Kikwete alitumia uchawi gani?

Kikwete alitumia uchawi gani?

kikwete ana mapungufu kama binadamu lkn tulikula bata sana ktk utawala wake

hongera yako mim sijawahi kuona raha na bata hizo maana nilikuwa na pambana leke ysngu na sasa sijaona tofauti , hongera yako wew kwa kula bata za bwerere
 
Mkwere alinipotezea hamu ya kula ila sasa hivi Naboreka na kukereka kila kukicha kwa kauli za mkuu.
Kama Unasishi dar,matatizo haya ni yako mpaka miaka mitano au kumi ipite
1.Makonda,hawa wamekuwa hawaishi kutoa matamko na ahadi zisizotekelezeka
2.Mapoliccm haya ni magari ya kisasa yanajitahidi kutaka kuuzuia UKUTA ulojengwa na NYATI CEMENT chini ya MAINJIA WASOMI hali ya kuwa wao ni form 4 failures.
3.Siri ya MUtungi,huyu ni jaji lakini mtupu kabisa anapigana na vyama vya upunzani akiacha vyama vya siasa viwili tawala kuwa huru kuandamana yaani (POLICCM na UVCCM).
Mimi sio zitto kabwe,nitashiriki kuujenga na kuuimarisha UKUTA kama tamka litakavyonitaka hapo kesho.
#NikoTayariKwaUKUTA sep 1.
 
swali lako rahisi mno hata mtoto wa kindergaten analijibu kwa ufasaha.
Kikwete hakuandaa nguvu bali ajiandaa kiakili.
na Kikwete alitumia akili na sio Nguvu kama WASUKUMA wanavyofanya huko mashambani.
#NikoTayariKwaUKUTA sep 1.
 
Huwezi kuwalazimisha watu wote wakae ndani ya box la CCM as if hiyo ndiyo best practice na standard ya mwisho ya Watanzania.

Tatitzo lake hamna lolote wanabaki kudandia juu juu agenda za wapinzani bila kujua namna ya kuzitekeleza.

Nilitegemea mbele ya kusifia ujenzi wa shule, barbara na majumba ya kisasa, uongezee mzigo wa kodi kwa wafanyakazi, kiwango cha elimu Tanzania ambacho ndiyo mtaji wa taifa na vizazi vyake, uzungumzie ufisadi ulikithiri kuanzia Richmond, EPA, Escrow, Kagoda, meremeta, ujenzi wa bomba la gas, L, iptl nk.

Kisha uendelee kidogo hadi kwenye ongezeko la kutisha la deni la serikali lisilo maelezo, uangalie hujuma za mali asili zetu ikiwamo usafirishaji wa wanyama na mauaji ya tembo, hatua gani serikali ilichukua, thamani ya hujuma hizi ulinganishe na uwekezaji kwenye hiyo barabara na magorofa NSSF unayoyasema.

Mwisho utazame mauaji ya kisiasa ya kina Mwangosi, uovyo wa huduma za afya kitu ambacho ni cha msingi kuliko yote, habari za M'nyang, ulimboka, na wengine walioteswa kwa maslahi ya mtu mmoja, watanzania wanaoendelea kufa hadi leo kwa sababu ya ukosefu wa huduma za afya, uharamia na hujuma zilizofanywa juu ya katiba ya nchi uliolengesha kwenye kile kinachoendelea sasa, uchakachuaji wa kura na hitimisha uchaguzi wa zanzibar.

Yeyote mwenye akili timamu anajua kabisa yanayotokea leo hii, ni matokeo ya utawala wa huyo mkwere wenu asiyekuwa na maono wala mipango ya maana ya maendeleo ya taifa zaidi ya kulinda maslahi yake na ya familia yake.

Lawama zote zirudi kwa mkwere kwa sababu ndiye muasisi wa udikteta na utawala unaoendelezwa hapa Tz. Kila kitu aliasisi yeye na sasa anafurahia matunda ya mkono wake wa mgongoni.

Kama unataka kujifunza kaa kando waanchie Watanzania waongoze nchi kwa ufanisi bila kutumia nguvu ya majeshi kama mnavyofanya sasa.

TUMECHOKA NA CCM!
Acha chuki zako wewe hizo hazikusaidii kwa mstaafu elezea ukweli wa mambo na sio kumchukia tuu.
 
WANAFIKI WAKUBWA NYIE CHADEMA MIAKA YOTE MLIKUWA MKIMTUKANA JK MARA DHAIFU, MARA ANACHEKACHEKA, MARA HACHUKUI HATUA HALAFU LEO MNAMSIFIA DUUU!
 
Kumbe mnaikubali CCM inatekeleza Ilani zake tunashukuru kwa kutukumbusha kazi zilizofanywa na CCM
 
Kuna hali fulani hivi unayokumbana nayo.....mfano; ukijichafua nguo unahisi kila mtu anakuona, ukiwa katika kipindi cha harusi kila ukionacho unakitazama jinsi gani kitakufiti siku yako ya ndoa etc etc.....Usiwasemee wenzako, kwa hakika maisha yalikuwa mazuri/rahisi kwako kwangu mimi mfano mshahara wangu ulikuwa unanifikia tarehe 35 ya mwezi, sikuwa wahi pata perdiem ya serikali wala kupata urahisi wowote huku kila siku nikijiuliza hivi nikiwa na tatizo nani wakunisaidia? Nilishwahi gongewa gari makusudi na mtu kwa dharau akaniita ofisini kwake bila kujali kuna sheria....Sasa mm huyu ukiniuliza nitakwambia sasa najiona kama nimetoka shimoni.....And I presume kwa wale ambao walikuwawanasababisha matatizo yangu kwao hao leo hii hawawezi kuwa na furaha hata kidogo.

Ili kuwa objective na consistent jiulize walio wengi wapo kundi lipi? Lakwangu mimi au lako ukiwa na fact and figures then come back otherwise tuache hizi sweeping statements...
 
Hata magu akiondoka madarakani tutamsifia sana na kumponda atakaekuwa madarakani, Wa Tz ndio zetu hizo, siasa nyingii.
 
Acha chuki zako wewe hizo hazikusaidii kwa mstaafu elezea ukweli wa mambo na sio kumchukia tuu.

Kama huwezi kuchambua hoja unaongea kwa mihemuko achana na mimi. Sijadiliani na mapumbavu!
 
Yule hakuwa tayari kuhamia Dodoma na ndiyo maana nilisem vile. Yaani wewe rais halafu mawaziri wako ndiyo wakutawale wewe? Kwa Tanzania hii, tunahitaji rais anayendesha watu kiuhakika si kucheka na kusikiliza taarab tu Ikulu. Rais usipokuwa serious na maauzi yako your subordinates will never take you seriously, muulize kijana mtalii a.k.a. Mze wa kucheka bila sababu atakuambia.
huyo alikuwa mtalii lakini ametuachia UDOM, barabara za lami kila kona ya nchi, Kikwete heart institute, shule kila kata, freedom of expression and speech, umeme mpaka huku kwetu madongo kuinuka/kuinama, maji amesambaza kwa kiasi chake na mengine mengi pengine kuliko rais yeyote yule aliyewahi kuongoza nchi hii. He will always be my role model. na wewe kumkashifu kwako hapa nakuona kama mbwa tu.
 
Acheni nyie jk kakopa mpaka baas!Kama vipi Jpm naye aingie bank akope trilioni 30 kama alizokopa jk
 
JPM KESHA KOPA TRILION 10. KWA WACHINA KUJENGA RELI NDANI YA MIEZI KAZAA TU. JK TRILION 30 KWA MIAKA10
 
Wote tulilaumu ufisadi

Kodi zilikuwa hazilipwi?

Rais aliitwa dhaifu kwa kutokuwa mkali!

Wana ccm wakabadili gia Dodoma na kuhama!

Rais alikuwa anasafiri karibu kila mwezi

Lakini barabara zilijengwa, Vyuo vikuu na shule nchi nzima.

Majengo ya kisasa na upanuzi mkubwa wa miji wenye majengo ya kisasa kabisa!

Watumishi wa umma na wafanyabiashara walineemeka!

Na Rais wetu alikuwa full kutabasamu, urais kwake ilikuwa kitu kidogo kama ukiranja wa zamu tu!

Leo sasa!

Kila kitu kimerekebishwa, na rais hacheki cheki!

Lakini Mambo yamezidi kuwa magumu, na hata mwenyewe amesikika akisema anajutia uamuzi wake wa kukitaka kikombe hiki!

Je, ni wakati wa kurejea kupata semina elekezi toka kwa "mkwere"?

Au Mkuu apitie tu kisirisiri hadidu za rejea za serikali ya "mkwere" ili mambo yasiende mrama!


Umesahau kitu cha maana ambacho sikielewi, na Deni la taifa limeongezeka....
 
Uko obsessed na Mkwere!
Yeye sio mwanzilishi wa CCM, yet wote mnaimba na kuabudu jina la mwanzilishi wa CCM!
Yeye si aliyeanzisha azimio la Zanzibar lililofuta ujamaa!
Pia ufisadi ulianza labda hata kabla ya mkwere kumaliza shule, rejea issues za uhujumu uchumi enzi hizo za Mwalimu na hadithi za fagio la chuma za Mwinyi!
Serikali ya mkapa pia had a lot of scandals and possibly most of hizi cases zilikuwa ni muendelezo wa mambo yaliyotangulia!

Essence ya uandishi wangu sio kumsifu mkwere kuwa ndio raisi bora, na kubeza Magu na team yake! Ila ni ukweli kuwa uwezo wa kufikiri na kuplan kwa sasa haupo!
Tulipokuwa hatukusanyi kodi na kulinda rasilimali mali za nchi ndio mambo yalipaswa kuwa mabaya! Leo tumeongeza uwezo wa ndani, tu!epunguza wafanyakazi hewa na wanafunzi hewa, lkn hizo huduma za jamii kama afya, elimu ndio zimedorora maradufu!

States walizofikia che nkapa na mkwere hadi leo tumesharudi more than 5 steps back! Hii case chanjo inayozuka kama rumours kwa sasa ikiwa ni kweli utakuja kuwa balaa kubwa! Hizi cases za kipindupindu cha mwaka mmoja hakijawahi kutokea, outbreak ya nchi nzima kwa zaidi ya miezi 6!

Anyway nyie ndio mnaofanya watu wa awamu hii wasiwajibike!
Tuna tatizo leo, mnaamsha blames kwa tawala zilizopita!
Si tulishasema tunataka mabadiliko ya kweli?
Si tulijua kikwete katuangusha na sasa ndio wakati wa kampeni wote tuliamua kuhubiri mabadiliko!

So we knew exactly wapi kuna tatizo!
We had plans ambazo zilikuwa better than hizo za waliotangulia!
Now, huu ni wakati wa kuonesha ufundi na kuleta tija kwa mtanzania sio tena turudi kule kuliko tufelisha!
Mimi bado nina tofauti na mlio wengi, bado naamini mkwere alikuwa na vitu vya msingi sana katika kufanya mambo yaende! We need him, tukubali tukatae, time will tell!

We jamaa una akili sana. Pata sharubati ya Tende hapo ulipo malipo juu yangu.
 
Issue sio mkopo, unatumiaje ulichokopa!
Jifunze kupitia familia!
Wanaolisha wenzao ktk familia ndio pia wanadaiwa na mabenki na taasisi nyingine za kifedha! Hakuna mtu anayemdai maskini duniani, ila matajirii karibu wote wana madeni ikiwemo USA!
Fikiria tena juu ya deni la taifa!
Mbona Qatar na Brunei hawadaiwi salsa?
 
Sina la kusema sana. Nadhani Mrais wote kila moja wao ana mazuri na mabaya. Nyerere alikuwa mzalendo wa wote na kubana kidogo democrasia kwa wakati ule ilikuwa sahihi kwani nchi ilikuwa na wasomi wachache mno. Alijenga viwanda vingi muhimu. Alithibiti viongozi ila tulikosa bidhaa nyingi nchini. Nampa % . Naendelea
 
Mwinyi alikuwa mtu mzuri. Nyerere baada ya kuona wasomi wameongezeka aliruhusu kuwe na vyama vingi. Mwinyi alikuwa mzee wa ruksa. Uongozi wake ulikuwa wa wastani. Ile kuachia uhuru kidogo ilisaidia. Ila hakuweza kukusanya kodi na mwisho wa siku wafanyakazi karibu wakose mishahara ila viwanda viliendelea lakini uzalishaji ulishuka kiasi. Nampa 55%. Naendelea
 
Mkapa alikuwa kiongozi hodari. Alikusanya kodi nyingi. Shuguli za serikali pamoja na nidhamu kazini ilirudi. Lakini hakuingilia upinzani sawa kama Mwinyi. Alikuwa mkali. Safi kama kiongozi. Ila wakati wake ufisadi wa hali ya juu ulianza kama vile EPA. Viwanda vikauzwa na havikuendelezwa. Mpaka leo anajutia hilo. Nyumba za serikali aliuza kwa upendeleo mkubwa na hasara kwa uma. Benki ya TZ iliuzwa bei chee pamoja na majengo yote ya benki kwa hasara na baada ya hapo ndiyo ikawa mwisho wa benki hiyo. Wakubwa walijichukulia mali pia hata yeye mwenyewe. Nampa 50%.
 
Back
Top Bottom