JPM nadhani bado hatumjui. Ana nia njema sana. Ila anaonekana kama vile anagawa raia wake kama walivyokuwa wanafanya wakoloni. Sijui ni kwa nini. Anapendelea jeshi la polisi, anapendelea ccm, anapendelea Chato yake akifanya safari nyingi huko na hata kutaka uwanja wa ndege huko, anagawa watu kwa ukanda eti kila mwanasiasa awe nyumbani kwake. Mtu kama Zitto hatakaa apate members mahali pengine. Pia inavyoonekana ni kama hapendi ushauri, anapenda utawala wa mtu moja, anashindwa kuishi na wapinzani katika serikali yake akisahau kuwa nchi ni ya vyamavingi, anapigana vizuri na mafisadi lakini inakuwa kama vile anachagua nani wa kumwondoa na nani wa kumwacha. Kiujanjaujanja bila haki. Isitoshe lugha yake siyo ya kiuongozi kwani mara nyingi husema maneno yanayopinga sheria ama sera za nchi kwa mfano kuhusu wapinzani, sera ya uzazi wa mpango, wamachingamatumizi ya jeshi la polisi kama vile kuwatenganisha polisi na wananchi kwa kutumia lugha kama vile "msiwachekee raia, hakuna polisi jamii", case ya wamachinga!!!!. Inaonekana kuwa nguvu nyingi ya serikali inatumika katika kupambana na watu wake badala ya kuwasaidia watu wake. Viongozi wamekuwa watawala wanadhani kuwa raia ama sehemu aliyoagizwa kuiongoza ni mali yake na raia hana usemi na anachotendewa na kiongozi wala yeye mwenyewe hana uamuzi wowote. Uongozi umekuwa unyapara badala ya maridhiano kama ivyotakiwa. Asili mia hamsini ya watu imeanza kuogopa na kudhani kuwa kuna matamko tu hakuna sera nzuri za kutufikisha huko. Kama ziko wananci hawazijui ni hiyo inaogopesha. Kwa mfano tunafikaje kwenye nchi ya viwanda. Nk. . Wengi tunauliza je kama mkuu anadhani siasa zinazuia kazi basi aagize zifanyike tu weekend. Na wote wafuate hasa yeye mwenyewe. Kwa hofu aliyonayo ya upinzani ni kama vile hakushinda kweli. Na tunajua alishinda. Kwa nini basi awe na woga huo ambao unaleta mashaka na unapoteza muda na raslimali ya taifa? Score. Bado muda wake lakini kwa sasa hivi hazidi 50%. Huenda akaongeza hapo baadaye. Ana mengi ya kusahihisha jamani. Tuwe tunamwambia ukweli kama yeye mwenyewe anavyowaambia watu ukweli. Hivi tutamsaidia na kujisaidia pia.