Infact ni mara ya nne toka aanze rasmi mbio za urais. awali ilikuwa ni ile ya 2005, then zimewahi kutokea mbili hapa katika katika.
Ni vema sasa tuambie Rais wetu anaumwa nini? Ansbert Ngurumo aliwahi kuandika:
Rais wetu si dhaifu kama wananchi wake ambao wengi wanalalala au kushinda njaa; wanapata mlo mara moja moja (na wenyewe haujakamilika virutubisho); wanafanya kazi nzito na ngumu zinazokula nguvu ya mwili na akili; wana pato duni sana (chini ya shilingi 1000 kwa siku); wanakabiliwa na magonjwa hatari na hawana huduma ya matibabu inayoeleweka na inayoaminika; wanaishi katika mazingira hatari; wanakabiliwa na magonjwa sugu kwa miaka mingi; wanatembea kwa miguu au baiskeli, bajaji au wanasafiri kwa malori na mabasi mabovu; hata kwa wanaosafiri kwa ndege, wanatumia madaraja ya chini yanayochosha; wanalala kwa saa 2 au tatu kila siku; wanasumbuliwa na umaskini wa kutisha kiasi kwamba kila wanapolala hawana tumaini kama wataiona kesho.
Watanzania hawa hawazimii, hawaishiwi nguvu wala hawaanguki, aanguke rais mwenye afya isiyotetereka (kama tulivyoelezwa) na mwenye matunzo ya viwango vya juu?.."
Sasa iweje huyu? Kijua ndio hichi ni vyema Rais akate shauri sasa. kwani kwa hali yoyote, lazima mgombea binafsi ndo aongoze kampeni kwa nguvu zaidi..... na pengine wabunge waliopita bila kupingwa. ile confidence ya kusimama na kuikimbiza kura kwa hali ha hila lazima ipungue...
Ni faida kwa wengine walio katika mbio? historia itatuambia....