Kikwete amenitukana.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete amenitukana....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by VUTA-NKUVUTE, Nov 21, 2011.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Nasikitika kusema kwamba Rais wangu wa Tanzania amenitusi.Hii imetokea siku ya Ijumaa alipokuwa akihutubia Wazee wa Dar es Salaam.Alinitusi kwa kuniambia uongo huku akiwa anaujua ukweli.Aliniona mimi zuzu.

  Alidai kuwa eti mimi nanunua sukari kwa bei chee baada ya Serikali sikivu kushusha bei ya bidhaa hiyo.Ukweli ni kwamba kila uchwao,bei ya sukari inazidi kupaa.Niishipo mimi,kilo moja ni shilingi 2300.

  Je,matusi haya kwangu ni kwakuwa amepotoshwa na wasaidizi wake? Je,amewatukana pia na Wazee waliokuwa wakimsikiliza?

  Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
   
 2. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ndo mkome, na bado
   
 3. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  CCM oyeeeeeeeeeeeeeee, wananchi ziiiiiiiiiiiii
   
 4. A-town

  A-town JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Kigumu chama cga mapinduziiiiiii.........kigumuuu.......
   
 5. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Nilishasema na nitasema tena: maisha yakizidi ugumu Watanzania waoga wa mabadiliko na wavivu wa kufikiri wanaodanganywa miaka nenda rudi watatia akili!!
   
 6. KIHENGE

  KIHENGE JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 339
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  katutukana pia kwa kusema anayeishi nyumba za tembe ni kwa kupenda tuuu!
  wakati ukipita kwao msoga zipo kibao! JAMAA HATA HAFIKILIII (ZEZETE TUU!)
   
 7. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  .... :director: Mh ! Nyamurenge??
   
 8. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anakalilishwa jinsi ya kuongea hajui kitu.
   
 9. N

  NIPENDEMIMI Member

  #9
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Woga ni adui wa haki!
   
 10. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #10
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Wazee nao bana, si wangemuuliza imeshuka wapi?....inawezekana kuwa ni kweli imeshuka lakini Magogoni
   
 11. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #11
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kama bei ya sukari ni matusi, na yale ya David Cameron nayo utayaitaje? Au kwa sababu yametamkwa na Mzungu?
   
 12. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #12
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Yote matusi tu..
   
 13. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #13
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  JK anatumia udhaifu wa watanzania walio wengi, umbumbumbu! eti wanaambiwa hii nchi a.k.a kisiwa cha amani, eti uchumi wetu unakua, eti JK anasafiri nje kila uchao kututafuta wafadhili, eti tumefaulu kutokomeza malaria nk nk.
   
 14. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #14
  Nov 21, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Inabidi tunaofatilia hotuba za Kikwete tukuone wewe kama ulivyoandika mwenyewe hapo juu. Hii hapa ni hotuba ya Kikwete ilippongelea Sukari ni wapi umeyatowa hayo unayosema wewe? au ndi unanihii wenyewe huo?:

  Hali ya Uchumi
  Ndugu Wananchi;
  Katika kuelezea hali uchumi nchini, naomba nianze kwa kuelezea hali ya uchumi duniani kwani yanayotokea nchini yana uhusiano mkubwa na yanayotokea duniani. Hali ya uchumi duniani siyo shwari. Ukweli ni kwamba hali katika uchumi wa mataifa ya Marekani, Ulaya Magharibi na Japan haijatengemaa kufuatia machafuko ya masoko ya fedha na mdororo wa uchumi wa miaka miwili iliyopita. Hivi sasa uchumi wa mataifa tajiri ya Ulaya , wanachama wa Umoja wa Ulaya na hasa wanachama wa Umoja wa Sarafu ya Euro unapita katika kipindi kigumu na mashaka. Thamani ya sarafu hiyo inashuka na hata kuaminika kwake ni kwa mashaka. Mfumuko wa bei umepanda, ukosefu wa ajira umeongezeka na ipo hofu kubwa ya uchumi wa nchi hizo kudorora tena. Lakini nchi hizi ndiyo masoko makubwa ya bidhaa zetu, watalii na bidhaa za viwandani. Hivyo, athari zao zinatugusa na sisi. Kuongezeka kwa mfumuko wa bei kunaongeza bei ya bidhaa tunazonunua kutoka kwao. Aidha, kutetereka kwa uchumi wao nako kumepunguza masoko ya bidhaa zetu.
  Lakini kulegalega kwa sarafu ya Euro kumesaidia kuimarika kwa sarafu ya dola ambayo kabla ya hapo ilikuwa imepungua nguvu. Kwa sababu hiyo thamani ya sarafu ya dola imepanda duniani ikilinganishwa karibu na sarafu nyingine zote pamoja na yetu. Wakati huo huo bei ya mafuta imeendelea kupanda duniani kutoka dola 76.1 kwa pipa Septemba,, 2010 hadi dola 100.5 Septemba, 2011. Jumla ya yote haya ni kuongezeka kwa mfumuko wa bei kutoka asilimia 4.2 Oktoba, 2010 hadi asilimia 17.9 Oktoba, 2011.
  Ndugu Wananchi;
  Serikali na vyombo husika vimekuwa vinachukua hatua mbalimbali kukabiliana na matatizo ya kushuka kwa thamani ya shilingi, bei ya mafuta, bei ya sukari na matatizo ya umeme. Kuhusu kushuka kwa thamani ya shilingi Benki Kuu imeendelea kuchukua hatua zilizopo ndani ya mamlaka yake hususan kubana ulanguzi wa fedha za kigeni, kudhibiti matumizi ya fedha kigeni kufanyia malipo hapa nchini na kuongeza fedha za kigeni katika masoko ya fedha. Kwa kweli uwezo wao una ukomo. Jawabu la uhakika lipo kwenye uchumi wa mataifa makubwa kuchukua hatua thabiti kuimarisha uchumi wao ili thamani ya dola irejee mahali pake stahiki na bidhaa zetu zipate masoko ya uhakika na bei nzuri ili mapato yetu ya fedha za kigeni yaongezeke.
  Kwa upande wa mfumuko wa bei, ni vyema tukatambua kuwa Asilimia 75 ya ongezeko hili imetokana na kupanda kwa bei ya chakula na mafuta. Asilimia 25 iliyobaki imechangiwa na sera za fedha. Kwa upande wa mafuta, tunaamini utaratibu wa kuagiza mafuta kwa pamoja utasaidia kudhibiti bei za ndani za bidhaa hiyo. Aidha, itsaidia kupunguza makali ya athari ya bei za dunia zinazopanda. Kwa upande wa bei za vyakula, tatizo kubwa ni uhaba wa chakula katika nchi jirani unaosababisha wote kututegema sisi na hivyo kupandisha bei nchini. Tunaendelea kudhibiti magendo ya chakula na wakati huo kutengeneza taratibu rasmi za kuziuzia chakula nchi jirani.
  Kwa upande wa sukari tumeamua kuruhusu tani 120,000 ziagizwe ili kupunguza uhaba wa bidhaa hiyo na kushusha bei yake.


  Hatuko Peke Yetu

  Ndugu Wananchi;
  Ni vizuri tukafahamu kuwa, matatizo ya mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya fedha yetu siyo yetu peke yetu. Nchi zote za Afrika Mashariki zinakabiliana na matatizo haya. Kwa mfano, mfumuko wa bei kwetu ni asilimia 17.9, Kenya wako asilimia 18.9 na Uganda asilimia 30.5. Wakati mwaka wa jana sote tulikuwa kwa wastani karibu asilimia 5. Kwa upande wa kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola sote tumeathirika. Shilingi ya Tanzania imeshuka kwa asilimia 9.4, Kenya kwa asilimia 6.8 na Uganda kwa asilimia 17.4. Randi ya Afrika Kusini kwa asilimia 18.7, Rupia ya India kwa asilimia 9.8, Pauni ya Uingereza kwa asilimia 6.6. na Euro kwa asilimia 9.7.
   
 15. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #15
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [​IMG]hawa nao wamepanda bei sana hawa....kilo buku saba>!!!
   
 16. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #16
  Nov 21, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kwanini kilo moja ya sukari inauzwa 2300??
   
 17. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #17
  Nov 21, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145


  Sijui kama Kikwete anajua kuwa hapa alichemka
   
 18. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #18
  Nov 21, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  NDUGU WANANCHI ....(sina undugu nae kabisa)
   
 19. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #19
  Nov 21, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  wazee walishiba pilau!!!
   
 20. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #20
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160

  Ndio maana hawezi kuwaita ninyi vijana....tatizo watukutu sana halafu "mnajidai" mnajua sana hivyo mtabana kumuuliza

  Hivi ukiangalia vile vizee kuna hata mmoja ambae angeweza kuona na kuuliza hilo unaloliona na kuliuliza?

  Inabidi angalau mara moja ajitutumue (sijui kama ataweza, labda ataishia wale vijana wa "mashina" ambao wakishavaa kijani wanasahau kila kitu) atuite na sisi vijana hasa kwa kuzingatia kuwa under 35 wanatengeneza karibu zaidi ya 70 % ya population ya Tanzania....hili ndilo kundi la kuongea nalo
   
Loading...