Kikwete anastahili sifa

zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,240
3,910
Baada ya Rais Kikwete kuunda upya mfumo wa ukaguzi wa mahesabu ya Serikali na baada ya kulazimisha ukaguzi huo uwe unafanywa kwa haraka zaidi, sio kama ilivyokuwa kwa uongozi wa kabla yake, na baada ya kufanya kila njia hesabu hizo ziwe zinajadiliwa kwa uwazi bungeni. Tunaona matunda yake.

Kikwete, unastahili kila sifa njema kwa kuwa mwenye kutoa na kufanya maamuzi kidemokrasia bila kuchukuwa hatua mkononi mwako (udikteta). Tunaona CAG ilivyofanya kazi, hakuna aliyetegemea kama itakuwa hivi.

Wapinzani, wameirukia hoja kama vile ni ubunifu wao, wanasahau kuwa wewe ndiye muasisi wa huu mfumo mpya na wewe ndiye uliyemteua Utoh.

Wanasahau pia kuwa wewe ndiye uliyeamuwa na kuanzisha mfumo wa hizi ripoti za mkaguzi mkuu zijadiliwe bungeni, hakuna aliyekuwa na moyo huo kabla yako. Mungu akuweke uendelee kuonesha njia.
 
kweli anastahili sifa kwa kuchagua mawaziri wabovu,wezi wajeuri walafi.!

Huo ni ufinyu wa kufikiri. Ni wewe ulianzisha mfumo huu ambao leo hii unaweza kuwajua wabadhirifu? funguka kidogo.

Mliibiwa awamu zote za kabla ya Kikwete bila kujijuwa, leo kawaonesha njia mbadala inabidi mumpe kila sifa. Mngeyajuwa haya?
 
Ukweli kwa hili suala anastahili pongezi. Amewapa meno na uwezo watu wa CAG kukagua kwa uwazi kila wizara na kuruhusu ripoti zao zisomwe na kujadiliwa bungeni kama ilivyokuwa kwenye kikao cha bunge lililopita. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Kawaida ya vipofu ni kusifia hata yasiyostahili kusifiwa! Huo ni wajibu wake, alafu umeona mahesabu ya Ikulu na ofisi ya waziri mkuu hayakuwekwa wazi; unafikiri hakuna wizi huko?
 
huo ni ufinyu wa kufikiri. Ni wewe ulianzisha mfumo huu ambao leo hii unaweza kuwajua wabadhirifu? Funguka kidogo.

Mliibiwa awamu zote za kabla ya kikwete bila kujijuwa, leo kawaonesha njia mbadala inabidi mumpe kila sifa. Mngeyajuwa haya?

inatusaidia nini kama anaweka mifumo lakini anashindwa kufanyia kazi matunda ya mifumo husika? Nyie ndio mnafurahia wingi wa shule bila kusikitikia wahitimu mbumbumbu... Kwa taarifa yako ni bure kuoga kwa nje wakati rohoni unajua u-mchafu. Apewe sifa kama anayoyaanzisha yanabadilisha maisha ya wanyonge na taifa linapiga hatua kimaendeleo, ni bora tuwe maskini kwa kukosa mifumo hiyo kuliko kuwa nayo angali tu mafukara
 
Kawaida ya vipofu ni kusifia hata yasiyostahili kusifiwa! Huo ni wajibu wake, alafu umeona mahesabu ya Ikulu na ofisi ya waziri mkuu hayakuwekwa wazi; unafikiri hakuna wizi huko?

Hayo uliyoyaona uliyaona kabla? Huko unapopataja kuna hesabu za usalama wa Taifa ambazo haziwekwi wazi hata kidogo, wacha kuwa mzembe wa kufikiri.
 
Kawaida ya vipofu ni kusifia hata yasiyostahili kusifiwa! Huo ni wajibu wake, alafu umeona mahesabu ya Ikulu na ofisi ya waziri mkuu hayakuwekwa wazi; unafikiri hakuna wizi huko?

Mkuu, penye ukweli uwongo hujitenga. Kikwete kawapa meno hawa jamaa wa CAG kukagua wizara yoyote bila woga wowote. Rejea hotuba yake ya ufunguzi wa jengo la CAG pale Morogoro. Naomba pia pitia ripoti ya CAG uone kama hakuna matumizi ya ofisi ya waziri mkuu na ikulu.
 
inatusaidia nini kama anaweka mifumo lakini anashindwa kufanyia kazi matunda ya mifumo husika? Nyie ndio mnafurahia wingi wa shule bila kusikitikia wahitimu mbumbumbu... Kwa taarifa yako ni bure kuoga kwa nje wakati rohoni unajua u-mchafu. Apewe sifa kama anayoyaanzisha yanabadilisha maisha ya wanyonge na taifa linapiga hatua kimaendeleo, ni bora tuwe maskini kwa kukosa mifumo hiyo kuliko kuwa nayo angali tu mafukara

Roho chafu ni zenu ambazo hamuoni mema ya Kikwete ambayo hayajawahi kutokea kabla yake. Uliwahi kusikia ripoti za mahesabu ya utawala wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa, yakijadiliwa bungeni?
 
Sifa zipi? Mbona Raisi wa malawi anaweza? Au na wewe ndio walewale wachumia tumbo?

Muone na huyu nae, watu wapo Tanzania wewe unatuletea habari za Malawi. Nenda basi kaishi Malawi, unangoja nini?
 
Ukweli ni kwamba jamaa ni msikivu.

Kabla ya kuwa mali ya umma report zile hupitiwa na waheshimiwa akiwemo Rais.

Kitendo cha kuridhia jamii ione madudu yale ni ishara ya kutaka kufanya mabadiliko.

JK Anatisha, kweli ni msikivu, tatizo taasisi za serikali kuna majambazi na kuzisafisha at one point ni issue.
 
Baada ya Rais Kikwete kuunda upya mfumo wa ukaguzi wa mahesabu ya Serikali na baada ya kulazimisha ukaguzi huo uwe unafanywa kwa haraka zaidi, sio kama ilivyokuwa kwa uongozi wa kabla yake, na baada ya kufanya kila njia hesabu hizo ziwe zinajadiliwa kwa uwazi bungeni. Tunaona matunda yake.

Kikwete, unastahili kila sifa njema kwa kuwa mwenye kutoa na kufanya maamuzi kidemokrasia bila kuchukuwa hatua mkononi mwako (udikteta). Tunaona CAG ilivyofanya kazi, hakuna aliyetegemea kama itakuwa hivi.

Wapinzani, wameirukia hoja kama vile ni ubunifu wao, wanasahau kuwa wewe ndiye muasisi wa huu mfumo mpya na wewe ndiye uliyemteua Utoh.

Wanasahau pia kuwa wewe ndiye uliyeamuwa na kuanzisha mfumo wa hizi ripoti za mkaguzi mkuu zijadiliwe bungeni, hakuna aliyekuwa na moyo huo kabla yako. Mungu akuweke uendelee kuonesha njia.
mkuu umemaliza kila kitu, ila tatizo ni sekretariet ya chama chetu imelala wanashindwa kutoa elimu ya umma ili watanzania waelewa ukweli halisi
 
Roho chafu ni zenu ambazo hamuoni mema ya Kikwete ambayo hayajawahi kutokea kabla yake. Uliwahi kusikia ripoti za mahesabu ya utawala wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa, yakijadiliwa bungeni?

tumsifie then...? acha upompompo wewe
 
Ili CAG awe na MENO anatakiwa awajibike kwa bunge na pia apewe nguvu ya kuwapeleka mahakamani watu wa namna hiyo. Yote haya ni mabadiliko kwenye sheria zetu but so far good move.
 
ningempa sifa kama walioiingiza nchi kwenye mikataba mibovu wangachukuliwa hatua....

Ningempa sifa kama waliotajwa kwenye ripoti wangechunguzwa na kuchukuliwa hatua....

Ningempa sifa mfumko wa bei ungethibitiwa na mchele kushuka toks sh 3000 hadi 1250

ningempa sifa kama bei ya petroli ingeshuka toka 2231 iliyopo sasa.....

Ningempa sifa kama wawekezaji kama yule wa monduli wangechukuliwa hatua....

Ningempa sifa kama madinu yetu yangetunufaisha wenyewe.....

Ningempa sifa kama waliouza Uda wangechukuliwa hatua......
 
Mkuu auditor sio polisi, akikuandikia taarifa anapaswa kukushauri ufanye nini, then weww ulioshauriwa uchukue hatua/ufanyue kazi ushauri wake, unaweza kumuita mahakamani kama shahidi tu....

Ili CAG awe na MENO anatakiwa awajibike kwa bunge na pia apewe nguvu ya kuwapeleka mahakamani watu wa namna hiyo. Yote haya ni mabadiliko kwenye sheria zetu but so far good move.
 
Baada ya Rais Kikwete kuunda upya mfumo wa ukaguzi wa mahesabu ya Serikali na baada ya kulazimisha ukaguzi huo uwe unafanywa kwa haraka zaidi, sio kama ilivyokuwa kwa uongozi wa kabla yake, na baada ya kufanya kila njia hesabu hizo ziwe zinajadiliwa kwa uwazi bungeni. Tunaona matunda yake.

Kikwete, unastahili kila sifa njema kwa kuwa mwenye kutoa na kufanya maamuzi kidemokrasia bila kuchukuwa hatua mkononi mwako (udikteta). Tunaona CAG ilivyofanya kazi, hakuna aliyetegemea kama itakuwa hivi.

Wapinzani, wameirukia hoja kama vile ni ubunifu wao, wanasahau kuwa wewe ndiye muasisi wa huu mfumo mpya na wewe ndiye uliyemteua Utoh.

Wanasahau pia kuwa wewe ndiye uliyeamuwa na kuanzisha mfumo wa hizi ripoti za mkaguzi mkuu zijadiliwe bungeni, hakuna aliyekuwa na moyo huo kabla yako. Mungu akuweke uendelee kuonesha njia.

Tatizo lake kubwa ni kutokuwepo nchini kujua kinachoendelea that means he is not on preventiion but on reaction
 
Back
Top Bottom