Kikundi cha Watekaji Je, Ndiyo Hawa Hapa?.

Kikundi cha Watekaji Je, Ndiyo Hawa Hapa?.

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
15,265
Reaction score
25,539
Niliwahi kusoma sehemu fulani na baadaye nikaambiwa kwa comment hili jambo.

Habari ya jumapili ndugu Mtanzani.

Hili jambo la wasiojulikana limezungumzwa sana kwenye majukwaa mbalimbali na hata JF.

Nimejiuliza mara kadhaa na sijapata jibu kwa hili swali langu, je hawa watekaji ni sehemu ya wananchi wa Tanzania?.

Hawa watekaji ni kikundi kutoka idara gani hapa nchini?.

Naweza kupata jibu au nisipate je ndicho kile kikundi kisichoingiliwa na taasisi au mhimili wowote wa nchi yetu?.

Kwamba bunge lilipitisha azimio kuwa na kikundi maalum ambacho kinaweza kufanya jambo lolote na asiwepo wa kuhoji?.

Maswali ni mengi ila bado kidogo jibu lipatikane.

Bunge halina meno kuhoji wale wanao wapigia kura kutekwa, kuumizwa na kuuawa?

Je, mbunge (mhimili) wangu hana mamlaka niliyomkanidhi kulingana na katiba ya nchi kuhoji watendaji wa serikali inayokuja mtaani kunikamua kodi kwamba mbona mlipa kodi fulani kapotea au kaumizwa na hakuna majibu ya maana?.

Ina maana hicho kikundi kilipewa nguvu kufanya haya au kimeingia mkenge kwa wanasiasa na kasahau target yao ilikuwa ni wavamizi wa nchi yetu?.

PK perspective!.
 
Onyo kali kwa wananchi!.

20250511_104459.jpg

°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°
UPDATE;
May 24.2025
Alichoongea askofu wa ufufuo na uzima.

Mara baada ya bandiko hili takribani wiki mbili alichoongea huyo mbunge wa kawe ndicho sehemu ya hiki nilichoandika hapo.

Hiki kikundi kipo kipo ndani ya idara gani na nani anakipa nguvu?

Majibu kayatoa askofu/mbuge wa kawe J. Gwajima.
 
Kuanza kushutumu watu hatuwezi kupata suluhu ya tatizo ,ni bora kutulia na kushirikiana na tuliowapa madaraka ili kujua ila panic watu wataendelea kuishi ..Hili suala sio la jana wala leo.
 
Kuanza kushutumu watu hatuwezi kupata suluhu ya tatizo ,ni bora kutulia na kushirikiana na tuliowapa madaraka ili kujua ila panic watu wataendelea kuishi ..Hili suala sio la jana wala leo.
Kama bado unawaamini Polisi basi una matatizo ya akili.

Wameshindwa kuwakamata walomchukua mzee Kibao mchana kweupe kweny bus waje kuweza ya Mdude alochukuliwa usiku??

Polisi ndo watuhumiwa wa kwanza kabisa. Tatizo wanatuona sisi hatuna akili qmmk zao.
 
Kuanza kushutumu watu hatuwezi kupata suluhu ya tatizo ,ni bora kutulia na kushirikiana na tuliowapa madaraka ili kujua ila panic watu wataendelea kuishi ..Hili suala sio la jana wala leo.
shida washapoteza uhalali
 
Kama bado unawaamini Polisi basi una matatizo ya akili.

Wameshindwa kuwakamata walomchukua mzee Kibao mchana kweupe kweny bus waje kuweza ya Mdude alochukuliwa usiku??

Polisi ndo watuhumiwa wa kwanza kabisa. Tatizo wanatuona sisi hatuna akili qmmk zao.
Inawezekana ila utekaji umeanza leo ,Sativa alitekwa mpaka Tajiri wa nchi ...Mbona hawatoa ushirikiano hao waliotekwa .
 
Tuwe kitu kimoja hasa sisi wananchi.
hii nakuunga mkono asilimia 100 mkuu --- na jambo hili ndo bado halijatimia.

ndo maana unaona wengi tupo tu tunasubiri CDM wafanye maajabu, TEC wakitoa tamko kali tunafurahia, BAKWATA wakitoa tamko kali tunafurahia, hivi karibuni tunafurahia BUNGE LA ULAYA pamoja na tetesi la SENETI YA MAREKANI.

hii yote ni dalili kwamba hatutaki kuhusika --- this is my analysis
 
Kama bado unawaamini Polisi basi una matatizo ya akili.

Wameshindwa kuwakamata walomchukua mzee Kibao mchana kweupe kweny bus waje kuweza ya Mdude alochukuliwa usiku??

Polisi ndo watuhumiwa wa kwanza kabisa. Tatizo wanatuona sisi hatuna akili qmmk zao.
Sifa moja wapo ya IGP Wambura hata akaapanda ngazi ni KUUA
 
Inawezekana ila utekaji umeanza leo ,Sativa alitekwa mpaka Tajiri wa nchi ...Mbona hawatoa ushirikiano hao waliotekwa .
Sativa hatoi ushirikiano?

Si kila siku anamtaja Mafwele kule X na mpk sasa kila mtu anamfaham Mafwele.

Sativa amehojiwa mara kibao tang akiwa hospitar kule Katavi, Aga Khan na mpk leo anamtaja aliyemteka.

Polisi wamefanya nn mpk sasa??
 
Haya mambo mnayepeleka kisiasa siku moja utanielewa. ukifuta mambo ya siasa watu watakuwa kitu kimoja.
 
Back
Top Bottom