GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

Inawezekana raisi hamsikilizi daktari wake ! na daktari naye hajaamua kujiudhuru kwasababu decision algorithm yake haijafika mwisho...

Mkuu .... usiweke "dh" kwenye hili neno ...... ole wako Kiranga akusome...lol
 
Ushauri wangu kwa wanajukwaa wote, ukiweka mbali siasa za vyama sisi sote tu watanzania. Linapotokea jambo lisilo la furaha na tulipokee hivyo kama Watanzania, la Furaha nalo tulipokee kama Watanzania. Jambo la kuanguka Raisi wa Nchi si jambo dogo, linaweza hata kuathiri bei za Hisa za Makampuni yalijaindikisha DSE. Tucheke pale panapostahili kucheka, panapohitaji pole na tuseme pole, ushabiki mwingine haujengi!!!
 

Hakuna la safari na wala baba yake safari: JK ni mgonjwa tu period. Kwani alipoanguka mwanza alikuwa amefunga???? Hivi kwa nini tusijiulize vipi daktari wake alipotoa riport alimtetea sana kuhusu afya yake. Sasa mbona leo mpaka sasa yuko kimya.... Watatunga sababu kibao lakini Mungu atawaumbua tu....!!! Waache walete mchezo tu siku ataanguka asiamke. Ndo wonder yeye mwenyewe anakwenda kupima akili USA, labda alifikiri ataambiwa yeye ni kipanga wa TZ..............!!!!
 
Mbona yeye huwa anacheka cheka tunapomwambia vitu serious kuwa maliasili zinakwisha lazima equilibrium iwepo, angekuwa rais serious na anaonekana kuwa na uchungu na wananchi wake na mali ya taifa sidhani kama kungekuwa na komenti unazoziona leo.
 

Mkuu huwa tunajisahau sana kuwa hakuna Rais wa Tanzania bara!
 

Hizo hisa na zianguke tu! Kama ni mgonjwa na hataki kuwapisha wenye afya wasimame kugombea kumbe tusemeje? Kura hapati period!:mad2:
 
Guys lets be honesty on this issue...i ve never ever heard President fall down on stage in this world!!!Ni Tz tu nimeona,hivi kweli mtu kama Obama au David Cameroon usikie kaangua jukwaani sijui maelezo yangekua kama ya kwetu ya kujikanyaga!
I think we need to be more serious with president health..waseme ukweli kuna nini????
 
Form seven in taabu kwel kwel

hahaaaa eti yuko mwanza na jana kaonekana kapanda ndege saa 6 dakika 48 machana amekwenda nje kutibiwa..hahaaaa kumbe swaumu na glucose kushuka inatibiwaga ulaya.....
 

....ndio itaathiri bei ya hisa ...positivelly ....bei zitapanda....ikiwa na maana kuwa hata hiyo investors community haina confidence na kikwete......ukiniambia rais kama Obama akianguka bei zitashuka nitakubali.....au hata uganda na rwanda ....lakini sidhani kama kikwete wetu ana uwezo hata chembe..wa ku influence bei za hisa ..tusimvishe kofia isiyomkaa[who the cap fits ,let him weir it!!].......sana sana kikwete ana influence bei za bidhaa kupanda madukani....yaani hao wenye viwanda kila siku wanatupandishia bei za vyakula........kwa kuwa hawana uhakika na JK!!
 
....rudia hii habari ,hawajakusikia...

Kweli Mkuu, hii habari inahitaji kuongezewa nyama kidogo ili kitu kitoke mchicha. Vinginevyo utamu wake unapotea.

Hata hivyo, tukilinganisha JK na watu kama Mgabe, Kibaki na wengine wengi tu, nani alitegemewa kudondoka hadharani? Ni aibu kwa mkuu wetu wa nchi kuzimika zimika kama mshumaa halafu watu wanatuletea vijisababu vya kiswahili swahili. Inabidi tupewe maelezo ya kina kwa sababu Rais ni mtumishi wetu na tunalipa kodi ili aweze kutufanyia kazi. Jamani kuna mtu anaweza kuvumilia mfanyakazi wake ambaye afya ni mgogoro wakati kazi anayotakiwa kufanya ni ngumu sana?
 
ameanguka akisema..."tupeni ridhaa yenu, tutafanya zaidi..."
kudanganya umati wa masikini, mchana kweupe tena ukiwatazama machoni kuna ongeza stress na presha...
 
mungu amuweke hai ili ashuhudie kushindwa kwake na Dr. Slaa october
 

Kuna tofauti bana! JK kaanguka kwa kukosa fahamu, lakini Slaa alianguka wakati akiogea sabuni ya bamia!
 

Jamani kusema ukweli ndo ustaarabu! au ustaarabu ni kunyenyekea upumbavu?
 
jamani hii video hapana..................imenibidi nimuonee huruma tu! sijamuonea huruma kama rais au ccm, ila kama mtu mzima, baba wa watoto, mwanamme, unaanguka kwa ugonjwa mbele ya watu, unabebwa kama mfu, kisha dunia nzima imekuona!

mmmh
 
Kweli nimetazama anavyoanguka kwenye hii video imeniuma sana na imenisikitisha. Katika hali ya ubinadamu, inasikitisha sana kuona binadamu mwenzio akizimika vile. Halafu alipoanza kusema 'aise' kabla hajaanguka, nadhani alikuwa anajisikia vibaya sana au maumivu lakini akajikaza aendelee na hotuba. Nimeumia pia jinsi sauti ilivyoanza kufifia kama anayetaka kutafuna ulimi, yaani kama ni ndugu yako yuko katika hali hiyo utatishika sana.

Kama kuna wanaofurahia kitendo cha binadamu mwenzao kuteseka vile mbele ya watu, hao ni makatili tu. Hakuna siasa hapa. Siasa ni kupingana kwa hoja na si kutakiana mabaya. Mimi napinga CCM kwa dhati, lakini nimesononeshwa sana na madhila yaliyompata JK pale jukwaani. Kama binadamu mwenye umri sawa na babangu, nimemtazama anavyoanguka kwa masikitiko makubwa, ikanijia picha kama babangu mzazi akianguka vile mbele ya umati, itakuwaje. Nimeumia sana.

Pole sana mheshimiwa, Mungu akujalie afya njema uwe salama, urudi kwenye mpambano. Tunahitaji mpambano baina ya watu walio wazima wa afya ndio maana napenda upone, tupate nafasi ya kukusikia katika kampeni, ujibu hoja zetu ukiwa mzima tufanye uchaguzi tukiwa tumesikia hoja za wagombea wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…