Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,748
- 134,500
- Thread starter
-
- #141
.Kwa mazingira yaliyopo ndani ya CCM hivi sasa, kweli mtu ambaye ana nia ya dhati ya kuleta mabadiliko anaweza kwenda kugombea kupitia CCM?
Mama Simba tayari ameishasema ndani ya CCM hakuna aliye msafi, kwa hiyo hata yeye mwenyewe ni mchafu na JK nae ni mchafu. Kauli hiyo ina maana kubwa sana kwa wale wenye nia ya kuingia kwenye siasa.
Mabadiliko ya kweli hayataletwa na hii CCM ya JK, EL na RA. Basically naweza kusema ni CCM ya RA na EL. JK ni boya tu amewekwa pale kama Mwenyekiti, lakini wenye final say ni akina EL na RA. Ndiyo maana hakuna lolote la maana linalofanyika, mikutano yao imekuwa ni kumbi za mipasho utadhani watu wako rusha roho pale Lango la Jiji.
Habari nilizozipata toka ndani ya Kikao cha Tume ya Mapatano na Maridhiano ya CCM na wabunge wake kilichomalizika jana hapa mjini Dodoma, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, ametema cheche na kukubali kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya Chama iwapo itaundwa tume huru kuthibitisha yale ya tume ya Mwakiembe.
Miongoni mwa Cheche alizotema, ni pamoja na kumlipua Spika Sitta kana kwamba ni kumkomelea msumari wa mwisho kuthibitisha chuki binafsi za Spika Sitta dhidi ya Edward Lowassa.
RA amesema Kamati ya Mwakiembe ni siasa chafu, ni ubia kati ya Spika Sitta na Mwakiembe dhidi ya Lowassa na Rostam.
RA anadai Six aliomba kwa El kupewa nyumba yenye hadhi yake Dar es Salaam na Dodoma pamoja na ofisi yenye hadhi, Urambo, EL alimtilia ngumu kuwa ni kinyume cha taratibu. Pia aliomba lami toka Urambo-Tabora na Motorcade lakini EL alimgomea, hivyo jamaa akawa na hasira na kutafuta upenyo wa kufanya visasi.
RA alishauri iundwe Public Inquery ikigundua kuhusika kwake, yeye atajiuzulu nyadhifa zake zote.
Hata hivyo, RA hakuzungumzia kabisa issue za Kagoda kama uthibitisho wa dhati kuwa hahusiki aslan.😡😡
Bantugbro haya ya kuanza kupachikana majina ya Mkuu wa idara yanatokea wapi?.Mkuu wa idara,
Wakati sisi tunakazania kukabana makoo na kulipiza visasi, waungwana Maalim na A.K wameamua kukutana faragha na kupata gahawa kidogo! (tutazamie Azimio la Zenji Party II?) nadhani washajionea kuwa nchi hii haina mwelekeo tena mara leo E.L kesho R.A kesho kutwa lioness Sofia. Hivi nani ni nani? nani wakuleta order katika nchi hii kwa sasa? inasikitisha kwakweli..
Amani.
Naye Rostam Azizi alisema ni jambo la aibu wabunge wa CCM kuitwa mbele ya kamati ya wazee wa CCM na jambo hilo akasema halifai kujivunia kwani linaonesha namna chama hicho kilivyogawanyika. Alisema tuhuma juu ya kampuni ya Kagoda inayodaiwa kuwa ni yake hazina ukweli wowote na wanaofanya hivyo wanamsulubu bure kwani si ajenda ya CCM bali ni ya Chadema, akashangaa iweje wabunge wa CCM washikie bango jambo ambalo si ajenda yao. Alisema kwamba yeye anaamini kuwa kumsulubu yeye au Lowassa juu ya suala la Richmond ni kukikusulubu chama.
Rostam pia anadai kusema kwamba mpasuko kati ya wabunge na wabunge wa chama hicho ni uchaguzi wa mwaka 2005 baada ya watu kushindwa kupata urais ndipo wakaanzisha vita na kundi la watu ambao waliingia madarakani.
Kuhusu ripoti ya Richmond, Rostam alisema tangu mwanzo kulikuwa na hila mbaya ndio maana yeye alinyimwa fursa ya kutoa maoni yake mbele ya kamati hiyo.
Lakini Rostam pia alienda mbali na kutaka chama kuanzia sasa kiwachukulie hatua kali wabunge wanaoikosoa Serikali. Kuhusu kuumizwa kwake kisiasa alisema licha ya kuwa ameumizwa sana kuhusu jambo hilo yeye tayari ameshasamehe, kwani Mungu amemjaalia moyo wa kusamehe.
.Mkuu Mkandara,
Hoja yako ndiyo niliipigia sana kelele zama zile za msuguano wa wana-Kyela mara baada ya mwana JF kutangaza nia ya kugombea.
Kwa mazingira yaliyopo ndani ya CCM hivi sasa, kweli mtu ambaye ana nia ya dhati ya kuleta mabadiliko anaweza kwenda kugombea kupitia CCM? How many times wabunge wa CCM wamefungwa midomo wasiseme maovu ya wenzao ama ya serikali? Tena wengine kwa kutishiwa maisha.
Hivi kweli tuhuma inamhusu Makamba, ama RA au EL, utaingia kwenye vile vikao vya wabunge wa CCM uombe ridhaa ya kuongelea hoja hiyo Bungeni na uruhusiwe? Nape Nnauye isingekuwa huruma ya Muungwana leo hii asingekuwa mwana UVCCM wala mwana CCM, kisa aligusa tuhuma za kigogo wa CCM. Chama kimejaa untouchables (miungu watu) ambao hutakiwi kuwasema wala kwenda kinyume nao vinginevyo unaweza kufungishwa virago.
Hao wanaoitwa wapiganaji wameibuka kuinusuru CCM baada ya kuona chama kinapoteza umaarufu mbele ya wananchi. Baada ya Dr. Slaa kumwaga radhi ya LIST OF SHAME na Zitto kupeleka hoja ya Buzwagi ndipo akina Mama Kilango wakaibuka. Mama Kilango akiwa Bungeni alisema hawezi kukubali akae kimya awaachie akina Slaa na Zitto wapate umaarufu kwa kuibua kashfa na hoja nzito nzito, kisa anaogopa kushughuliwa na Chama ama serikali. Je, leo hii hao wapiganaji wanaitwaje ndani ya CCM? Hata kama una ka-doa kidogo, unaweza kujikuta unatwishwa kashfa ya mwaka 1947 ili kukunyamazisha usiseme. Ukiwauliza walikuwa wapi hawakukushughulikia, hawana jibu la kukupa.
Sasa hivi kamati ya Mzee Mwinyi inatapatapa tu, hawajui watachukua kipi waache kipi. Mama Simba tayari ameishasema ndani ya CCM hakuna aliye msafi, kwa hiyo hata yeye mwenyewe ni mchafu na JK nae ni mchafu. Kauli hiyo ina maana kubwa sana kwa wale wenye nia ya kuingia kwenye siasa.
Nikimsikia kijana anasema anakwenda kugombea Ubunge kupitia CCM ninamuona ni opportunist tu kwa kuwa kama yeye ana nia safi na dhamira njema, hawezi kwenda kujichanganya na waliovunda ama kuoza kabisa. Hivi kweli kama mtu ni msafi anaweza kwenda kukaa jalalani ama kujichanganya na wachafu? Umeambiwa kabisa hili ni jalala, ni sehemu iliyojaa takataka, bado mtu anakwenda kukaa hapo hapo. Hapo lazima ujiulize sana kama kweli mtu huyo ana nia na dhamira ya kweli ya kuwatumikia wananchi.
Hivi, ili ushinde Ubunge ni lazima upitie CCM? This is the opportune time for young men and women who wish to vie for MP posts kuingia kazini kumwaga sera za kueleweka. Unajua huu uchafu ambao CCM wanapakana sasa hivi utakuja kuwasumbua sana kuusafisha ikifika 2010, labda kwa kuwa ni mafisadi watatumia hela za ufisadi ili washinde. Lakini kama kuna mtu yuko serious na mapambano ya kweli, watanzania wa sasa wanasomesheka vizuri tu na wanaelewa. Ujinga unaoendelea ndani ya CCM ni faida kwa upinzani na wale wanaotaka kuingia kwenye siasa kupitia upinzani.
Mabadiliko ya kweli hayataletwa na hii CCM ya JK, EL na RA. Basically naweza kusema ni CCM ya RA na EL. JK ni boya tu amewekwa pale kama Mwenyekiti, lakini wenye final say ni akina EL na RA. Ndiyo maana hakuna lolote la maana linalofanyika, mikutano yao imekuwa ni kumbi za mipasho utadhani watu wako rusha roho pale Lango la Jiji.
NB: Kumradhi mwana JF ambaye ulitangaza kugombea kupitia CCM. Niliahidi kwamba ukishinda Ubunge nitaendelea kukumbusha mabandiko yako ya hapa ndani, unless na wewe upotee kama akina Dr. James Msekela ambao kwenye TANZANET walionekana wafurukutwa na walipoingia kwenye system wamemezwa na wamekuwa mute kama hawapo.
Mkandara, sisi wana JF tunagombea kipande cha mkate na nani ili tushibe?mbona tunapiga kelekele kila siku?Mtanzania,
Mkuu wangu kwanza pole sana.. ndio siasa za Bongo hizo kwani hakuna jimbo lolote unaloweza gombea kwa tiketi ya CCM ukawa salama - HAKUNA..hivyo sii tu kina Sitta na Mwakyembe isipokuwa ni tabia zenu nyote kama chama. Sitta na Mwkayembe wote wamepata upinzani toka vyama vya Upinzani hna sikuona mauaji au kitu kinachokaribia hivyo. Utanisamehe nitakuja strong kidogo kukupa changamoto!
Nina swala, hivi Katika kujisafisha wewe... Je, unaweza kusema wazi EL na RA ni Mafisadi?.. au usafi ni wa mwili wako na sii kauli..Hivi Unafiki wa mtu ni usafi au?.. sasa kama wewe unataka kujisafisha nakuomba ulaani vitendo vya kina Lowassa, Rostam na wengine wote kwani usafi wa mtu huanza kwa kufahamu matendo mabaya..Hivi ukiona mtu kaua inabidi usireport hadi wewe utakapo kisafisha na makosa ya uasherati au kuchukua posho mbili!
Tofauti kubwa ya WApiganaji na wengine wote ni kwamba hawa wanatoa report ktk vyombo vya sheria na hao kina RA wanazungumza haya pembeni kazi kuita waandishi wa habari wakidai wapiganai nao sii wasafi...
Mkuu wangu tatizo lako na hao kina Mwakyembe na Sitta mnagombea kipande cha mkate ambacho kila mmoja wenu ndio shibe yake. has no interest in political balance towards social harmony and common good, na ndicho nilichjokiona hapa JF.. Kifupi mkuu wangu utanisamehe lakini usafi ungeuanza hapa JF, kila nilichosoma ktk kuburuzana kwenu nimewasoma kama ni selfintrest zaidi..Kila mmoja wenu anarusha magumi pasipo kukubali kujitazama yeye. It's been wewe hivi wewe vile, mimihivi mimi vile, na hakuna mmoja wenu anayekubali kujitazama na kutambua mapungufu yake..
Mwakyembe na Sitta wanaweza kutokuwa wasafi, but they represent our problem na our needs Kitaifa, hivyo sifa zangu kwa Sitta na Mwakyembe ni ktk maswala yanayolihusu taifa zima.. Hayo ya Kyela nawaachia wana Kyela.
Na kusema kweli nimeshindwa sana kukupa support moja kwa moja kwa sababu Mpiganaji wa kweli hujiunga Upinzani kwa lugha yangu kuwa Conservative kifikra ili upate kuisafisha system ilinayowabeba Mafisadi..Haramu ni Ufisadi, na ndicho kinachotakiwa kupigwa vita.. Usafi wa mtu unaanza na nafsi,uwezo wa kutambua mabaya na ukayakemea.
Kama ndio ingekuwa hivyo tusingekuwa na Mapadre, Masheikh na kadhalika wakitoa mawaidha na kufundisha neno la Mungu..Miyume wenyewe hawakuwa perfect ama niseme wasafi..kwanza hakuna mtu msafi na ndio maana tumeunda sheria, magereza na vyombo vya usalama.. Hiyo ndio kazi yao.. Sitta au Mwakyembe aren't clean wapelekeni ktk vyombo vya sheria..Na kama haiwezekani then system nzima inafail, systema mbayo wewe unataka kujiunga nayo..
Kama unataka kugombea Ubunge kwa sababu huridhiki na hali halisi ya Utawala uliopo na unataka kuleta mabadiliko ktk utawala basi jiunge na Upinzani wa sio kuwaletea wananchi mfumo ule ule wanaoupiga vita..Kyela haikuanza kutawaliwa na Mwakyembe, mapungufu ya Kyela hayakuanza miaka mitano iliyopita isipokuwa ni mlolongo wa viongozi wa CCM waliwakilisha wananchi wa Kyela kushindwa kuwaletea mabadiliko..And I believe wee pia utakuwa katika hesabu ya viongoz hao kwani changes haziletwi na kichwa kimoja isipokuwa policies za chama kinachoongoza.
lakini kama unagombea kwa sababu ya Mwakyembe au malalamiko ya wana Kyela, hapo mkuu wangu usiyachukulie mawazo yangu kwa uzito hivyo kwani all what ai'm for Upinzani wa system nzima iliyopo na sii WATU. Wapiganaji wana represent Upinzani na sii Upinzani wa jina la mtu...
Bantugbro haya ya kuanza kupachikana majina ya Mkuu wa idara yanatokea wapi?.
Hili la kukutana Maalim na AK ni ishara nzuri sana kwa siasa za Zanzibar. CUF itangaze kumtambua AK kama rais wa ZNZ, Karume awateu wale wawakilishi wawili wa CUF barazani akiwemo Juma Duni kwa kipindi kifupi kilichobakia, utekelezaji wa muafaka uridhiwe, ZNZ mambo mswano, kazi sasa ni huku kwetu bara, 2010 moto!
Huyu ROSTAM AZIZ ndiye aliyeifikisha nchi hapa ilipo. Ni mgeni aliyekuja kutoka Uajemi ili kuwaangamiza watanzania baada ya kuwapora raslimali zao akishirikiana na watu wenye uroho wa utajiri wa kupindukia kama vile LOWASSA. Hawa wengine wanaom-support kama Sofia Simba, Makongoro Mahanga, Kingunge, n.k. wanaambulia makombo tu ya akina ROSTAM na LOWASSA.
Tunafahamu 'war chest' yao ni kubwa na ndio maana unaona watu kama akina Sofia Simba wanaropoka ovyo na kujishushia hadhi kwani wana uhakika wa malipo mazuri kwa kazi yao chafu.
Sasa sisi wana wa nchi hii tunasema hivi: Enough is enough! Tunaingia rasmi kwenye mapambano ya kutetea uhuru wetu na raslimali zetu. Kwa wale wapiganaji wa kweli maelekezo yatafuata... Stay tuned.
Kwako wewe huo utumbo aliosema rostam ndio AMETEMA CHECHE!!! and you invite us to share that gabbage!you r so foolish!!!Habari nilizozipata toka ndani ya Kikao cha Tume ya Mapatano na Maridhiano ya CCM na wabunge wake kilichomalizika jana hapa mjini Dodoma, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, ametema cheche na kukubali kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya Chama iwapo itaundwa tume huru kuthibitisha yale ya tume ya Mwakiembe.
Miongoni mwa Cheche alizotema, ni pamoja na kumlipua Spika Sitta kana kwamba ni kumkomelea msumari wa mwisho kuthibitisha chuki binafsi za Spika Sitta dhidi ya Edward Lowassa.
RA amesema Kamati ya Mwakiembe ni siasa chafu, ni ubia kati ya Spika Sitta na Mwakiembe dhidi ya Lowassa na Rostam.
RA anadai Six aliomba kwa El kupewa nyumba yenye hadhi yake Dar es Salaam na Dodoma pamoja na ofisi yenye hadhi, Urambo, EL alimtilia ngumu kuwa ni kinyume cha taratibu. Pia aliomba lami toka Urambo-Tabora na Motorcade lakini EL alimgomea, hivyo jamaa akawa na hasira na kutafuta upenyo wa kufanya visasi.
RA alishauri iundwe Public Inquery ikigundua kuhusika kwake, yeye atajiuzulu nyadhifa zake zote.
Hata hivyo, RA hakuzungumzia kabisa issue za Kagoda kama uthibitisho wa dhati kuwa hahusiki aslan.😡😡
hata hao wa mjini wenye uelewa mkubwa hawapigi kura na wakienda kupiga kura wanasema sasa mimi nimpigie nani "bora zimwi ulijualo".
Keil umenena, niko nyuma yako kwa asilimia 100% but only if Watanzania wa vijijini nao watafunguliwa macho na masikio yao, kwanza kwa kuelimishwa kuwa CCM haina hati miliki ya kuitawala nchi hii na mwenye uamuzi wa mwisho ni mwananchi mwenyewe. Watu waone madudu ya CCM na Kusikia huyo mbadala anakuja na ahadi gani.
Thanks.Kwako wewe huo utumbo aliosema rostam ndio AMETEMA CHECHE!!! and you invite us to share that gabbage!you r so foolish!!!
...thanks too.Thanks.
..halafu jifunze kuandika majina ya watu vizuri!! ulisoma wapi wewe darasa la kwanza??Habari nilizozipata toka ndani ya Kikao cha Tume ya Mapatano na Maridhiano ya CCM na wabunge wake kilichomalizika jana hapa mjini Dodoma, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, ametema cheche na kukubali kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya Chama iwapo itaundwa tume huru kuthibitisha yale ya tume ya Mwakiembe.
Miongoni mwa Cheche alizotema, ni pamoja na kumlipua Spika Sitta kana kwamba ni kumkomelea msumari wa mwisho kuthibitisha chuki binafsi za Spika Sitta dhidi ya Edward Lowassa.
RA amesema Kamati ya Mwakiembe ni siasa chafu, ni ubia kati ya Spika Sitta na Mwakiembe dhidi ya Lowassa na Rostam.
RA anadai Six aliomba kwa El kupewa nyumba yenye hadhi yake Dar es Salaam na Dodoma pamoja na ofisi yenye hadhi, Urambo, EL alimtilia ngumu kuwa ni kinyume cha taratibu. Pia aliomba lami toka Urambo-Tabora na Motorcade lakini EL alimgomea, hivyo jamaa akawa na hasira na kutafuta upenyo wa kufanya visasi.
RA alishauri iundwe Public Inquery ikigundua kuhusika kwake, yeye atajiuzulu nyadhifa zake zote.
Hata hivyo, RA hakuzungumzia kabisa issue za Kagoda kama uthibitisho wa dhati kuwa hahusiki aslan.😡😡