Kweli nimetazama anavyoanguka kwenye hii video imeniuma sana na imenisikitisha. Katika hali ya ubinadamu, inasikitisha sana kuona binadamu mwenzio akizimika vile. Halafu alipoanza kusema 'aise' kabla hajaanguka, nadhani alikuwa anajisikia vibaya sana au maumivu lakini akajikaza aendelee na hotuba. Nimeumia pia jinsi sauti ilivyoanza kufifia kama anayetaka kutafuna ulimi, yaani kama ni ndugu yako yuko katika hali hiyo utatishika sana.
Kama kuna wanaofurahia kitendo cha binadamu mwenzao kuteseka vile mbele ya watu, hao ni makatili tu. Hakuna siasa hapa. Siasa ni kupingana kwa hoja na si kutakiana mabaya. Mimi napinga CCM kwa dhati, lakini nimesononeshwa sana na madhila yaliyompata JK pale jukwaani. Kama binadamu mwenye umri sawa na babangu, nimemtazama anavyoanguka kwa masikitiko makubwa, ikanijia picha kama babangu mzazi akianguka vile mbele ya umati, itakuwaje. Nimeumia sana.
Pole sana mheshimiwa, Mungu akujalie afya njema uwe salama, urudi kwenye mpambano. Tunahitaji mpambano baina ya watu walio wazima wa afya ndio maana napenda upone, tupate nafasi ya kukusikia katika kampeni, ujibu hoja zetu ukiwa mzima tufanye uchaguzi tukiwa tumesikia hoja za wagombea wote.
Mods, mbona ile picha ambayo mkulu kabebwa mmeiondoa? Can you give us details? Kumetolewa shinikizo nini?
Mods, mbona ile picha ambayo mkulu kabebwa mmeiondoa? Can you give us details? Kumetolewa shinikizo nini?
Ushauri wangu kwa wanajukwaa wote, ukiweka mbali siasa za vyama sisi sote tu watanzania. Linapotokea jambo lisilo la furaha na tulipokee hivyo kama Watanzania, la Furaha nalo tulipokee kama Watanzania. Jambo la kuanguka Raisi wa Nchi si jambo dogo, linaweza hata kuathiri bei za Hisa za Makampuni yalijaindikisha DSE. Tucheke pale panapostahili kucheka, panapohitaji pole na tuseme pole, ushabiki mwingine haujengi!!!
Wildcard acha kuongopea watu mchana mchanaRais wetu keshaamka. Nawasifu JF. Hakuna chombo kingine cha habari kilichothubutu kuweka picha ya aina ile hapa Tanzania.
Wildcard acha kuongopea watu mchana mchana
Video mbona bado zipo na watu tumezicopy kwa kumbukumbu kuwa kuna siku rais wetu alidondoka jukwaani, angalia post no.1.watanzania na unafiki ndiyo maana hatuna maendeleo sasa hii video ina kitu gani cha ajabu mpaka watu wengine wanaitoa kulinda heshima sijui nini upumbavu nothing graphic at all
Hiv hapa jamvini hakuna wataalamu wa afya watueleze ukweli? Sio siri tena, afya ya JK sio nzuri na haijaanza leo, ni tatizo alilonalo muda mrefu na analifahamu.
Muuguzi mmoja alinifahamisha kuwa hizo huwa ni dalili za kifafa, kwamba humtokea mtu anapokuwa excited. Kwa mazingira ya sasa ya JK niwazi yuko excited. Zaidi ya hapo amejiongezea strees, kutoka zile za kuwemo safarini kila siku hadi zinazotokana na msimamo hasi wa wafanyakazi dhidi yake baada ya kutoa matamshi yenye kashfa na sasa ndio anatambua madhara yake kwa safari yake kurudi Magogoni. Ujio wa Dr Slaa kwenye kinyang'anyiro cha Urais ni jambo ambalo hakulitegemea, alitegemea mteremko ule ule kutoka kwa kina Lipumba, ghafla anaingia mpambanaji wa kweli, imemuongezea stress.
Jambo la msingi hapa ni Watanzania, hususani CCM kuachana na unafiki, kuingalia afya ya mgombea wao katika uhalisia wake badala ya kulionea aibu
Ukiangalia hiyo picha utagundua kwamba mke wa JK halii bali anasononeka wakati majirani zake wanalia. Hivi hiyo inaashiria nini????
Kwenye picha hiyo Mama Saima hayupo au ana mwingine?Ukiangalia hiyo picha utagundua kwamba mke wa JK halii bali anasononeka wakati majirani zake wanalia. Hivi hiyo inaashiria nini????