Mkuu nchi sio kijiji. Na mazoea Hujenga tabia. Magufuli kachukua nchi yenye watumishi waliozoea kujitengenezea safari za ovyo kila kukicha semina na warsha nje ya nchi wenye kula mishahara ya watu kibao. Hivi hujasikia bado kuna waajiri hawajawasilisha taarifa za Wafanyakazi wao?
Watu hawaamini kuwa wanatakiwa wabadilike Na kuwa sasa mambo ya ovyo ovyo yaishe.
Wengine wanatamani hata kazi waache. Yote hii ni kudhibiti matumizi ya serikali. Serikali ikishamaliza hili kifuatacho ni kujua kwa usahihi inatumia kiasi gani wapi na wapi na kipi cha kufanya kuboresha maisha ya Watanzania.
Haya mambo yanaenda kisayansi na kimpangilio zaidi.
Jamani tafakarini na fikirieni kwa bidii.
Hivi mnafikiri magufuli anapeleka wapi kusikostahili hela zetu? Maana ughaibuni kutanua haendi
The problem ni kwamba, wakati wewe unazungumzia administrative issues mimi nazungumzia general economic situation! Tatizo lingine, wakati wewe unachukulia this's JK VS JPM issue, mimi nachukulia ni tatizo la kiserikali !!
Kwamba huyu anafuja na yule hafuji, isn't the topic of my interest... nataka result! Unaweza usifuje lakini ukawa na poor allocation of funds wakati watu wanataka kuona matokeo! Isitoshe, historia haishawishi vinginevyo!
Ingawaje sipuuzi jitihada za JPM lakini jitihada zake hazifai kuwa jitihada za mtu bali jitihada za mfumo! Zinahitajika kuwa ni jitihada za mfumo kv hii nchi imeoza tangia miongo kadhaa sasa ingawaje wengine wanataka kutuaminisha vinginevyo! Isitoshe, haya anayofanya JPM sio mapya katika siasa za Tanzania, kilichobadilika ni approach!
Kwa mfano, Mkapa alipoingia tu alitimua timua sana kule bandarini na TRA lakini alikuwa anafanya kimya kimya!! Hali kadhalika, kama ilivyo sasa, Mkapa pia alifunga ajira serikalini indefinitely! Huu ukaguzi wa wafanyakazi hewa, Mkapa aliufanya kwenye zabuni hewa! Ripoti ilipotolewa, ikaonekana by average, kwa mfano serikali walikuwa wananunua ndizi moja mbivu kwa Sh. 1500!!! Kwa utani, Mzee Mkapa akabatizwa jina na kuwa Mzee Ukapa; kumaanisha kwamba pesa iliota mbawa kwenye utawala wake kama inavyoongelewa hii leo!! Na natika kupigia msumari, akaunda kabisa Tume ya Jaji Warioba kuchunguza mianya ya rushwa!
Lakini hatimae ni serikali hiyo hiyo yenye mikakati yote hiyo ya kubana matumizi hadi kuitwa serikali ya Ukapa na kutuaminisha kwamba walikuwa wanapiga vita rushwa; ndiyo hiyo hiyo ilikuja kutuachia EPA, Radar Scandal, IPTL, Kagoda, Deep Green Finance na Meremeta!! Wakatumia mabilioni ya pesa kununua ndege ya Rais!! Mkapa administration ikauza kila kilichoonekana kinafaa kuuzwa! Ikauzwa hadi Container Terminal wakati ilikuwa ndo roho ya bandari! Zikauzwa hadi nyumba za serikali (Mheshimiwa nae ashasema atauza majengo ya serikali wakishahamia Dom...!!)!!
Mzee Mwinyi na yeye aliingia kwa mbwembwe za fagio la chuma likilenga kufagia uozo serikalini! Haya ya akina Hamisi Kigwangala kufunga mageti Muhimbili yalishatokea enzi za Mwinyi na Mrema wake... Bosi akichelewa kazini; toeni kiti chake!! Lakini serikali ya Mwinyi nayo ikageuka kuwa the worst government in history!
Kwahiyo badala ya kusema kinafanyika hiki au kile, watu tunataka results, PERIOD!! Tangible results! Msituambie kwamba makusanyo yameongezeka kwa vile tunaofuatilia haya mambo hilo nalo sio issue kv suala la kupanda mapato haalijaanza jana wala juzi!! Mzee Mwinyi aliacha mapato kwa mwezi ni less than 100 Billion, $1 = Sh. 550 hadi 600
- Mkapa aliacha makusanyo kwa mwezi kiasi cha 300-400 billion
- Kikwete aliacha around 900 Billion;
- Hivi sasa tunacheza kwenye 1.2 Trillion.
Tukija kwenye
Tanzania Official Exchange Rate nako,
- Mwinyi aliacha $1 = Sh. 574
- Mkapa kapokea dola moja ikiwa chini ya Sh. 600 na kaiacha ikiwa Sh.1200
- Kikwete kapokea $1 = Sh. 1,200 na kaiacha ikiwa Sh.2000 hadi 2,100
- Hivi sasa $1 = 2,200
Hivyo basi, hizi simulizi za hiki na kile kimeongezeka kwangu sio habari! Mwisho wa siku tunataka matokeo ya jumla manake hata kupanda kwa mapato nako tushazoea! Tunataka impact ya hayo mapato yaliyopanda! Inasemekana kuna Uwanja wa Ndege unataka kujengwa Chato... God forbid, naomba habari hii isiwe kweli! Lakini kama ni ya kweli basi wala sioni tofauti kati ya aliyekuwa anapanda ndege na genge lake kwenda Uropa na Amerika na yule anayejenga Uwanja wa Ndege sehemu ambayo economic feasibility haishawishi kufanya hivyo!