Hivi Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kilimsibu Nini Hadi akaachana na fikra za kumuenzi JPM?

Weakman

JF-Expert Member
Jul 23, 2021
861
1,384
Salamu zenu nyote!

Mtakubaliana na Mimi kuwa Rais wetu alipoapishwa kuendeleza kijiti Cha Urais, alipania kuendeleza Yale aliyoyafanya JPM.
Kwanza, alitoa kauli iliyoashiria ukuu wa mamlaka kwa kuweka wazi hatopenda kuchezewa na mtu, Kama ambavyo Magufuli hakupenda!
"Anayesimama hapa ndio Raisi katika umbo la kike!"

Akaweka kauli mbiu iliyoweka wazi kuwa Mambo yaliyofanywa na Magufuli yanaendelezwa!
"Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kazi uendelee!"

Akaweka msisitizo wa wakuu wa mikoa, na wilaya kutatua kero, na akiona bango la wananchi kwenye ziara zake, mhusika atatumbuliwa immediately!
Of course hiyo Ni hulka ya Magufuli.

Tukumbuke pia, Lile katazo la mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa liliendelezwa kwenye kipindi chake, hio kuonesha wazi Mama yetu aliutamani Sana umagufuli

Kuna walamba asali wengi walitamani miradi ya JPM iachwe, but naona mama amekaza!
Kuna walamba asali walitamani, viongozi wote wa Magufuli waondolewe serikalini, Kama Waziri mkuu, na wengineo, but mama amekaza!
Na huenda hata Mbowe, kwenye vikao vyake na mama, alipendekeza waondolewe viongozi wote wa Serikali waliotekeleza maagizo ya JPM ya kuwabana Chadema!

Mama amewahi kukiri kuwa viatu vya JPM vimempwaya!
Kauli hii inathibitisha matamanio yake ya kupita njia za Magufuli, Ila tu ameshindwa kufanya hivyo!

Mama Ni mfuasi Halisi wa Magufuli!
Kuna pahala hapakumuendea vizuri
Wajuzi tufahamishane yaliyomsibu huyu Rais wetu mpendwa, kipenzi Cha utawala wa mpendwa wetu Dr. John Pombe Maguli!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mambo gani ya Magufuli aliyoyaacha? Hembu yataje angalau matatu ili uzi wako uweze kujadilika.
 
Taja hizo fikra alizoachana nazo
 
Fikra za late shujaa wa Africa legend JPM haziwezi bebwa na weak minded people. Hawa wapiga dili wajanja wajanja wana flourish kwenye mazingira kama haya ya sasa. Ujanja mwingi mbele giza.
 
Fikra zipi?
 
Madam President ni mtu smart, ameendeleza yale yaliyo ya msingi na tija kwa Taifa, yale ya kipuuzi na kidikteta kaachana nayo maana hayana afya kwa Taifa.
 
Hakuna kitu kama miradi ya mtu, bali ni utekelezaji wa miradi iliyoainishwa katika ilani ya uchaguzi. Huwezi kuuita miradi inayosimamiwa na serikali kuwa ni ya kiongozi fulani, bali inatekelezwa na kusimamiwa na utawala mmoja kwenda mwingine katika kipindi husika.

Huwezi kuuita mradi wa ujenzi wa TAZARA kuwa ni wa Mwl. Nyerere, ama mradi wa ujenzi wa daraja la Umoja ama Uwanja wa Taifa kuwa ni ya Mkapa, ama mingine mingi iliyotekelezwa wakati wa vipindi vya utawala wa Mwinyi na Kikwete kuwa ni yao.
 
Yeye Magufuli kilimsibu nini mpaka akaanza kuwabeza Watangulizi wake?
 
Back
Top Bottom