Ikiwa leo tunakamilisha siku 21 za maombolezo ya kifo cha Dkt Magufuli,naomba kaa kimya kwa sekunde kumi kumkumbuka na kumuombea makazi salama huko aliko.
Ahsante,Nianze ka kumpongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mama yetu ,Samia Suluhu kwa hotuba mzuri,hotuba iliyobeba matumaini kwa Watanzani.
Hotuba ya leo hakika imejaa faraja na imani kubwa kwa watanzani kwamba huyu mama atatufikisha nchi ya ahadi.
Katika Quraan sura ya 104(Surat Hummazah) aya ya kwanza ,Allah amewaonya walamba Visogo/Wasengenyaji "Backbiters".
Kifo cha Rais magufuli kimenifunza mambo mengi .Mosi Dunia ni mapito,tujitahidi kufanya mema kwa aiili ya baadae
Pili ,nimebaini Rais Magufuli alizungukwa na walamba visogo ,Watu ambao akiwa nao walikuwa wanamchekea akitoka wanamng'ong'a.
Hata Siku 21 za maombolezo hazijakamlika watu hao tyr wametanua makucha yao.
JPM alizungukwa na wasaidizi wanafiki.Makamu wa Rais ni mshauri namba moja wa Rais,kama Rais alisema jambo na ww ukachekelea ukaona linafaa leo hii hayupo unasema halifai ,ww tukuelewe vp?, Ni kama ulikuwa unasubir anguko lake ili umvue nguo hadharani.
Wakati mama anazungumzia miradi,kuna mahali alisema kuna miradi mingine ipo kwenye makaratasi sijui itawezekana ila nataka niione.Hivi alikuwa na maana gani?.
Afu akasema kuna Issue alikuwa anasolve baadae ikamshinda nguvu akaachana nayo.
Any way,naochotaka kusema hapa,Binadamu huwezi kupatia kila kitu,Yale ambayo Rais Magu aliteleza ni vema kuyarekebisha kwa hekima ukiangalia mzee hajatoka madarakani kwa kustaafu bali ni kifo.
Staili aliyoanza nayo ya kumponda mtangulizi wake na walikuwa wakifanya kazi pamoja itamletea shida.
RIP JPM
"Jamhuri ya muungano wa Tanzania,Kazi iendelee"
Usichokijua tu ni kwamba huyu Mama kavumilia mengi sana ( yaliyo nyuma ya Pazia ) aliyokuwa akifanyiwa na Aliyelala mazima sasa.
Kwa Kilichofanywa Kwake hadi Familia yake haraka sana ikamkimbiza nje Kumuokoa leo hii Mama wa Watu angekuwa ameshamtangulia Yeye ila Mwenyezi Mungu alimuhitaji zaidi ili leo hii aje Kuturejeshea Tabasamu na Amani ya Rohoni.
Wadanganyeni hapa Wanafiki na Wapuuzi wenzenu just ya Mazuri ya aliyelala Wenu Milele ila kwa Sisi wengine tuliokuwa tunazipata zile za ndani tena kutoka Jikoni tumempongeza tu Israeli kwa kufanya Kazi yake mapema na kwa Ustadi wa Kipekee.
Zisingekuwa Busara za Hayati Mzee Mkapa na Mzee Makini Rais Mstaafu Kikwete Mama wa Watu angeshatangaza kutoka hapo Kitambo sana tu.
Halafu msitutibue na Sisi wengine tukaomba kuundwe Tume Huru Kuchunguza Kifo cha Rais Mstaafu Mzee Mkapa ambaye mara kwa mara alionya Wanasiasa kusema neno 'Tanzania yangu' na Kujiona ni miungu Watu huku akisisitiza juu ya Ukomo wa Urais kuwa ni kwa Awamu mbil tu.
Na mkizidi Kutukera zaidi sasa tutaanza taratibu Kugusia uliokuwa Mpango wa SIRI wa Kuwanyamazisha ( Kipumzi ) Wastaafu akina Mzee Mangula, Msekwa, Kikwete na Butiku kwakuwa walionekana kuwa Kikwazo katika nia ya Mtu Kuitawala Milele Tanzania kama Mali yake binafsi.
Isingekuwa tu Miti Shamba ya Kihehe pamoja na Mila zao leo hii Mzee wa Watu Mangula pengine angekuwa Historia ndiyo maana tunaoipenda ile CCM ya Nyerere ( Generalist nikiwa Mmoja wao ) nikimwona Mzee wa Watu yupo Hai hivi huwa nafurahi na Kufarijika mno.
Kwahiyo mlitaka Mama Samia ( Mheshimiwa Rais ) abakie na Uozo uliokuwepo? Halafu ungekuwa tu na Akili ( IQ Kubwa ) usingeshangaa kwanini kila Rais ajaye hupenda kuja na Team ( Safu ) yake kwani hili ni Jambo la Kawaida sana Politically and Administratively ili kuwa na Ustawi na Utawala ( Uongozi ) wako.
Mwacheni Mama wa Watu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan atuongoze na kama ni Kumpima tutampima ifikapo mwaka 2025 ila kwa dalili zake hizi nzuri alizoanza nazo na Kutuonyesha Watanzania tuna Imani nae na huenda akaja kuwa Rais mzuri kuwahi kutokea nchini Tanzania na tukamsahau Kimoja huyo aliyekuwa Intarahamwe Wenu nyie Wanafiki Wenzake wakiongozwa na Wewe Mwandamizi wao hapa.
Endeleeni tu Kutukera ili sasa akina Generalist tuanze Kufunguka sababu Kuu ya Mtu kutopenda Kukaa Ikulu ya Magogoni Feri Dar es Salaam na Kupenda kuishi Ikulu ya Dodoma au kule Kwao alikotaka Kukufanya ni White House ya Marekani.
Kuhamishia Serikali nzima Mkoani Dodoma wala haikuwa Mpango wake na tena hakupenda ila katika Kuwazuga Wanafiki na Wapuuzi Wenzake kama Wewe akajifanya anatimiza Ndoto za Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere wakati ukweli ni kwamba kuna Misingi ya Kiutamaduni ya Marais wote wa Tanzania hutakiwa kuifanya Wakishaapishwa ila Yeye akaleta Kiburi chake na Jeuri zake hadi akapaona hapamfai.
Rais sasa ni Mama Samia tu msitukere!!!