GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

Mtu B,

Je hawa watu wako huwa wanawaonea huruma hawa watu?




Hizo picha mbili ni athari za mgodi wa dhahabu Mara ambazo aliyeweka sahihi anafahamika. Watu wanaumia na wao wanapeta tu na mashingi yao ya bei mbaya. Halafu huyu kama ni mama au mdogo wako/mwanao, unategemea kuwa utajisikia huruma?

Angelikuwa anachakalika kuokoa watu kama hao juu, amini amini nakuambia, hata Dr.Slaa asingelikuwa maarufu na sanasana wangelikuwa wote serikali na huku akimfanya Dr. Slaa kuwa PM wake na siyo huyo Mamvi aliyekuja kukomba hela bila hata kunawa. Hapo hatujamzungumzia Mkono na Rostam Azziz ambao hao ndiyo kabisaaaa.........
 
Ha ha ha hii forum na Kikwete ni kama pete na kidole.

Picha zimekwenda wapi tena?
 
ai jamani nyie ...........angekuwa baba yenu nyie mngefurahi anadishwe kila kona alivyoanguka na alivyobebwa kama maiti?

Angekuwa baba yangu ambaye anaacha wanawake wajawazito wanarundikwa kwenye wodi za wazazi wakati yeye anazunguka dunia kutalii kwa mabilioni ya shilingi, nisingemwonea haya hata kidogo. Tena ningekuwa mtu wa kwanza kabisa kuhakikisha kuwa baba yangu anakaa mbali sana na uongozi wa nchi au hata kuweka jela kabisa.
 
kuanguka kwa kikwete hakuna na mahusiano na imani.

Inategemea unaongelea imani ipi mkuu .... kuna imani za kishirikina (hasa kwa yule msemaji mkuu wa washirikina wote wanaosaidia kampeni ya Kikwete ----- Ya haya who sane --- shehe yahaya)
 

Vilikuja ghafla!
 
Mkuu ukizitaka sema ninazo kwenye makataba yangu! Naona leo wale jamaa zetu wapo wengi sana

ohh I see,

Mzee wangu Masa....... hawa jamaa jinsi wanavyojiaibisha hadi inachekesha.

Yaani Raisi wa nchi anaanguka,

Mijamaa yote inakimbia kumbeba mzobe mzobe bila hata kutumia machela au kitu chochote maalumu. Bila kujali kama kuanguka kwake kumetokana na ukosefu wa hewa au la, minjemba yote inajazana na kumeza oxygen yote.

Badala ya kukaa na kujadili namna ya kufanya vyema next time (trust me, there will be a next time on this guy), yenyewe inakuja hapa kupumua kijuu kama imeishiwa hewa.

Zitunze tu mkuu maana kuna siku zitatumika kwa ufanisi zaidi.
 
swaumu ilikuwa kali zaidi alipoanguka mwanza..............
 
sheikh yahya kafanya kazi yake sawasawa ya kuwa mshirikina....................
 

Jamaa hata gloves hawajavaa hawajui operational risk? Mfano muungwana kama anamagojwa ya kuambukiza si wote wale ilikuwa wanaathirika? Jamaa kuna siku ataanguka akiwa kwenye mkutano wa UN na jamaa watamfix huko apatiwe tiba
 
hata sijui niseme vipi ieleweke... si mara ya kwanza wala ya pili kwa mheshimwa kuanguka, na tena kuna uwezekano ikatokea tena... kuna gharama gani kwanza kwake yeye mwenyewe kukubali kuachia majukumu haya mazito ila apate kheri ya kuishi na familia yake?!!! na kama itabidi kulazimishwa kuachia madaraka baada ya uchaguzi (hypothetically), je hii nchi ina uwezo wa kugharimia uchaguzi mwingine?

kwani hii nchi haina washauri na watu wenye mapenzi mema nayo ambao huyu mheshimiwa anaweza kuwasikiliza ili tuondokane na uongo uliokithiri?!!!!

kweli inanitia hasira tuuuuuuuuuuuu.... kwani sababu zoooooote zinatolewa haziingii akilini.... labda nimeerevuka sana hivyo sidanganyiki au ni mpumbavu saaaana hivyo sielewi maana.
 
Ha ha ha hii forum na Kikwete ni kama pete na kidole.

Picha zimekwenda wapi tena?

Mkuu hata mimi najiuliza sana tena sana. Kwa nini picha za hii thread ni mobile kiasi hiki. Yaani huwezi kuwa na hakika na picha utakazozikuta kila unapofungua.

Nadhani Mod aweke mambo vizuri tu kuwa hizo picha za KJ alipokuwa anaanguka hazitakiwa hapa JF. Naona yanakaribia kuwa kama mambo ya Swaziland ambapo jamaa alitupwa jela kwa kukutwa na gazeti linaloongelea kisa cha mke wa King Mswazi kufumaniwa. Mhhh. hata siamini.
 

Ndio JF mpya hiyo mkuu .... mambo yamebadilika sana hapa
 
Ngoja tusubiri, labda mod atatujibu. But kama ni hivyo basi ....life is never the same as it used to be!!

I will bet you a pack of bud light kuwa hii thread itafungwa muda si mrefu. Au ili wasionekane wanafiki, wataihamishia kwenye lile jukwaa la ushushushu (ikapotelee huko kabisaaaa)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…