Invisible
Robot
- Feb 11, 2006
- 9,075
- 7,878
Taarifa tulizopata punde ni kuwa Rais Kikwete na ujumbe wa CHADEMA wamekutana Ikulu muda si mrefu, Slaa ni mmoja wa waliohudhuria. Inasemekana ni mwendelezo wa maongezi ya mjadala wa Katiba.
Picha:
Wakiwasili:
Ndani:
JK akaja:
Wakiondoka Ikulu:
WanaJF,
Nawashukuru wote wanaofuatilia thread hii. Nawaomba kwa mara nyingine muwe na amani. Nawahakikishia hakuna wala hakutakuwa na usaliti. Chadema iko makini sana. Tunasukumwa na uzalendo na nia njema kwa Taifa letu.
Aidha kama alivyosema MMJ, tumekuwa tukisukuma mabadiliko makubwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kabla Rais hajateua Tume ya kukusanya maoni. Tulieleza wazi kuwa vinginevyo hatutashiriki mchakato wa kukusanya maoni.
Ni dhahiri busara ya kawaida inataka tupate progress ya majadiliano hayo hayo na utekelezaji wake. Katiba nzuri ndio afya na uhai wa Taifa hata kama si ufunguo wa matatizo yote yanayotusibu leo. Wakati mwafaka utakapofika tutatoa Taarifa kwa umma.
Msiwe na hofu mtuamini.
Picha:
Wakiwasili:
Ndani:
JK akaja:
Wakiondoka Ikulu: