Kikao cha NEC ya CCM yampongeza Mh. Edward Lowassa, mjini Dodoma

Kikao cha NEC ya CCM yampongeza Mh. Edward Lowassa, mjini Dodoma

Umenena vyema mkuu.......kuna watu wanahoji eti utajiri katoa wapi akawajibu kuwa kila shillingi aliyokuwa anapata lazima atenge senti kadhaa kwa ajili ya kufanya kabiashara na kununua ngom'be ila wenzake wakipata shillingi wanamaliza kwenye starehe na kuwa na wanawake wengi, na watoto wengi sasa kwa nini usiyumbe kifedha....leo hii hakuna utajiri mkubwa kama wa ngom'be, ngo'mbe moja wa wastani anakwenda mpaka laki saba au nane sasa ukiwa nao 600 tu kwa hakika wewe ni millionea tayari.....ila hilo kundi dogo ndani ya ccm wamebaki majungu majungu na fitina muda woteeeee

Unaona akili hio mkuu? Leo hii vijanandio wamemgundua Robert Kiwasaki wa Rich Dad Poor Dad na the Four Quadrant ndio wanamshupalia wakati tuna mtu alikua aki practice philosophy hizo toka enzi za Nyerere ambako kila mtu ilikua fikra za mwenyekiti zi dumu, lakini the man was a Capitalist! Anaeielewa hela na namna ya kuitengeneza, na ndio mtu tunamuhitaji kuongoza Taifa letu. Mwenye uelewa wa investments, market characteristics e.t.c. we nee a succesful business man ambae anajua ni mkataba gani utatuleta faida na upi tunapigwa, tunahitaji mtu anae amini uAfrika wetu na kuamini akili zetu na uwezo wetu sisi waAfrica na kwamba kujikomboa kunatokana na sisi wenyewe sio kwa kuomba misaada ya wazungu na hadi kudiriki kusema hatuwezi wekeza kwenye vitu vikubwa kama gesi na madini ila sisi tufungue viwanda vya pipi, sasa Mungu katupatia hizo rasilimali za nini kama hatuwezi kuzimiliki, tuziache basi hapo chini mpaka tuweze ila sio kuwapa wa nje.
Nina imani kwa wooote waliopo CCM, Lowassa ndio anaweza! Na zaidi anavyopigwa vita na ------ ndio ninaongeza nguvu ya kumpenda. Serikali ya ------ imefuja sana mali ya umma, imeiba kupitiliza hivyo basi yeyote ------ atakaempinga ndie anatefaa sababu atakua against hao waliofuja mali zetu.
Lowassa sio malaika, bali ni mwenye chongo kati ya vipofu CCM. Najua kuna kitu kikubwa huyu mtu anataka kufanya sababu hela alizo nazo na umri aliofikia ingekua mtu asie na nia ya dhati ya kumkomboa mtanzania, angekua mbinafsi basi angepumzika zake ale bata ya kufa mtu kokote kule duniani, lakini upendo wake kwa nchi yake ndio unamsukuma kutaka kuiongoza ili nasi tuwe watu katika watu dunia hii!
 
Mungu atakaemchagua Lowasa Lazima atakua anakula na kwenda chooni...ama atakua anakunya kinyesi kigumu au kuharisha

We unamdhihaki Mungu. Naomba uwache hayo mambo ya kijinga. Mungu hadhihakiwi, ukimdhihaki Mungu urakuja kuzama kama titanic.
 
Wewe unaumwa dhambi ya ubaguzi ya ukabila.

Unanichumia dhambi kwani kikwete na lowasa nyerere si aliwapiga chini wakati wanaitwa BOYS 11 MEN? Akampendekeza Mkapa? Au huijui siasa ya tanganyika? Husiwe na akili kama ya TBC.
 
Unanichumia dhambi kwani kikwete na lowasa nyerere si aliwapiga chini wakati wanaitwa BOYS 11 MEN? Akampendekeza Mkapa? Au huijui siasa ya tanganyika? Husiwe na akili kama ya TBC.

Je mkapa aliweza kukidhi matakwa ya Mwalimu?. Ni kwamba wengi mna mtizamo hasi dhidi ya Kikwete, ni vizuri mkafahamu kuwa Kikwete kafanya mengi sana ndani ya utawala wake. Kwa sababu hamumpendi hamuwezi pia kuona mazuri yake. Na hata ukiambiwa hauwezi-kuelewa kwa sababu, akili yako imechukuwa mrengo wakutokuelewa tena kwa makusudi.
 
Ni kweli kabisa kwa ufisadi ,Lowasa ni kiongozi wa kipekee

Mtapiga kelele sana na ufisadi huu wa Lowassa ambao ni wakusadikika. Lowassa siyo mbadhirifu wa mapato yake. Nyie wengine mkipata fedha mnatumbua tu. Rejea neno la kwenye biblia la talanta wazipewa watu wale. Waliozalisha maradufu walizidishiwa. Wewe endelea kupiga domo.
 
Nape aliuponda sana huu mradi.atakuwa anaona aibu sana aisee!

ata mimi nmeshangaa kwa lowasa kusifiwa. kama alisifiwa basi alipakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.

Nimuhuni sana uyu bwana. Keshafanya yake hapo .

Sina imani naye kabisa. na ngoja #MIZENGO amkaushe kwanza ndo ajue hatutaki wafanyabiashara Ikulu.
 
lakini hiyo asilimia 25 ni hela refu ambayo wasingeweza binafsi kuwekeza. hiyo matokeo ya uamuzi ngumu ya laigwenan.

Kwa taarifa yako huyo anayeitwa mwekezaji si mwekezaji kitu kwa sababu hata mkopo alioupata kuwekeza kwenye jengo hilo alitumia hati za viwanja husika mali ya UVCCM,akenda mbali zaidi kwa kuingia mkataba unaomtambua yeye na kizazi chake kuendelea kula 75% milele.
Huo mkataba wa kifisadi ndio ulikuwa umuondoe Nape CCM baada yakushutukia dili hiyo ya Lowasa Nchimbi Makamba na mafisadi papa wengine bila Kikwete kuingilia kati hatima ya Nape ilikuwa mashakani.
 
labda kama kuna mwenye taarifa atuwekee terms na nani na nani walihusika na hii project. Kwenye hii maamuzi ngumu ya laigwenan...baadhi ya watu wanaona hivi. kama una land lakini huna mtaji huwezi kufanya kitu. ila unaweza kufanya joint na mwenye pesa na ukapata mgao kutegemeana na utakavyonegotiate..
 
Kikao Cha Jana Cha NEC{halmashauri Kuu Ya CCM -Taifa} Pamoja Na Mambo Mengine Kilitoa Pongezi Maalum Kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Ngoyai Lowassa Kwa Kubuni Na Kusimamia Ujenzi Wa Jengo kubwa La Kitega Uchumi kwa ajili ya Umoja Wa Vijana{UVCCM}

Hili jengo si ndilo lilimfarakanisha Lowassa na Nnape au?
 
Mtapiga kelele sana na ufisadi huu wa Lowassa ambao ni wakusadikika. Lowassa siyo mbadhirifu wa mapato yake. Nyie wengine mkipata fedha mnatumbua tu. Rejea neno la kwenye biblia la talanta wazipewa watu wale. Waliozalisha maradufu walizidishiwa. Wewe endelea kupiga domo.

Kwa hiyo unataka niseme Lowasa ni mwadilifu? Huo ujinga ubaki nao wewe.
Mimi niko upande wa Nyerere,rudisha kumbukumbu nyumba uone Nyerere alisema nini kuhusu huyu fisadi wakati anataka kugombea urais 1995.
 
Back
Top Bottom