Kikuu vs AliExpress

Mkuu nakubaliana na wewe Alliexpress wako vizuri binafsi nimekuwa nikiwatumia kuagiza vitu kadhaa toka mwaka japo sina sanduku la posta nilikuwa naandika tu sehem nilipo ,mizigo ikifika napigiwa simu na wahudumu wa posta naenda kuchukua mzigo.Lakin hivi karibuni nimekuja kuhisi inawezekana kuna matapeli pia kwa sababu kuna mzigo niliagiza,yule seller akaniomba nimtumie Address nikamwambia atumie ile iliyopo kwenye profile yangu tukakubaliana,kweli mzigo nikitrack ulikuwa unaonyesha umekuwa shipped ,Mara baadaye naona inaonyesha umerudi nikawauliza vipi ,wakaniambia sijui transporter wao kasema Address haijakamilika mzigo hauwezi fika ,wakati mizigo niliyoagiza kwa wakati mmoja japo seller tofauti kwa anuani ile ile ilifika kwa wakati.Nikamtumia anuani ya Sanduku la posta kabsa la rafiki yangu mpaka Leo kimya toka August. Halafu nikiangalia kule kwa ktrack inaonekana delivery successfully, Wale jamaa na hisi wamenipiga maana Hela hazijarudi .Nimesitisha kuagiza mizigo mpaka nifungue sanduku la barua kabsa.
 
Duh pole ndugu na ulishajaribu kuwa kazia kuhusu refund wakagoma
 
Sijachunguza saana maana nimeanza kuagiza juzi tu hapa ngoja nifatilie ntakupa majibu
Changamoto ni kwamba kupitia app yao sikuona mahali ambapo naweza contacts na Alliexpress moja kwa moja.
Kama unafahamu tusaidiane itafaa hata kwa siku nyingine
 
Sawa kaka
- Fika posta iliyokaribu nawe, utapewa maelekzo ya nini na nini kinahitajika.
- Utapewa fomu na kujaza.
- Utalipia kiasi kidogo utakachoambiwa kulipia.

Then kila mwaka utakuwa unalipia ili uendelee kumiliki hilo sanduku lako la posta.
 
Changamoto ni kwamba kupitia app yao sikuona mahali ambapo naweza contacts na Alliexpress moja kwa moja.
Kama unafahamu tusaidiane itafaa hata kwa siku nyingine
Kama ni mawasiliano na Aliexpress Ukifungua App nenda Account then shuka chini kabisa utaona option ya Help Center.


Kama ni mawasiliano na Seller katika kila bidhaa ipo option ya Contact Seller.
 
Kumbe hata AliExpress waajabu mzigo asaivi umemaliZa siku 19 na haujafika mzigo wenyewe sio kusema wa hela ndogo Dola 20 naa
 
Hapa nimepokea memory zangu za GB 16 zote mbili na flash Toshiba 2 gb 32 na smart watch na simu dogee x50 saaafi Ali express is the best na huo juu ni ujumbe Wa Posta kukutaarifu ukachukue mzigo wako. Mzigo inafika fresh japo sometimes inachelewa.
Chini kabisa lens ya camera ipo njian na jins unavyofatilia mzigo wako.
 

Attachments

  • Screenshot_2019-12-19-23-24-19.png
    68.1 KB · Views: 15
  • IMG_20191119_163626.jpg
    150.3 KB · Views: 16
  • ae_1576655069102.jpg
    16.3 KB · Views: 16
  • Screenshot_2019-12-19-23-33-38.png
    18.2 KB · Views: 15
  • Screenshot_2019-12-19-23-33-21.png
    16.9 KB · Views: 12
  • IMG_20191119_163655.jpg
    108.7 KB · Views: 11
  • IMG_20191202_122553.jpg
    123.7 KB · Views: 14
Ouk sawa kamanda ngoja tuwe wavumilivu tu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kumbe Bora kikuu katika swala la kuwahi,maaana kipindi naagizia kupitia kikuu haijawahi zidi siku 20 mzigo umenifikia ndugu


Sent using Jamii Forums mobile app

huwezifananisha Kikuu na Aliexpress hata siku moja (kuanzia wingi wa bidhaa, unafuu wa bidhaa, usalama wa wallet, refunding policies ) , rejea comment #8 au post za Mwl RCT ndio utaelewa vizuri

na kuhusu kuwahi au kuchelewa hakuna iliyo bora kuliko mwenzake , unless uwe unatumia njia za express ( dhl, fedex, tnt, usps)
 
Duh,ok swaibaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu nimekwama,
Unalipiaje kwa mpesa Mastercard?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…