Kikwete ampokea Ikulu kijana aliyesafiri kutoka Geita kwa baiskeli kwenda kumpongeza!

Atampa msaada gani, wewe unadhani huyo anaweza kusema anataka msaada gani wa kumkomboa?Kama huyo mtoa msaada mwenyewe aliulizwa na Bush mna matatizo gani tuwasaidie...akasema tunasumbuliwa na malaria...so tuwasaidieje....akaomba vyandarua!!!!Kweli anaweza kumshauri na kutoa msaada wa maana? Anyway hivi kweli kila mtanzania mwenye shida akitaka kupata suluhu ya mtatizo yake aende kumpongeza ikulu? Je style ya baiskeli inaruhusiwa kutumiwa na wengine au kila mtu abuni style yake? Just ushauri, Jk wewe ni rais wa watu wa Tanzania hivyo, jukumu lako si kusaidia mtu mmoja mmoja, jukumu lako ni kufanikisha uundwaji wa sera za kukomboa watanzania wote na kuhakikisha utekelezaji wake unatimia. Kwaheri!
 
Mimi nitakwenda na punda....sijui nitapokelewa ila sitampongeza bali nitamuuliza kama kweli kashinda na kama anaweza kuapa mbele za Mungu...
 
Habari za Kuaminika ni kuwa Hapo Kasamwa ni Ngome ya Chadema, Hata Diwani wa pale kwa sasa ni Chadema hivyo wanajaribu kujipamba pamba ili watu wabadilike, Aaaah wapi. BeatKiLL...Piga Ua Kasamwa ni Chadema Tuuu.

Uelewa ndiyo Tatizo, hajui kama anajipa kilema cha Maisha na mwisho atakuja juta wenzake wakila Kuku kwa mirija. Wangapi tumewaona wametembea kwa miguu mikilometa kibao Eti kuasisi baadhi ya viongozi baada tuu ya kuhitimisha wanapongezwa kwa maneno then wanabaki wanaugulia.

:target:
 
anafaa sana kuuza mayai ya kuku kutoa kitunda kuyaingiza katikati ya jiji. Na hapa town hatoki ndo ameshafika hivyo.
 
Mtazamo wangu:

  1. Kijana alikuja Dar kwa shughuli zake, akakutana na wasanii wakampa dili maana sijaona hata kama amevaa nguo za CCM;
  2. JK nae hana kazi za kufanya kushughulikia wananchi wengi maskini wenye shida za kweli lakini ana muda wa kupiga magitaa, kufungua airtel (wezi wa kodi za wananchi) na kufotoa foto na mpanda baiskeli
  3. Hao waandishi wa habari na ma-edita wao wanaoipa hii habari kavaregi wana matatizo makubwa ya akili kwani tuna ya maana zaidi ya hiki kipicha cha huyo kijana na JK

Naamini kama media ingeipotezea hii habari, lingekua jambo jema kabisa
 
Kwa mtu mwenye akili hawezi kwamwe kutoka Geita hadi Dar kwa baiskeli kwa lengo la kumpongeza JK !!! Nasisitiza mwenye akili timamu. - Kwa TZ ya leo.
 
Wandugu,

Mmeisikia hiyo???? Kuna kijana amesafiri kwa baiskeli kutoka wilayani Geita hadi Ikulu Dar es Salaam kumpongeza mhe. jk kwa kushinda kwa mara nyingine kiti cha urais. ITV wamemwonyesha kijana akiwa anamkabidhi mhe. jk bahasha ya kaki ya A4 sijui ilikuwa na nini ndani yake!!! Vipi wakuu, inaingia akilini hiyo????

Chanzo cha Habari: Taarifa ya Habari ya Saa 2 Usiku.

How can we be sure he did come all they way from Geita?
Nadhani huyo katokea hapo Bagamoyo tu na sasa wanataka kutuaminisha kuwa katokea Geita,mbona hawaja tuonyesha alipokuwa anaanza safari yake na clip zingine alipokuwa njiani kuja Dar.
Mi vyombo vingine vya habari vinachosha kuviangalia maana habari zingine ni kuwapotezea wa TZ muda wao wakupunzika au kufanya shughuli muhimu.
 
Mie Kikwete sijawahi kumtia machoni, namuonaga kwenye picha tuu.

it need heart to do something like that, from Kigoma to..........

Huyu kanunuliwa tu.
 
i like this ...huyu jamaa ...katoka kitunda .......acheni utani mwana hivi mnajuwa geita,,,ni mbali....yaani ni unatoka geita...sengerema....unavuka mv misungwi..unaingia mwanza...unaitafuta shinyanga ...tabora...singida..dodoma.....moro...[msoga-chalinze]..pwani..dar....its more than 1,200 km....kati kati kuna mapori..wanyama wakali..majambazi..milima na mabonde......
kwanini alipoanza matembezi hatukuambiwa ili watu angalau ...wamuunge mkono huko mabarabarani...na safari hiyo haata iweje ni lazima itumie siku 40 hadi 60..just assuming kila siku alikuwa anatembea kilometa 20 hadi 30...assuming hakuugua au kupata uchomvu uliopitiliza....tuacheni usanii jamani..

Analysis yako nimeipenda sana. kwa kuzingatia analysis hii sasa nahitimisha kwamba HUU NI USANII MKUBWA.
 
:painkiller:Kwanza huyo jamaa ni mwongo, hakuna safari ya siku 7 toka Geita hadi mwanza!
Pili what is soo special?Angejua muda huo angetumia kwenda kuchoma mkaa na kuandaa shamba kwani mvua imewadia ili atimize kauli mbiu ya maisha duni kwa kila mtnzania!!
Wandugu,

Mmeisikia hiyo???? Kuna kijana amesafiri kwa baiskeli kutoka wilayani Geita hadi Ikulu Dar es Salaam kumpongeza mhe. jk kwa kushinda kwa mara nyingine kiti cha urais. ITV wamemwonyesha kijana akiwa anamkabidhi mhe. jk bahasha ya kaki ya A4 sijui ilikuwa na nini ndani yake!!! Vipi wakuu, inaingia akilini hiyo????

Chanzo cha Habari: Taarifa ya Habari ya Saa 2 Usiku.
 
The boy has got problem between his two ears; Badala angetumia huo muda na hizo nguvu constructive kupanda mahindi (Since mvua karibia zinaanza) kuliko ku - waste his energy, kama alitaka sana kumpokea angetuma sms..... Wastage of energy
Wewe umesema, sijui ni msukuma gani hyu, ktk hili siamini, ni familia ya nani itamruhusu afanye uzembe huo, sijui kama kuna ukweli, pengine kweli labda atakuwa ametokea kitunda tu, tena alikuja kuuza mayai akaona afanye usanii.
 
Nikisema waTanzania asilimia 75 ni wapumbavu mnanizonga!
Huyu kijana mzima na akili zake anaumia matak.o na kifua kwenda kkumpongeza JK!? mARA zote uvivu ni nyumba ya njaa!
Mimi ningekuwa rais ningeamuru achapwe bakora a kutosha kwa uzembe na UZURURAJI!
 
Tukio hili linanikumbusha mtu mmoja aliyekuwa anaitwa sipendi rajabu. Mwaka 1981 alitutembelea shuleni kwetu pale tanga akiwa na kabrasha kubwa lenye mihuri ya kila aina. Alichotuambia kilituacha na maswali mpaka leo:-

alisema yeye ni mzaliwa wa musoma, amekuwa akitembea kuunga mkono azimio la arusha. Makabrasha aliyokuwa nayo yalionyesha kwamba pamoja na kupita karibu mikoa yote nchini, pia alikuwa katembelea nchi jirani kama kenya na uganda.

Ukimuuliza analielewaje hilo azimio la arusha, alikuwa hana hoja yoyote ya msingi, zaidi ya kuamua kutembea kuliunga mkono!.......

Jamii haikosi vituko.
 
Back
Top Bottom