Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

Haa haa kumbe rushwa sio agenda tena ya makamanda jamaa kapewa ten billion kavuta faaaasta hapo bado hawajafika ikulu haya ndo tunawaita watetezi wa wanyonge aiseee bora nibaki kuwa muumin wa dini sio siasa!!kwaheri mzee wa safari ya rushwa!!

Hivo 10 billion kapewa kwenye gunia au zimehamishiwa kwenye account yake!?
 
Nimetumiwa hizi muda huu... Ndo imekua hivi au ni macho yangu. Sijaelewa bado
 
Its Photoshop hata ukiangalia mood za watu hapo.
Angalia mkono wa kulia wa EL na uzoom.
Dr Slaa kavaa nguo tofauti ktk picha mbili.
Pure Photoshop.
 
Lowassa akihudhuria kikao Kamati kuu CHADEMA
attachment.php

attachment.php

Siasa ni timing tu hapa CDM wamecheza kama pelle cjui kwa jirani wa kijani kama kura zitatosha sijui
 
tatzo mnafanya mzaha hebu leten mambo sereouz bhana
 
Lowassa: "Siwezi kuhama CCM, ambaye anaona hafai ahame yeye"

Mbowe: "Lowassa ni fisadi na yuko katika list of shame".

Slaa: "Hatupokei makapi ya CCM"

Leo hii they all have same mindset!?


Hahaha...Tanzania nchi yangu nakupenda sana, ila ukombozi wako bado sana!
Pole sana mkuu wangu nilikuwa nakusoma unapinga sana hizi habari.
 
japo nilisikia hizi tetesi kwa muda mrefu ila nimepata mshtuko kuona hizi picha.

Sikujua tuna wanasiasa muflisi namna hii, kumbe Tanzania hakuna upinzani bali wasaka tonge.

Hakika <b>A WEEK IS VERY LONG IN POLITICS <b/>
 
Tumkaribishe Lowasa lakini asipewe nafasi ya kupeperusha bendera ya UKAWA. Awe kama kina Mzee Mtei. Na asaidie kuongoza mapambano ya kuimaliza Ccm. Naogopa hawa wanaotoka Ccm wasije kuwa kama kina Shibuda wakatuharibia Chama. Pia kuna walio tumikia chama kwa uaminifu wakitegemea kugombe nafasi kwenye uchaguzi huu. Sasa wakikoseshwa nafasi zao zikichukuliwa na hawa wageni kutakuwa na kuvunjika moyo kwa hilo kundi. Ni mawazo yangu binafsi.
 
Ninachoshangaa waliokuwa wakipinga mpk mapovu yanatamalaki kwamba Mzee Sio fisadi Leo mapovu yanatamalaki kuwa Mzee ni fisadi
 
Sio photoshop hiyo bana,,,,


Lakini ukweli ni kwamba kama tunahitaji kumtoa ccm madarakani hatuna budi kuhakikisha tunampokea lowasa na kundi lake ili tushinde kirahisi.
 
kama kweli nimefurahi sababu chadema wamekula matapishi na wamejiua kisiasa
 
Kama akiwa ccm alikuwa fisadi basi hata akienda #CHADEMA bado atakuwa fisadi ntasema ukweli daima Lowasa hafai kuwa raisi wa tanzania Tetty
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom