Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

uchaguzi uwe huru na haki, wananchi tutaamua wenyewe, hayo majina sio ishu, ishu ni kura
 
Makamanda wametweta, Baregu kajiinamia kaficha uso asipigwe picha, Slaa kaduwaa, kwa ujumla makamanda wote hawana sura ya furaha hata chembe, jembe ni jembe limetia timu.

Kimsingi propaganda ni nyingi sana wakati huu.Hizi picha zimeungwa.Sakafu alipo Baregu na hiyo alipo Msigwa na picha ya Lowasa ni tofauti.Pili bega la kulia la Salimu Mwalimu limekatwa vilevile bega la Lowassa limekatwa kudhihirisha kipande cha picha ya Lowasa kimeingizwa.
 
Wakati anafanya yote hayo huyu Lowasa alikuwa chama gani? 🏊
 
Too strange in my all living life,
anyway , ktk siasa hakuna rfk wala adui wa kudumu, maslah kwanza.
 
Kimsingi propaganda ni nyingi sana wakati huu.Hizi picha zimeungwa.Sakafu alipo Baregu na hiyo alipo Msigwa na picha ya Lowasa ni tofauti.Pili bega la kulia la Salimu Mwalimu limekatwa vilevile bega la Lowassa limekatwa kudhihirisha kipande cha picha ya Lowasa kimeingizwa.

Wacha kujifanya mtaalam wa picha we makengeza
 
Nimepokea ujumbe kupitia whatsapp ukisema sasa Lowassa rasmi chadema na baadae kuingia ukawa kama mgombea urais. Hii kwa upande wangu itakuwa ni historia ya aina yake na suala la kampeni litakuwa gumzo kubwa. Nazidi kujiuliza je; ccm watakuwa tayari kuona kada wao anawatesa na kumwacha aogeleee tu? Je; ikitokea amepata urais kina Nape, Makonda na wenzake waliomsema vibaya wataishi nchini au ughaibuni?

Hivi kundi lake la 4U Movement nalo litafanya kama lilivyofanya wakati wa kutafuta wadhamini? Je; kitatokea nini iwapo Lowassa hatashinda akiwa na ukawa?

MUNGU ibariki Tanzania
 
Lowassa karibu sana na waitee na wengine waambie bado nafasi wanayo ya kutubu na kuwatumikia watanzania kwa upendo, huna mpango na urais lakini Monduli Ubunge kama kawaida kupitia CHADEMA .

Wataisoma namba CCM huu mwaka.
 
Nakumbuka vizuri Askofu Mkuu Zakaria kakobe aliandika walaka mzito juu ya kusambaratika kwa Chama changu cha Ccm, kuna kila dalili kwamba unabii umetimia ccm iko mahututi soon itakufa karibu Rais Lowasa tuendeleze safari ya matumaini. binafsi sitakufuata chadema lakini nitakupa kura yangu. maana tuliowengi tulikuonea huruma kwa njinsi ulivyo pokonywa haki yako ya kuchanguliwa.

Tusidhalau watumishi wa Mungu yuko wapi ngeleja ???
 
Umekuwa ukivuga CCM unaifahamu sana kuliko wana CCM tunaotumia usafiri wa baiskeli kuinadi CCM vijijini bila hata maji wala malipo yoyote. Leo nataka nikuhabarishe kuwa kitendo walichofanya Kitengo kwa msukomo wa Nape,Riz,JK pamoja na Membe pasipo kumwacha Mkapa kimetufanya tuifahamu vizuri CCM kuwa si chama cha wanachama isipokuwa ni chama cha viongozi wachache wasiozidi hata 10. Nimefarijika sana kwa maamuzi haya magumu aliyochukua chaguo la Watanzania Lowassa.
 
Fisadi lowasa leo mnashangilia chadema haaahaaa haa mangi kula pesa
 
Juzi niliandika hapa kuwa EL atagombea kwa tiketi ya Chadema na mwenza ni yule makamu wa CUF visiwani. Mkanipinga saaaana mpaka uzi ukaondolewa.
Pingeni tena nami nitawataja mawaziri sita wa serikali ijayo.
 
Patashika nguo kuchanika....sasa siasa za Tanzania zitabadilika bwana...hizi zama siyo za chama kushika hatamu..........
 
Juzi niliandika hapa kuwa EL atagombea kwa tiketi ya Chadema na mwenza ni yule makamu wa CUF visiwani. Mkanipinga saaaana mpaka uzi ukaondolewa.
Pingeni tena nami nitawataja mawaziri sita wa serikali ijayo.
Duh! Ina maana tayari wamegawana vyeo?
 
Back
Top Bottom