nchi.[/h]
Soma: [h=3]Tanzania yaongozwa na Katiba ya CCM au Katiba ya nchi? Kikwete aiogopa CCM?[/h]
 
Kwa kweli huu uwazi aliotoa rais, ungesifiwa tu kama angekuwa responsive, tatizo la rais wangu kikwete ni kuteua watu kwa kuangalia eneo, kabila, dini na vingine visivyo vya maana na si utendaji. Na ndo maana wanamdondosha!
 
Akimwezesha CAG kutoa riport za wizara ya ulinzi, mambo ya ndani, ofisi ya Rais na Waziri mkuu sifa nitampa.
 
Ukweli kwa hili suala anastahili pongezi. Amewapa meno na uwezo watu wa CAG kukagua kwa uwazi kila wizara na kuruhusu ripoti zao zisomwe na kujadiliwa bungeni kama ilivyokuwa kwenye kikao cha bunge lililopita. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Sifa zingine unapozitoa ni kama unamkejeli mtu.....Tumpongeze kwa kujionesha wazi wazi asivyo na uwezo wa kuwajibisha wasaidizi wake na kusoma alama za nyakati mapema.....Usalama wa Taifa wanafanya nini....TAKUKURU wanafanya nini....Ina maana hayuko makini kiasi ch kushindwa kuwafatlia wasidizi wake.....Yeye ndo M/Kiti baraza la mawaziri ayestahili kujua mambo yanavyoendeshwa na kuchukua hatua kabla hayajatufikia sisi wananchi wa kawaida....

Yeye nadhani hana muda wa kuwabana wasaidizi wake....Anahangaika muda wote kubadilisha ndege kwa safari za kujifunza somo la Jiografia ya Dunia......
 
Riz1 kapata wapi utajiri huu wa kutisha! Rachel wako wapi?
Sifa mbaya ataendelea kupata hadi rafiki zake wezi na wanawe watakapokamatwa na kufungwa. Kinachofanyika sasa hivi ni mdumange tu.
 
Back
Top Bottom